William Miller: Kama Yesu hakujua Hisabati au kutafsiri mambo bora angalikaa Kimya. Mbona siku ya mwisho wa dunia inakokotoleka kirahisi?

Anaishi kukarili siyo anachojua
Mzee wa vijarida,
Nadhani alipokuwa mtoto gheto lake lilijaa magazeti ukutani asee,maana ndo ubongo wake

Ni shida sana. Ila kuna siku zinakuja watalaumu hii mitandao maana wengi wanafunguliwa
 
Kama William ana akili basi ajikokotolee siku za Kuishi na kuondoka hapa Duniani.
 
Okay naona mkuu SANCTUS ANACLETUS ameacha maswali ya kuongoza mjadala ambayo ungesaidia kuyajibu kwa faida ya wengi labda niyapaste upya

Kwa kuisoma Sadikifu (thesis) ya Miller na msimamo wa Yesu juu ya mwisho wa dunia,yafuatayo yanajitokeza:

1. Miller na wenzie walikosea wapi katika fomula yao kiasi kwamba Yesu hajawahi kuonekana toka mwaka 1843?

2. Je, wanahisabati wanaweza kuendeleza pale Miller na wenzie walipoishia katika kukokotoa mwisho wa dunia kwa kuihakiki hiyo fomula ya Kisabato juu ya kurudi kwa Yesu?

3. Je, Miller na wenzie hawakuwa wamefanikiwa kulisoma Agano Jipya ambamo msimamo wa Yesu juu ya tarehe ya mwisho wa dunia unawekwa wazi wazi kuwa tarehe husika haijulikani?

4. Je, ikiwa Miller na wafuasi wake akiwemo Mama wa “maono”,Ellen White, walikuwa wamelisoma Agano Jipya ni kwa nini wao waliamua kuasisi Fomula ya jambo ambalo Yesu alikwisha kusema hana uwezo nalo?

5. Je, kwa Yesu kusema haijui tarehe halafu Miller na Ellen White wakaja wakasema wanaifahamu tarehe ina maana Wasabato hao na wa leo mbingu ni yao kiasi kwamba wanaingia na kutoka hata wameweza kushirikishwa yanayoendelea huko Mbinguni?

6. Je, kwa Miller na Ellen kukubaliana kwamba wao walikuwa wameipata fomula ya kurudi kwa Yesu walimaanisha kwamba wao walikuwa ni wasomi sana na kwamba Yesu kusema haijui tarehe kulimaanisha Yesu alikisoma Kitabu cha Daniel na kutokikielewa au kwamba Yesu alikuwa anasoma mambo kwa kurukaruka?

7. Je, hadi sasa tumsikilize nani kati ya Yesu na wasabato juu ya mwisho wa dunia kwa sababu Ellen White ameshapewa maono yanayoonyesha kwamba Yesu ameshaanza kushuka na kwamba kwa sasa yuko katika chumba cha patakatifu pa patakatifu sana ambako anapitia majina ya wasabato na akitoka hapo moja kwa moja anatia timu hapa duniani?

Kwa yote hayo,sasa KARIBUNI kwa mjadala.
1:Miller hakukosea Muda ila alikosea tukio. Na hata yeye alikuwa hana imani kuubwa kuhusu timing/Time setting ndio maana usiku ule wa tarehe 22 alitoa kauli kuonyesha mashaka kuhusu kuja kwa Yesu maana alikumbukia kauli ya Yesu '' Hamjui siku wala saa''.

2: Hiyo formula sio ya Kisabato, maana hata miller hakuwa msabato, na wafuasi wake hawakuwa wasabato (SDA).
Pili Miller hakuasisi hiyo formula, Bali ni formula ya kibibilia. Imetumika siku nyingi kabla hata ya mwaka 1000 kung'amua kuwa mpinga kristo anayezungumzwa kwenye daniel na Ufunuo ni Upapa au atatokana na Roman empire. Aliitumia Daniel kuwakumbusha waisrael wasrael kuwa muda wao wa miaka 70 umepita warudi kwa israel kutoka babeli, waliitumia majusi waarabu kujua Yesu anazaliwa wakati huo maana Ilishatabiriwa. Aliitumia Jerome kusema mpingakristo ataibuka baada ya kuanguka kwa Dola la kirumi. Wanaitumia Wasabato SDA kutafsiri unabii wa siku za Mwisho. Haionyeshi siku ya Kuja kwa Yesu maana Yesu alishasema hakuna hajuae ila alitoa dalili za kuja kwake.

3:Hilo Swali wakiulizwa wao watatoa jibu zuri. Ila kwa Mujibu wa hata vikao vyao, mfano 1840 pale boston walikuwepo watu waliosimamia kauli ya Yesu kuwa hajui siku wala saa. Hata ile conference ya 1942 qualification ya kuingia ilikuwa uamini Yesu anakuja tena haraka ila sio lini, kwa sababu baadhi yao walikuwa na mashaka na time setting. Pia kama nilivyoonyesha hapo juu hata siku moja kabla ya disapointment hata miller mwenyewe alikuwa na mashaka kuhusu time setting ila alikuwa na uhakika kuwa Yesu anakuja upesi mno kwa mujibu wa ukokotozi wa kimakosa wa unabii.

