William Miller: Kama Yesu hakujua Hisabati au kutafsiri mambo bora angalikaa Kimya. Mbona siku ya mwisho wa dunia inakokotoleka kirahisi?

Anaishi kukarili siyo anachojua
Mzee wa vijarida,
Nadhani alipokuwa mtoto gheto lake lilijaa magazeti ukutani asee,maana ndo ubongo wake

Ni shida sana. Ila kuna siku zinakuja watalaumu hii mitandao maana wengi wanafunguliwa
 
Kama William ana akili basi ajikokotolee siku za Kuishi na kuondoka hapa Duniani.
 
1:Miller hakukosea Muda ila alikosea tukio. Na hata yeye alikuwa hana imani kuubwa kuhusu timing/Time setting ndio maana usiku ule wa tarehe 22 alitoa kauli kuonyesha mashaka kuhusu kuja kwa Yesu maana alikumbukia kauli ya Yesu '' Hamjui siku wala saa''.

2: Hiyo formula sio ya Kisabato, maana hata miller hakuwa msabato, na wafuasi wake hawakuwa wasabato (SDA).
Pili Miller hakuasisi hiyo formula, Bali ni formula ya kibibilia. Imetumika siku nyingi kabla hata ya mwaka 1000 kung'amua kuwa mpinga kristo anayezungumzwa kwenye daniel na Ufunuo ni Upapa au atatokana na Roman empire. Aliitumia Daniel kuwakumbusha waisrael wasrael kuwa muda wao wa miaka 70 umepita warudi kwa israel kutoka babeli, waliitumia majusi waarabu kujua Yesu anazaliwa wakati huo maana Ilishatabiriwa. Aliitumia Jerome kusema mpingakristo ataibuka baada ya kuanguka kwa Dola la kirumi. Wanaitumia Wasabato SDA kutafsiri unabii wa siku za Mwisho. Haionyeshi siku ya Kuja kwa Yesu maana Yesu alishasema hakuna hajuae ila alitoa dalili za kuja kwake.

3:Hilo Swali wakiulizwa wao watatoa jibu zuri. Ila kwa Mujibu wa hata vikao vyao, mfano 1840 pale boston walikuwepo watu waliosimamia kauli ya Yesu kuwa hajui siku wala saa. Hata ile conference ya 1942 qualification ya kuingia ilikuwa uamini Yesu anakuja tena haraka ila sio lini, kwa sababu baadhi yao walikuwa na mashaka na time setting. Pia kama nilivyoonyesha hapo juu hata siku moja kabla ya disapointment hata miller mwenyewe alikuwa na mashaka kuhusu time setting ila alikuwa na uhakika kuwa Yesu anakuja upesi mno kwa mujibu wa ukokotozi wa kimakosa wa unabii.

4:Hawakuasisi formula, walitumia formula iliyokuwepo miaka yote, Hata critics wao baadhi waliwashangaa kwa kutumia formula hiyohiyo.
Kwa nini waamini Yesu angekuja, hapo ninasema walikosea. Na sio wakristo wa kwanza kukosea. Walianza Mitume kukosea kuwa Yesu amekuja kuwapa utawala wa kidunia hadi mama zao yohana akawaombea vyeo kwenye utawala wao. Lkn hatujakataa Ukristo kwa sababu waliwahi kukosea bali kwa sababu walielewa walikosea wapi na kuendeleza ukweli wa bibilia. Ndio Maana SDA tangu imekuwepo 1863 haijawahi kumfundisha mtu yoyote kuwa Yesu anakuja siku flani exactly. Ila wanafundisha kwa peni na mdomo Yesu anakuja Upesi sana. Tena tofauti na uongo wa kuwa anakuja katika roho sijui si katika mwili. Wanafundisha anakuja katika mwili na kila jicho litamuona. anakuja kwa kuonekana kama alivyoondoka kwa kuonekana.

5:Hili alina msingi, maana hellen alikuwa mbaptist hakuwa msabato enzi akiwa mfuasi wa miller. Mungu alianza kumtumia baada ya great dissapointment. Hakuna msabato wala E.G White anayesema Yesu amemwambia anakuja lini kwa maana ya tarehe. Badala yake Wasabato SDA na Hellen White mwenyewe wanapiga marufuku Kuweka Muda wa Kuja kwa Yesu tangu wamekuwepo.

