1:Miller hakukosea Muda ila alikosea tukio. Na hata yeye alikuwa hana imani kuubwa kuhusu timing/Time setting ndio maana usiku ule wa tarehe 22 alitoa kauli kuonyesha mashaka kuhusu kuja kwa Yesu maana alikumbukia kauli ya Yesu '' Hamjui siku wala saa''.
2: Hiyo formula sio ya Kisabato, maana hata miller hakuwa msabato, na wafuasi wake hawakuwa wasabato (SDA).
Pili Miller hakuasisi hiyo formula, Bali ni formula ya kibibilia. Imetumika siku nyingi kabla hata ya mwaka 1000 kung'amua kuwa mpinga kristo anayezungumzwa kwenye daniel na Ufunuo ni Upapa au atatokana na Roman empire. Aliitumia Daniel kuwakumbusha waisrael wasrael kuwa muda wao wa miaka 70 umepita warudi kwa israel kutoka babeli, waliitumia majusi waarabu kujua Yesu anazaliwa wakati huo maana Ilishatabiriwa. Aliitumia Jerome kusema mpingakristo ataibuka baada ya kuanguka kwa Dola la kirumi. Wanaitumia Wasabato SDA kutafsiri unabii wa siku za Mwisho. Haionyeshi siku ya Kuja kwa Yesu maana Yesu alishasema hakuna hajuae ila alitoa dalili za kuja kwake.
3:Hilo Swali wakiulizwa wao watatoa jibu zuri. Ila kwa Mujibu wa hata vikao vyao, mfano 1840 pale boston walikuwepo watu waliosimamia kauli ya Yesu kuwa hajui siku wala saa. Hata ile conference ya 1942 qualification ya kuingia ilikuwa uamini Yesu anakuja tena haraka ila sio lini, kwa sababu baadhi yao walikuwa na mashaka na time setting. Pia kama nilivyoonyesha hapo juu hata siku moja kabla ya disapointment hata miller mwenyewe alikuwa na mashaka kuhusu time setting ila alikuwa na uhakika kuwa Yesu anakuja upesi mno kwa mujibu wa ukokotozi wa kimakosa wa unabii.
4:Hawakuasisi formula, walitumia formula iliyokuwepo miaka yote, Hata critics wao baadhi waliwashangaa kwa kutumia formula hiyohiyo.
Kwa nini waamini Yesu angekuja, hapo ninasema walikosea. Na sio wakristo wa kwanza kukosea. Walianza Mitume kukosea kuwa Yesu amekuja kuwapa utawala wa kidunia hadi mama zao yohana akawaombea vyeo kwenye utawala wao. Lkn hatujakataa Ukristo kwa sababu waliwahi kukosea bali kwa sababu walielewa walikosea wapi na kuendeleza ukweli wa bibilia. Ndio Maana SDA tangu imekuwepo 1863 haijawahi kumfundisha mtu yoyote kuwa Yesu anakuja siku flani exactly. Ila wanafundisha kwa peni na mdomo Yesu anakuja Upesi sana. Tena tofauti na uongo wa kuwa anakuja katika roho sijui si katika mwili. Wanafundisha anakuja katika mwili na kila jicho litamuona. anakuja kwa kuonekana kama alivyoondoka kwa kuonekana.
5:Hili alina msingi, maana hellen alikuwa mbaptist hakuwa msabato enzi akiwa mfuasi wa miller. Mungu alianza kumtumia baada ya great dissapointment. Hakuna msabato wala E.G White anayesema Yesu amemwambia anakuja lini kwa maana ya tarehe. Badala yake Wasabato SDA na Hellen White mwenyewe wanapiga marufuku Kuweka Muda wa Kuja kwa Yesu tangu wamekuwepo.
6: Day Year principle ya kutafsiri unabii nimeshasema sio ya miller wala helen bali ni ya kwenye bibilia. Unabii wa Daniel hautabili kuja kwa Yesu bali Matukio ya kabla ya Kuja kwake. Hivyo Miller alikosea kuweka timing, EGW kama miongoni mwa wafuasi tena akiwa sio msabato alikuwa anapitishwa katika uzoefu na baada ya kufunuliwa na kupata maarifa na anapiga marufuku time seting katika maandishi yake. Yeye sio wa kwanza hata Petro alikuwepo wakati Yesu anasema enendeni ulimwenguni kote mkaihubiri injili lkn ni petro huyohuyo aliyedhani Yesu alimaanisha wayahudi tu hadi kuwatenga wakina kornelio. na sio yeye tu kanisa zima hadi Mungu alipowafunulia. Mjinga ataweka kambi kwenye makosa ya Uelewa, ila mwerevu atashikamana na ufahamu mpya wa kweli wa kimaandiko.
7:Swali hili limejengwa katika upotofu. Na nadhani limewalenga wasio na maarifa na taarifa za kutosha kuhusu anasachosema EGW. maandiko yake yake yako wazi akipinga time setting. Kuhusu Yesu kushuka kufika chumba flani, Sentensi hiyo imekuwa calculated kupotosha kuwa Yesu Yuko njiani kwenye kachumba flani. Fundisho la SDA kuhusu Patakatifu ambapo image yake imeelezwa vzr katika Vitabu vya walawi, na waebrania liko wazi Mambo Yote ya Utakaso Yanayofanyika Mbinguni Yako Mbinguni ha hayana Uhusiano na Yesu Kushuka kuikaribia dunia, Bali yanauhusiano na Kumaliza kazi yake ambayo Hata Yeye anasema hajui itamalizika lini ila katuachia dalili sio siku. Na huu ndio msimamo wa EGW hadi anakufa, na Ndio Msimamo wa SDA na ndio msimamo wa Bibilia na Mitume Kuwa Yesu anakuja upesi ila Japo hatujui saa ila dalili ziko wazi.
Mkuu Zitto Jr sina wasiwasi na uwezo wa kupotosha wa mkuu Sanctus maana sio mara ya kwanza kukutana naye humu kwenye mijadala na bahati mbaya huwa haagi. Uwezo huo ni mkubwa kiasi kama hufuatilii matukio na kusoma katikati ya mistari unaweza kujikuta ukirushwa huku na kule na kila kama mtoto mdogo.
Fact Kuu ya Upotoshaji wa huyu bingwa ni, Miller alivumbua Formula ya kutafsiri kuja kwa Yesu au unabii wa Daniel wakati formula hiyo miaka Yote kabla hazijavumbuliwa na majesuits formula zingine mbili katika kipindi cha counter-reformation.
Preterism school of interpretation and Futurism school of interpretation zilizobuniwa na majesuit wakina fransisco ribera Robert Bellamine, Luis De Alcaser. Hii ilikuwa katika harakati za kudivert tuhuma za reformers kuwa pope is antichrist, na hata walokole wengi wameingia kwenye huu mtego.
Kama Msingi ni HISABATI alizotumia Miller basi Hakuzitunga yeye, Kama msingi ni Kuja kwa Yesu Miller alikosea, na White kabla ya kujua ukweli alikosea. Hata mimi ningekuwa hai nisingekubaliana nao, Ila nakubaliana na Msimamo wa white na SDA kuhusu kuja kwa Yesu maana 100% ni biblical supported.
Mbarikiwe Wakuu mbalimbali.
cc
SANCTUS ANACLETUS
Otorong'ong'o
karibuni kwa hoja mbalimbali wakuu.