4:Hawakuasisi formula, walitumia formula iliyokuwepo miaka yote, Hata critics wao baadhi waliwashangaa kwa kutumia formula hiyohiyo.
Kwa nini waamini Yesu angekuja, hapo ninasema walikosea. Na sio wakristo wa kwanza kukosea. Walianza Mitume kukosea kuwa Yesu amekuja kuwapa utawala wa kidunia hadi mama zao yohana akawaombea vyeo kwenye utawala wao. Lkn hatujakataa Ukristo kwa sababu waliwahi kukosea bali kwa sababu walielewa walikosea wapi na kuendeleza ukweli wa bibilia. Ndio Maana SDA tangu imekuwepo 1863 haijawahi kumfundisha mtu yoyote kuwa Yesu anakuja siku flani exactly. Ila wanafundisha kwa peni na mdomo Yesu anakuja Upesi sana. Tena tofauti na uongo wa kuwa anakuja katika roho sijui si katika mwili. Wanafundisha anakuja katika mwili na kila jicho litamuona. anakuja kwa kuonekana kama alivyoondoka kwa kuonekana.

5:Hili alina msingi, maana hellen alikuwa mbaptist hakuwa msabato enzi akiwa mfuasi wa miller. Mungu alianza kumtumia baada ya great dissapointment. Hakuna msabato wala E.G White anayesema Yesu amemwambia anakuja lini kwa maana ya tarehe. Badala yake Wasabato SDA na Hellen White mwenyewe wanapiga marufuku Kuweka Muda wa Kuja kwa Yesu tangu wamekuwepo.

6: Day Year principle ya kutafsiri unabii nimeshasema sio ya miller wala helen bali ni ya kwenye bibilia. Unabii wa Daniel hautabili kuja kwa Yesu bali Matukio ya kabla ya Kuja kwake. Hivyo Miller alikosea kuweka timing, EGW kama miongoni mwa wafuasi tena akiwa sio msabato alikuwa anapitishwa katika uzoefu na baada ya kufunuliwa na kupata maarifa na anapiga marufuku time seting katika maandishi yake. Yeye sio wa kwanza hata Petro alikuwepo wakati Yesu anasema enendeni ulimwenguni kote mkaihubiri injili lkn ni petro huyohuyo aliyedhani Yesu alimaanisha wayahudi tu hadi kuwatenga wakina kornelio. na sio yeye tu kanisa zima hadi Mungu alipowafunulia. Mjinga ataweka kambi kwenye makosa ya Uelewa, ila mwerevu atashikamana na ufahamu mpya wa kweli wa kimaandiko.

7:Swali hili limejengwa katika upotofu. Na nadhani limewalenga wasio na maarifa na taarifa za kutosha kuhusu anasachosema EGW. maandiko yake yake yako wazi akipinga time setting. Kuhusu Yesu kushuka kufika chumba flani, Sentensi hiyo imekuwa calculated kupotosha kuwa Yesu Yuko njiani kwenye kachumba flani. Fundisho la SDA kuhusu Patakatifu ambapo image yake imeelezwa vzr katika Vitabu vya walawi, na waebrania liko wazi Mambo Yote ya Utakaso Yanayofanyika Mbinguni Yako Mbinguni ha hayana Uhusiano na Yesu Kushuka kuikaribia dunia, Bali yanauhusiano na Kumaliza kazi yake ambayo Hata Yeye anasema hajui itamalizika lini ila katuachia dalili sio siku. Na huu ndio msimamo wa EGW hadi anakufa, na Ndio Msimamo wa SDA na ndio msimamo wa Bibilia na Mitume Kuwa Yesu anakuja upesi ila Japo hatujui saa ila dalili ziko wazi.

Mkuu Zitto Jr sina wasiwasi na uwezo wa kupotosha wa mkuu Sanctus maana sio mara ya kwanza kukutana naye humu kwenye mijadala na bahati mbaya huwa haagi. Uwezo huo ni mkubwa kiasi kama hufuatilii matukio na kusoma katikati ya mistari unaweza kujikuta ukirushwa huku na kule na kila kama mtoto mdogo.

Fact Kuu ya Upotoshaji wa huyu bingwa ni, Miller alivumbua Formula ya kutafsiri kuja kwa Yesu au unabii wa Daniel wakati formula hiyo miaka Yote kabla hazijavumbuliwa na majesuits formula zingine mbili katika kipindi cha counter-reformation.
Preterism school of interpretation and Futurism school of interpretation zilizobuniwa na majesuit wakina fransisco ribera Robert Bellamine, Luis De Alcaser. Hii ilikuwa katika harakati za kudivert tuhuma za reformers kuwa pope is antichrist, na hata walokole wengi wameingia kwenye huu mtego.
Kama Msingi ni HISABATI alizotumia Miller basi Hakuzitunga yeye, Kama msingi ni Kuja kwa Yesu Miller alikosea, na White kabla ya kujua ukweli alikosea. Hata mimi ningekuwa hai nisingekubaliana nao, Ila nakubaliana na Msimamo wa white na SDA kuhusu kuja kwa Yesu maana 100% ni biblical supported.