6: Day Year principle ya kutafsiri unabii nimeshasema sio ya miller wala helen bali ni ya kwenye bibilia. Unabii wa Daniel hautabili kuja kwa Yesu bali Matukio ya kabla ya Kuja kwake. Hivyo Miller alikosea kuweka timing, EGW kama miongoni mwa wafuasi tena akiwa sio msabato alikuwa anapitishwa katika uzoefu na baada ya kufunuliwa na kupata maarifa na anapiga marufuku time seting katika maandishi yake. Yeye sio wa kwanza hata Petro alikuwepo wakati Yesu anasema enendeni ulimwenguni kote mkaihubiri injili lkn ni petro huyohuyo aliyedhani Yesu alimaanisha wayahudi tu hadi kuwatenga wakina kornelio. na sio yeye tu kanisa zima hadi Mungu alipowafunulia. Mjinga ataweka kambi kwenye makosa ya Uelewa, ila mwerevu atashikamana na ufahamu mpya wa kweli wa kimaandiko.

7:Swali hili limejengwa katika upotofu. Na nadhani limewalenga wasio na maarifa na taarifa za kutosha kuhusu anasachosema EGW. maandiko yake yake yako wazi akipinga time setting. Kuhusu Yesu kushuka kufika chumba flani, Sentensi hiyo imekuwa calculated kupotosha kuwa Yesu Yuko njiani kwenye kachumba flani. Fundisho la SDA kuhusu Patakatifu ambapo image yake imeelezwa vzr katika Vitabu vya walawi, na waebrania liko wazi Mambo Yote ya Utakaso Yanayofanyika Mbinguni Yako Mbinguni ha hayana Uhusiano na Yesu Kushuka kuikaribia dunia, Bali yanauhusiano na Kumaliza kazi yake ambayo Hata Yeye anasema hajui itamalizika lini ila katuachia dalili sio siku. Na huu ndio msimamo wa EGW hadi anakufa, na Ndio Msimamo wa SDA na ndio msimamo wa Bibilia na Mitume Kuwa Yesu anakuja upesi ila Japo hatujui saa ila dalili ziko wazi.


Mkuu Zitto Jr sina wasiwasi na uwezo wa kupotosha wa mkuu Sanctus maana sio mara ya kwanza kukutana naye humu kwenye mijadala na bahati mbaya huwa haagi. Uwezo huo ni mkubwa kiasi kama hufuatilii matukio na kusoma katikati ya mistari unaweza kujikuta ukirushwa huku na kule na kila kama mtoto mdogo.

Fact Kuu ya Upotoshaji wa huyu bingwa ni, Miller alivumbua Formula ya kutafsiri kuja kwa Yesu au unabii wa Daniel wakati formula hiyo miaka Yote kabla hazijavumbuliwa na majesuits formula zingine mbili katika kipindi cha counter-reformation.
Preterism school of interpretation and Futurism school of interpretation zilizobuniwa na majesuit wakina fransisco ribera Robert Bellamine, Luis De Alcaser. Hii ilikuwa katika harakati za kudivert tuhuma za reformers kuwa pope is antichrist, na hata walokole wengi wameingia kwenye huu mtego.
Kama Msingi ni HISABATI alizotumia Miller basi Hakuzitunga yeye, Kama msingi ni Kuja kwa Yesu Miller alikosea, na White kabla ya kujua ukweli alikosea. Hata mimi ningekuwa hai nisingekubaliana nao, Ila nakubaliana na Msimamo wa white na SDA kuhusu kuja kwa Yesu maana 100% ni biblical supported.

Mbarikiwe Wakuu mbalimbali.
cc
SANCTUS ANACLETUS
Otorong'ong'o


karibuni kwa hoja mbalimbali wakuu.
 
Mtoa hoja ni ama anahitaji kushinda au Shetani amekifunga kichwa chake na minyororo mizito hata asisikilize maandiko ya Biblia yaliyotolewa humu kama majibu ya hoja yake.

Kama mkristo anakosoa Biblia (mfono: habari za hekalu la mbinguni ama Yesu kuwa kuhani mkuu) tutumie ushahidi upi sasa ?

Kujifunza Biblia ni utamaduni wa mwadventista msabato tangu unapozaliwa hadi kufa . Mkatoliki yeye ni "Mithale ya waumini" (yaani mafunzo ambayo kanisa limekusudia tu yaende kwa waumini).


Kama unahoji maandiko safari yako ni nyingine maana hata Yesu mwenyewe aliyaishi hayo maandiko
 
Uelewa wako ni mdogo sana katika maandiko. Haya mambo yanahitaji usaidizi wa Roho mtakatifu na wali siyo ujuaji wa kuungaunga.

Kwa mtazamo huo wa codes za mawasiliano za kina Yohana, je katika unabii wa Daniel yeye alikuwa anamuogopa nani na alikuwa anawasiliana na nani?


Kwa mtazamo wako ni kwamba habari za kitabu cha Ufunuo hazituhusu?
 