Mbarikiwe Wakuu mbalimbali.
cc
SANCTUS ANACLETUS
Otorong'ong'o

karibuni kwa hoja mbalimbali wakuu.
 
Mtoa hoja ni ama anahitaji kushinda au Shetani amekifunga kichwa chake na minyororo mizito hata asisikilize maandiko ya Biblia yaliyotolewa humu kama majibu ya hoja yake.

Kama mkristo anakosoa Biblia (mfono: habari za hekalu la mbinguni ama Yesu kuwa kuhani mkuu) tutumie ushahidi upi sasa ?

Kujifunza Biblia ni utamaduni wa mwadventista msabato tangu unapozaliwa hadi kufa . Mkatoliki yeye ni "Mithale ya waumini" (yaani mafunzo ambayo kanisa limekusudia tu yaende kwa waumini).

Kama unahoji maandiko safari yako ni nyingine maana hata Yesu mwenyewe aliyaishi hayo maandiko
 
Alichokuwa anakiona Yohana katika ndoto kuliashiria jambo jingine halisi. Kwa mfano anasema aliona Mwanamke amevikwa Jua,Nyota na Mwezi. Kwa hiyo huwezi kusema ni kweli kuna mtu anaweza kuvaa Jua au Nyota. Kumbe hayo maono kila moja lilikuwa na maana yake ambayo Kanisa la Mwanzo walikuwa wakielewa maana yake. Kimsingi lugha na staili aliyotumia ni lugha ya mafumbo iitwayo APOCALYPTIC. Ilikuwa ni lazima Yohana awasiliane na wanakanisa katika lugha hiyo ili kumkwepa Kaizari NERON ambaye ndiye leo wasbato mnasema ni PAPA ajaye.
Uelewa wako ni mdogo sana katika maandiko. Haya mambo yanahitaji usaidizi wa Roho mtakatifu na wali siyo ujuaji wa kuungaunga.

Kwa mtazamo huo wa codes za mawasiliano za kina Yohana, je katika unabii wa Daniel yeye alikuwa anamuogopa nani na alikuwa anawasiliana na nani?

Kwa mtazamo wako ni kwamba habari za kitabu cha Ufunuo hazituhusu?
 
TAFSIRI YA MNYAMA WA PILI WA UFUNUO 13.

“Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka.” Ufunuo 13:11. Bwana Wesley, katika maelezo juu ya Ufunuo 13 aliyoandika mwaka 1754, akizungumzia mnyama mwenye pembe mbili; “Hajaja bado, japo hawezi kuwa mbali sana: kwa maana amekusudiwa kuonekana mwishoni mwa miezi arobaini na miwili ya yule mnyama wa kwanza.”

Mnyama wa kwanza alipanda kutoka kwenye bahari, ambayo inaonyesha kuinuka kwake kutoka katika watu wengi na mataifa mengi ya wakati huo (Ufunuo 17:5), wakati huyu wa pili anainuka kutoka katika nchi. Hii inaonyesha kuwa mnyama wa pili angetokea mahali ambapo hapakuwa na watu wengi, wala mataifa, lugha na jamaa. Mwaka 1798, wakati mamlaka ya kipapa yalipotiwa jeraha la mauti, utawala wake ulienea maeneo yote muhimu ya Ulaya, Asia na Afrika; na mahali pekee kwa ajili ya mnyama wa pembe mbili kuendelea palikuwa ni bara la magharibi. Tukilitazama hili bara tunaona marekani ndilo taifa huru lililokuwa na idadi ndogo ya watu kwa wakati huo. Taifa la Marekani lilijitangazia uhuru wake kutoka kwa mkoloni mwingerza tarehe 4 Julai 1776. Hivyo wakati papa Pius VI akichukuliwa kwenda uhamishoni, taifa la Marekani lilikuwa likikua na kujiimarisha.

Pembe huwakilisha utawala au sehemu ya utawala, kama ilivyoainishwa katika Danieli 7:7, 8, 24, 25. Pembe kama za mwana-kondoo zinaonyesha uchanga, kutokuwa na hatia na upole. Soma Great controversy, 442. Pembe mbili zaweza kuwakilisha kanuni zilizoongoza serikali, uhuru wa kisiasa na kidini.

Mbali na kuwa na pembe mbili kwa maana kwamba dini na serikali ni vitu viwili tofauti, mnyama huyu baadae alikuja kunena kama joka! “Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.” Ufunuo 13:12. Sifa kuu ya upapa ilikuwa ni kuunganisha dini na serikali. Kanisa lilipoasi huko zamani likatafuta msaada kwa serikali na hivyo kutumia serikali kuwaadhibu wale ambao walijaribu kwenda kinyume na mafundisho ya kanisa. Ndipo tunasema upapa ulipata nguvu na mamlaka kutoka kwa yule joka. Joka aliwakilisha Shetani lakini kupitia serikali ya Rumi.

Taifa la marekani lilikuwa taifa la kiprotestanti tangu kuanzishwa kwake, na lilikuwa kimbilio kwa wakristo ambao walikimbia mateso kule Ulaya. Ni taifa ambalo lilikuwa na uhuru wa kidini, uhuru wa dhamiri, serikali haikuingilia mambo ya dini. Tarehe 7 Januari 1984, Raisi wa Marekani aliyekuwa madarakani, Ronald Reagan, alimteua balozi kuiwakilisha Marekani huko Vatican; huo ukawa mwanzo wa kujenga mahusiano baina ya Marekani ya kiprotestanti na upapa. Tangu hapo mahusiano baina ya pande hizi mbili yamekuwa yakiimarika siku baada ya siku ikiwemo viongozi kutembeleana. Na kama ilivyotabiriwa; katiba ya marekani imekuwa ikifanyiwa marekebisho kwa zaidi ya mara kumi na nne, lengo na kusudi ni kuondoa uhuru wa dhamiri, uhuru wa kidini, kuunganisha dini na serikali na hivyo taifa la Marekani lililokuwa la kiprotestanti litakuwa limefuata nyayo za Rumi na litakuwa limenena kama joka.

“Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu.” Ufunuo 13:13. Taifa la Marekani limekuwa kituo cha ishara na miujiza. Wahubiri wengi wenye kufanya miujiza wametokea katika taifa hili. Kunena kwa lugha kunakofanywa leo miongoni mwa wakristo kulianzia Marekani mwanzoni mwa miaka ya 1900. Watu wanadai kushukiwa na Roho mtakatifu lakini ukweli ni kwamba moto unaowaka ndani ya hawa watu siyo moto wa mbinguni bali ni moto wa kigeni! Vuguvugu la karismatiki ambalo linaenea kwa kasi miongoni mwa wakatoliki pia limeanzia katika taifa hili. Vuguvugu la kizazi kipya na wahubiri wakubwa wa mambo hayo chanzo chao ni Marekani. Dini nyingi za siri zinazomwabudu Lusifa zimeanzishwa katika taifa hili.

“Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi. Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.” Ufunuo 13:14-15. Juu ya sanamu ya mnyama, Ellen G White anaandika, “sanamu ya mnyama inawakilisha namna ya uprotestanti ulioasi ambao utaundwa wakati makanisa ya kiprotestanti yatakapotafuta nguvu ya serikali kwa ajili ya kushurutisha watu wafuate mafundisho yao ya dini” The great controversy ukurasa wa 445.

“Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.” Ufunuo 13:16-17. Baada ya makanisa ya kiprotestanti kuungana katika baadhi ya vipengele vya mafundisho ambavyo wanafanana hasa hasa ibada ya jumapili, yatashinikiza serikali kuweka sheria kwa kuifanya jumapili kuwa siku ya mapumziko na adhabu kutolewa kwa wale ambao watakiuka agizo hilo.

Kutiwa chapa katika mkono wa kuume ni kukubali kutii agizo kwa kutofanya kazi. Katika vipaji vya uso ni kusadiki au kuamini ya kwamba agizo hilo ni halali. Funuo 13:18, hesabu ya mnyama ni namba 666. Kofia ya papa imeendikwa kilatini "VICARIUS FILII DEI" ambayo tafasiri yake ni Vicar of the Son of God. Maana yake ni aliye badala ya Mwana wa Mungu. Ukilinyambulisha hilo neno VICARIUS FILII DEI kwa kutumia herufi za kirumi unapata jumla ya namba 666.
Hawa wakina SANCTUS kama wangekuwa wanasoma Biblia kwa unyenyekevu na kwa lengo la kujifunza haya mambo wangeyajua. Kwa mfano mambo mawili yanamhusu PAPA (ambaye ni mnyama aliyeandikwa katika kitabu cha Ufunuo
)
1. Alama ya mnyama=666

2. Kufuru = "badala mwana wa Mungu duniani"

Haya mambo hayawezi kuwa yametokea bahati mbaya

Huyu SANCTUS akane hapa kwa maandiko na kwa ushahidi wa kihistoria kwamba yale maandishi ya kofia ya papa hayafanyi jumla hesabu 666 au hayamaanishi "badala ya mwana wa mungu duniani"

Tena asije hapa akaanza kusema nimebadili maada. Kama anaijua hesabu ya Miller naamini anaelewa kuwa inahusisha ukatiri wa utawala wa kipapa kwa mamilioni ya wakristo. Na kama kweli ameisoma vizuri hesabu hii atakuwa anaelewa vizuri njinsi ambavyo unabii wa Daniel unavyoendana na unabii wa kitabu cha ufunuo.
 