Hawa wakina SANCTUS kama wangekuwa wanasoma Biblia kwa unyenyekevu na kwa lengo la kujifunza haya mambo wangeyajua. Kwa mfano mambo mawili yanamhusu PAPA (ambaye ni mnyama aliyeandikwa katika kitabu cha Ufunuo
)
1. Alama ya mnyama=666

2. Kufuru = "badala mwana wa Mungu duniani"

Haya mambo hayawezi kuwa yametokea bahati mbaya


Huyu SANCTUS akane hapa kwa maandiko na kwa ushahidi wa kihistoria kwamba yale maandishi ya kofia ya papa hayafanyi jumla hesabu 666 au hayamaanishi "badala ya mwana wa mungu duniani"

Tena asije hapa akaanza kusema nimebadili maada. Kama anaijua hesabu ya Miller naamini anaelewa kuwa inahusisha ukatiri wa utawala wa kipapa kwa mamilioni ya wakristo. Na kama kweli ameisoma vizuri hesabu hii atakuwa anaelewa vizuri njinsi ambavyo unabii wa Daniel unavyoendana na unabii wa kitabu cha ufunuo.
 
Hawa wakina SANCTUS kama wangekuwa wanasoma Biblia kwa unyenyekevu na kwa lengo la kujifunza haya mambo wangeyajua. Kwa mfano mambo mawili yanamhusu PAPA
Uelewa wako ni mdogo sana katika maandiko. Haya mambo yanahitaji usaidizi wa Roho mtakatifu na wali siyo ujuaji wa kuungaunga.

Kujifunza Biblia ni utamaduni wa mwadventista msabato tangu unapozaliwa hadi kufa . Mkatoliki yeye ni "Mithale ya waumini" (yaani mafunzo ambayo kanisa limekusudia tu yaende kwa waumini).
kanisa katoliki lina mahali maalumu (vyuo vidogo na vya kimataifa) pa kufundishia, kusomesha na kujifunza kila kilicho muhimu katika theology na biblia kuanzia lugha zote za biblia, uandishi, jumbe, hija na research katika nchi na mahali pote ambapo vitabu vya biblia viliandikwa na kutumika. na mifano ya vyuo hivyo ni

Pontifical University urbanian -ROME
Innsbruck University - AUSTRIA
St joseph's College -washington DC
Pontifical biblical Institute - ROME
Lateran University - ROME
NK

sasa ninyi ambao mnadai kuwa mnasoma biblia toka kuzaliwa hadi kufa. huku ukiwananga ndugu zako kuwa wanaishia kusoma misale ya waumini as if yaliomo kwenye misale ni maono ya mama white au bwana miller na sio neno la Mungu. MNA CENTER, COLLEGE AU CHUO GANI CHA KUJIVUNIA KINACHOJIHUSISHA NA BIBLIA ?? tuambie walau kimoja tu ili tukuamini na sio kila kukicha mnamsingizia na kumtwisha mzigo roho mtakatifu.

na muda sio mrefu hapa kwetu tanzania huko dodoma kama Mungu atapenda kanisa litatufunguli kituo cha kufundisha na kujifunza biblia yaani CATHOLIC BIBLICAL CENTER (CBC) lipo kwenye huo mchakato kwani sasa lina wataalamu wa kitanzania Mungu bariki. huko hata wewe msabato ambaye kila kukicha ni kulinanga kanisa katoliki unakaribishwa kujifunza biblia kwani mambo utakayo fundishwa huko ni pamoja na historia, lugha asili za biblia yaani kigiki na kiebrania na mengine mengi. karibu uondokane na ujinga wa kuvamia mambo yanayohitaji taaluma kama zilivo taaluma zingine kama udaktari, ualimu nk

sikuwa na nia ya kucoment chochote kuhusu uzi na biblia ila nimeona umeandika KIDHARAU SANA akati hata umri wa miaka 150 ya ukristo tanzania ninyi wasabato hata kiulimwengu hamjafikisha. hata robo ya robo ya umri wa kanisa HAMNA.

SIKU NYINGINE UWE UNAHAKIKI UNACHOANDIKA KABLA YA KUKIPOST.
 
Wewe jamaa unatia aibu na unatia huruma sana...unajivunia kuwa na vyuo vinavyofundisha mafundisho ya wanadamu badala ya kufundisha neno la Mungu. Yesu alisema "...nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu.

Ndugu yangu, hivyo vyuo ningeviona vya maana kama vingekufanya ujue kuwa:

1.Amri kumi za Mungu kama zilivyo katika Biblia zimechakachuliwa; ya pili inayokataza kuabudu sanamu imetolewa (kwa sababu ambazo unazijua). Ya nne inayohusu sabato imebadilishwa, ya kumi inayosema usitamani imegawanywa mara mbili ili kufanya idadi iendelee kuwa kumi.