Hawa wakina SANCTUS kama wangekuwa wanasoma Biblia kwa unyenyekevu na kwa lengo la kujifunza haya mambo wangeyajua. Kwa mfano mambo mawili yanamhusu PAPA
Uelewa wako ni mdogo sana katika maandiko. Haya mambo yanahitaji usaidizi wa Roho mtakatifu na wali siyo ujuaji wa kuungaunga.

Kujifunza Biblia ni utamaduni wa mwadventista msabato tangu unapozaliwa hadi kufa . Mkatoliki yeye ni "Mithale ya waumini" (yaani mafunzo ambayo kanisa limekusudia tu yaende kwa waumini).
kanisa katoliki lina mahali maalumu (vyuo vidogo na vya kimataifa) pa kufundishia, kusomesha na kujifunza kila kilicho muhimu katika theology na biblia kuanzia lugha zote za biblia, uandishi, jumbe, hija na research katika nchi na mahali pote ambapo vitabu vya biblia viliandikwa na kutumika. na mifano ya vyuo hivyo ni

Pontifical University urbanian -ROME
Innsbruck University - AUSTRIA
St joseph's College -washington DC
Pontifical biblical Institute - ROME
Lateran University - ROME
NK

sasa ninyi ambao mnadai kuwa mnasoma biblia toka kuzaliwa hadi kufa. huku ukiwananga ndugu zako kuwa wanaishia kusoma misale ya waumini as if yaliomo kwenye misale ni maono ya mama white au bwana miller na sio neno la Mungu. MNA CENTER, COLLEGE AU CHUO GANI CHA KUJIVUNIA KINACHOJIHUSISHA NA BIBLIA ?? tuambie walau kimoja tu ili tukuamini na sio kila kukicha mnamsingizia na kumtwisha mzigo roho mtakatifu.

na muda sio mrefu hapa kwetu tanzania huko dodoma kama Mungu atapenda kanisa litatufunguli kituo cha kufundisha na kujifunza biblia yaani CATHOLIC BIBLICAL CENTER (CBC) lipo kwenye huo mchakato kwani sasa lina wataalamu wa kitanzania Mungu bariki. huko hata wewe msabato ambaye kila kukicha ni kulinanga kanisa katoliki unakaribishwa kujifunza biblia kwani mambo utakayo fundishwa huko ni pamoja na historia, lugha asili za biblia yaani kigiki na kiebrania na mengine mengi. karibu uondokane na ujinga wa kuvamia mambo yanayohitaji taaluma kama zilivo taaluma zingine kama udaktari, ualimu nk

sikuwa na nia ya kucoment chochote kuhusu uzi na biblia ila nimeona umeandika KIDHARAU SANA akati hata umri wa miaka 150 ya ukristo tanzania ninyi wasabato hata kiulimwengu hamjafikisha. hata robo ya robo ya umri wa kanisa HAMNA.

SIKU NYINGINE UWE UNAHAKIKI UNACHOANDIKA KABLA YA KUKIPOST.
 
Wewe jamaa unatia aibu na unatia huruma sana...unajivunia kuwa na vyuo vinavyofundisha mafundisho ya wanadamu badala ya kufundisha neno la Mungu. Yesu alisema "...nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu.

Ndugu yangu, hivyo vyuo ningeviona vya maana kama vingekufanya ujue kuwa:

1.Amri kumi za Mungu kama zilivyo katika Biblia zimechakachuliwa; ya pili inayokataza kuabudu sanamu imetolewa (kwa sababu ambazo unazijua). Ya nne inayohusu sabato imebadilishwa, ya kumi inayosema usitamani imegawanywa mara mbili ili kufanya idadi iendelee kuwa kumi.

2. Papa hana mamlaka ya kusamehe dhambi, mwenye mamlaka ya kusamehe dhambi ni Mungu pekee.

3. Hatuhitaji kuomba msamaha wa dhambi kupitia Bikira maria. Yesu alisema ombeni lolote kwa jina langu nitalifanya.

4. Ubatizo wa watoto wadogo si ubatizo wa kibiblia. Yesu alisema...nendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu aaminiye na kubatizwa ataokoka. Nyie mnawabatiza watoto wadogo kinyume na biblia.

5. Fundisho la Indulgency (sin for sale) si fundisho la kibiblia...

6. Fundisho la kwamba roho hazifi ni kwamba mtu akifa roho yake inaenda Pulgatory (sehemu maalumu ya kutakasa roho kabla haijaenda jehanamu) si la kibiblia.

7. Fundisho la kwamba Kanisa la Roman Catholic lina mamlaka ya kubadili maandiko si la kibiblia.

8. Fundisho la kusali rosali si la kibiblia.

9. Fundisho la kwamba kanisa la Roman Catholic halikosei si la kibiblia.

10. Fundisho la kusali siku ya kwanza ya juma yaani jumapili si la kibiblia.

Kuna mambo mengi sana ambayo kanisa linayafundisha na kuyafuata ambayo ni mapokeo ya kipagani ambayo hayako kwenye Biblia...kwa leo hayo yanatosha.
 
1:Miller hakukosea Muda ila alikosea tukio. Na hata yeye alikuwa hana imani kuubwa kuhusu timing/Time setting ndio maana usiku ule wa tarehe 22 alitoa kauli kuonyesha mashaka kuhusu kuja kwa Yesu maana alikumbukia kauli ya Yesu '' Hamjui siku wala saa''.

2: Hiyo formula sio ya Kisabato, maana hata miller hakuwa msabato, na wafuasi wake hawakuwa wasabato (SDA).
Pili Miller hakuasisi hiyo formula, Bali ni formula ya kibibilia. Imetumika siku nyingi kabla hata ya mwaka 1000 kung'amua kuwa mpinga kristo anayezungumzwa kwenye daniel na Ufunuo ni Upapa au atatokana na Roman empire. Aliitumia Daniel kuwakumbusha waisrael wasrael kuwa muda wao wa miaka 70 umepita warudi kwa israel kutoka babeli, waliitumia majusi waarabu kujua Yesu anazaliwa wakati huo maana Ilishatabiriwa. Aliitumia Jerome kusema mpingakristo ataibuka baada ya kuanguka kwa Dola la kirumi. Wanaitumia Wasabato SDA kutafsiri unabii wa siku za Mwisho. Haionyeshi siku ya Kuja kwa Yesu maana Yesu alishasema hakuna hajuae ila alitoa dalili za kuja kwake.

3:Hilo Swali wakiulizwa wao watatoa jibu zuri. Ila kwa Mujibu wa hata vikao vyao, mfano 1840 pale boston walikuwepo watu waliosimamia kauli ya Yesu kuwa hajui siku wala saa. Hata ile conference ya 1942 qualification ya kuingia ilikuwa uamini Yesu anakuja tena haraka ila sio lini, kwa sababu baadhi yao walikuwa na mashaka na time setting. Pia kama nilivyoonyesha hapo juu hata siku moja kabla ya disapointment hata miller mwenyewe alikuwa na mashaka kuhusu time setting ila alikuwa na uhakika kuwa Yesu anakuja upesi mno kwa mujibu wa ukokotozi wa kimakosa wa unabii.

4:Hawakuasisi formula, walitumia formula iliyokuwepo miaka yote, Hata critics wao baadhi waliwashangaa kwa kutumia formula hiyohiyo.
Kwa nini waamini Yesu angekuja, hapo ninasema walikosea. Na sio wakristo wa kwanza kukosea. Walianza Mitume kukosea kuwa Yesu amekuja kuwapa utawala wa kidunia hadi mama zao yohana akawaombea vyeo kwenye utawala wao. Lkn hatujakataa Ukristo kwa sababu waliwahi kukosea bali kwa sababu walielewa walikosea wapi na kuendeleza ukweli wa bibilia. Ndio Maana SDA tangu imekuwepo 1863 haijawahi kumfundisha mtu yoyote kuwa Yesu anakuja siku flani exactly. Ila wanafundisha kwa peni na mdomo Yesu anakuja Upesi sana. Tena tofauti na uongo wa kuwa anakuja katika roho sijui si katika mwili. Wanafundisha anakuja katika mwili na kila jicho litamuona. anakuja kwa kuonekana kama alivyoondoka kwa kuonekana.

5:Hili alina msingi, maana hellen alikuwa mbaptist hakuwa msabato enzi akiwa mfuasi wa miller. Mungu alianza kumtumia baada ya great dissapointment. Hakuna msabato wala E.G White anayesema Yesu amemwambia anakuja lini kwa maana ya tarehe. Badala yake Wasabato SDA na Hellen White mwenyewe wanapiga marufuku Kuweka Muda wa Kuja kwa Yesu tangu wamekuwepo.

6: Day Year principle ya kutafsiri unabii nimeshasema sio ya miller wala helen bali ni ya kwenye bibilia. Unabii wa Daniel hautabili kuja kwa Yesu bali Matukio ya kabla ya Kuja kwake. Hivyo Miller alikosea kuweka timing, EGW kama miongoni mwa wafuasi tena akiwa sio msabato alikuwa anapitishwa katika uzoefu na baada ya kufunuliwa na kupata maarifa na anapiga marufuku time seting katika maandishi yake. Yeye sio wa kwanza hata Petro alikuwepo wakati Yesu anasema enendeni ulimwenguni kote mkaihubiri injili lkn ni petro huyohuyo aliyedhani Yesu alimaanisha wayahudi tu hadi kuwatenga wakina kornelio. na sio yeye tu kanisa zima hadi Mungu alipowafunulia. Mjinga ataweka kambi kwenye makosa ya Uelewa, ila mwerevu atashikamana na ufahamu mpya wa kweli wa kimaandiko.

7:Swali hili limejengwa katika upotofu. Na nadhani limewalenga wasio na maarifa na taarifa za kutosha kuhusu anasachosema EGW. maandiko yake yake yako wazi akipinga time setting. Kuhusu Yesu kushuka kufika chumba flani, Sentensi hiyo imekuwa calculated kupotosha kuwa Yesu Yuko njiani kwenye kachumba flani. Fundisho la SDA kuhusu Patakatifu ambapo image yake imeelezwa vzr katika Vitabu vya walawi, na waebrania liko wazi Mambo Yote ya Utakaso Yanayofanyika Mbinguni Yako Mbinguni ha hayana Uhusiano na Yesu Kushuka kuikaribia dunia, Bali yanauhusiano na Kumaliza kazi yake ambayo Hata Yeye anasema hajui itamalizika lini ila katuachia dalili sio siku. Na huu ndio msimamo wa EGW hadi anakufa, na Ndio Msimamo wa SDA na ndio msimamo wa Bibilia na Mitume Kuwa Yesu anakuja upesi ila Japo hatujui saa ila dalili ziko wazi.

Mkuu Zitto Jr sina wasiwasi na uwezo wa kupotosha wa mkuu Sanctus maana sio mara ya kwanza kukutana naye humu kwenye mijadala na bahati mbaya huwa haagi. Uwezo huo ni mkubwa kiasi kama hufuatilii matukio na kusoma katikati ya mistari unaweza kujikuta ukirushwa huku na kule na kila kama mtoto mdogo.

Fact Kuu ya Upotoshaji wa huyu bingwa ni, Miller alivumbua Formula ya kutafsiri kuja kwa Yesu au unabii wa Daniel wakati formula hiyo miaka Yote kabla hazijavumbuliwa na majesuits formula zingine mbili katika kipindi cha counter-reformation.
Preterism school of interpretation and Futurism school of interpretation zilizobuniwa na majesuit wakina fransisco ribera Robert Bellamine, Luis De Alcaser. Hii ilikuwa katika harakati za kudivert tuhuma za reformers kuwa pope is antichrist, na hata walokole wengi wameingia kwenye huu mtego.
Kama Msingi ni HISABATI alizotumia Miller basi Hakuzitunga yeye, Kama msingi ni Kuja kwa Yesu Miller alikosea, na White kabla ya kujua ukweli alikosea. Hata mimi ningekuwa hai nisingekubaliana nao, Ila nakubaliana na Msimamo wa white na SDA kuhusu kuja kwa Yesu maana 100% ni biblical supported.

Mbarikiwe Wakuu mbalimbali.
cc
SANCTUS ANACLETUS
Otorong'ong'o

karibuni kwa hoja mbalimbali wakuu.
Umeshamaliza kila kitu mkuu...labda ubishi tu. Nimependa hii sentensi "mjinga ataweka kambi kwenye makosa ya uelewa "
 
unajivunia kuwa na vyuo vinavyofundisha mafundisho ya wanadamu badala ya kufundisha neno la Mungu.
ndio tunajivunia na tunavyo vingi kwelikweli vya mafundisho unayoyaita ya waanadamu vipo vingi tu na vya neno la Mungu vipo vingi tu. na hatuko wachoyo yeyote anasoma hata anaetutukana ruksa anasoma.

Kuna mambo mengi sana ambayo kanisa linayafundisha na kuyafuata ambayo ni mapokeo ya kipagani ambayo hayako kwenye Biblia
pia kuna mengi sana zaidi ya yaliomo kwenye biblia ambayo yesu na mitume wake waliyafanya na kufindisha ila hayajaandikwa. usijisahaulishe kuhusu hilo
 
unajivunia kuwa na vyuo vinavyofundisha mafundisho ya wanadamu badala ya kufundisha neno la Mungu.
ndio tunajivunia na tunavyo vingi kwelikweli vya mafundisho unayoyaita ya waanadamu vipo vingi tu na vya neno la Mungu vipo vingi tu. na hatuko wachoyo yeyote anasoma hata anaetutukana kuwa sisi ni "mama wa makahaba" ruksa anasoma tu ilimradi havunji sheria hata hapa kwetu tz kuna segerea, kuna kipalapala unasoma tu
Kuna mambo mengi sana ambayo kanisa linayafundisha na kuyafuata ambayo ni mapokeo ya kipagani ambayo hayako kwenye Biblia
pia kuna mengi sana zaidi ya yaliomo kwenye biblia ambayo yesu na mitume wake waliyafanya na kufundisha ila hayajaandikwa kwenye biblia usijisahaulishe kuhusu hilo
 
ndio tunajivunia na tunavyo vingi kwelikweli vya mafundisho unayoyaita ya waanadamu vipo vingi tu na vya neno la Mungu vipo vingi tu. na hatuko wachoyo yeyote anasoma hata anaetutukana kuwa sisi ni "mama wa makahaba" ruksa anasoma tu ilimradi havunji sheria hata hapa kwetu tz kuna segerea, kuna kipalapala unasoma tu

pia kuna mengi sana zaidi ya yaliomo kwenye biblia ambayo yesu na mitume wake waliyafanya na kufundisha ila hayajaandikwa kwenye biblia usijisahaulishe kuhusu hilo
Hayo ambayo hayako kwenye Biblia mimi siyajui...jambo lolote ambalo haliko kwenye biblia si mhimu kwa wokovu wetu!
 
Hii hatorudi imekufumbua wewe ni nani
Hilo ndo tatizo la kuhamishia ufahamu wote kwenye hicho kitabu, kiufupi mijadala ya aina yako huwa haifikii kuafaka. Ila ni haki yako kuamini hivyo na ni haki ya wengine kuamini vingine, cha msingi ni kila upande kuheshimu upande mwingine. Kwani masuala ya imani ili yawe ni tija ni vizuri yakwa very personal business.
 
kanisa katoliki lina mahali maalumu (vyuo vidogo na vya kimataifa) pa kufundishia, kusomesha na kujifunza kila kilicho muhimu katika theology na biblia kuanzia lugha zote za biblia, uandishi, jumbe, hija na research katika nchi na mahali pote ambapo vitabu vya biblia viliandikwa na kutumika. na mifano ya vyuo hivyo ni

Pontifical University urbanian -ROME
Innsbruck University - AUSTRIA
St joseph's College -washington DC
Pontifical biblical Institute - ROME
Lateran University - ROME
NK

sasa ninyi ambao mnadai kuwa mnasoma biblia toka kuzaliwa hadi kufa. huku ukiwananga ndugu zako kuwa wanaishia kusoma misale ya waumini as if yaliomo kwenye misale ni maono ya mama white au bwana miller na sio neno la Mungu. MNA CENTER, COLLEGE AU CHUO GANI CHA KUJIVUNIA KINACHOJIHUSISHA NA BIBLIA ?? tuambie walau kimoja tu ili tukuamini na sio kila kukicha mnamsingizia na kumtwisha mzigo roho mtakatifu.

na muda sio mrefu hapa kwetu tanzania huko dodoma kama Mungu atapenda kanisa litatufunguli kituo cha kufundisha na kujifunza biblia yaani CATHOLIC BIBLICAL CENTER (CBC) lipo kwenye huo mchakato kwani sasa lina wataalamu wa kitanzania Mungu bariki. huko hata wewe msabato ambaye kila kukicha ni kulinanga kanisa katoliki unakaribishwa kujifunza biblia kwani mambo utakayo fundishwa huko ni pamoja na historia, lugha asili za biblia yaani kigiki na kiebrania na mengine mengi. karibu uondokane na ujinga wa kuvamia mambo yanayohitaji taaluma kama zilivo taaluma zingine kama udaktari, ualimu nk

sikuwa na nia ya kucoment chochote kuhusu uzi na biblia ila nimeona umeandika KIDHARAU SANA akati hata umri wa miaka 150 ya ukristo tanzania ninyi wasabato hata kiulimwengu hamjafikisha. hata robo ya robo ya umri wa kanisa HAMNA.

SIKU NYINGINE UWE UNAHAKIKI UNACHOANDIKA KABLA YA KUKIPOST.
Wewe nae unafanya kosa kwa kufikiri kwamba elimu ya mbingu inapimwa kwa degree . Hata ukijenga chuo angani kama Roho hayupo ni bure. Sisi pia tunavyo hivyo vyuo kwa mfano hapa Tanzania tuna ARUSHA UNIVERSITY.

Kipimo ni Biblia ,Yesu alifundisha Biblia , mitume walifundisha Biblia .

Ungekuwa unasoma Biblia ungejua visa vya Mafarisayo na Waalimu (walikuwa na elimu ya juu sana ya dini lakini hawakuyaelewa mafundisho ya Yesu au hawakutaka kubadilika kwa kiburi) au ungejua habari za SAULI /PAULO ambaye kwa elimu ya dini angekuwa na PhD lakini kabla ya kupewa roho hakuwaelewa mitume aliwatesa na kuwaua

DEGREE HAZIHITAJI HAPA
 
ndio tunajivunia na tunavyo vingi kwelikweli vya mafundisho unayoyaita ya waanadamu vipo vingi tu na vya neno la Mungu vipo vingi tu. na hatuko wachoyo yeyote anasoma hata anaetutukana kuwa sisi ni "mama wa makahaba" ruksa anasoma tu ilimradi havunji sheria hata hapa kwetu tz kuna segerea, kuna kipalapala unasoma tu

pia kuna mengi sana zaidi ya yaliomo kwenye biblia ambayo yesu na mitume wake waliyafanya na kufundisha ila hayajaandikwa kwenye biblia usijisahaulishe kuhusu hilo
Husomi maandiko ...ungejua kuwa Biblia (neno la Mungu) iliandikwa na wanadamu walioongozwa na Roho wa Mungu.

Hayo yaliyoandikwa ndiyo Mungu alikusudia tujifunze

Hayo ambayo hayakuandikwa ni kitabu gani na unayajuaje?
 
Back
Top Bottom