2. Papa hana mamlaka ya kusamehe dhambi, mwenye mamlaka ya kusamehe dhambi ni Mungu pekee.

3. Hatuhitaji kuomba msamaha wa dhambi kupitia Bikira maria. Yesu alisema ombeni lolote kwa jina langu nitalifanya.

4. Ubatizo wa watoto wadogo si ubatizo wa kibiblia. Yesu alisema...nendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu aaminiye na kubatizwa ataokoka. Nyie mnawabatiza watoto wadogo kinyume na biblia.

5. Fundisho la Indulgency (sin for sale) si fundisho la kibiblia...

6. Fundisho la kwamba roho hazifi ni kwamba mtu akifa roho yake inaenda Pulgatory (sehemu maalumu ya kutakasa roho kabla haijaenda jehanamu) si la kibiblia.

7. Fundisho la kwamba Kanisa la Roman Catholic lina mamlaka ya kubadili maandiko si la kibiblia.

8. Fundisho la kusali rosali si la kibiblia.

9. Fundisho la kwamba kanisa la Roman Catholic halikosei si la kibiblia.

10. Fundisho la kusali siku ya kwanza ya juma yaani jumapili si la kibiblia.

Kuna mambo mengi sana ambayo kanisa linayafundisha na kuyafuata ambayo ni mapokeo ya kipagani ambayo hayako kwenye Biblia...kwa leo hayo yanatosha.
 
Umeshamaliza kila kitu mkuu...labda ubishi tu. Nimependa hii sentensi "mjinga ataweka kambi kwenye makosa ya uelewa "
 
unajivunia kuwa na vyuo vinavyofundisha mafundisho ya wanadamu badala ya kufundisha neno la Mungu.
ndio tunajivunia na tunavyo vingi kwelikweli vya mafundisho unayoyaita ya waanadamu vipo vingi tu na vya neno la Mungu vipo vingi tu. na hatuko wachoyo yeyote anasoma hata anaetutukana ruksa anasoma.

Kuna mambo mengi sana ambayo kanisa linayafundisha na kuyafuata ambayo ni mapokeo ya kipagani ambayo hayako kwenye Biblia
pia kuna mengi sana zaidi ya yaliomo kwenye biblia ambayo yesu na mitume wake waliyafanya na kufindisha ila hayajaandikwa. usijisahaulishe kuhusu hilo
 
unajivunia kuwa na vyuo vinavyofundisha mafundisho ya wanadamu badala ya kufundisha neno la Mungu.
ndio tunajivunia na tunavyo vingi kwelikweli vya mafundisho unayoyaita ya waanadamu vipo vingi tu na vya neno la Mungu vipo vingi tu. na hatuko wachoyo yeyote anasoma hata anaetutukana kuwa sisi ni "mama wa makahaba" ruksa anasoma tu ilimradi havunji sheria hata hapa kwetu tz kuna segerea, kuna kipalapala unasoma tu
Kuna mambo mengi sana ambayo kanisa linayafundisha na kuyafuata ambayo ni mapokeo ya kipagani ambayo hayako kwenye Biblia
pia kuna mengi sana zaidi ya yaliomo kwenye biblia ambayo yesu na mitume wake waliyafanya na kufundisha ila hayajaandikwa kwenye biblia usijisahaulishe kuhusu hilo
 
Hayo ambayo hayako kwenye Biblia mimi siyajui...jambo lolote ambalo haliko kwenye biblia si mhimu kwa wokovu wetu!
 
Hii hatorudi imekufumbua wewe ni nani
Hilo ndo tatizo la kuhamishia ufahamu wote kwenye hicho kitabu, kiufupi mijadala ya aina yako huwa haifikii kuafaka. Ila ni haki yako kuamini hivyo na ni haki ya wengine kuamini vingine, cha msingi ni kila upande kuheshimu upande mwingine. Kwani masuala ya imani ili yawe ni tija ni vizuri yakwa very personal business.
 
Wewe nae unafanya kosa kwa kufikiri kwamba elimu ya mbingu inapimwa kwa degree . Hata ukijenga chuo angani kama Roho hayupo ni bure. Sisi pia tunavyo hivyo vyuo kwa mfano hapa Tanzania tuna ARUSHA UNIVERSITY.

Kipimo ni Biblia ,Yesu alifundisha Biblia , mitume walifundisha Biblia .

Ungekuwa unasoma Biblia ungejua visa vya Mafarisayo na Waalimu (walikuwa na elimu ya juu sana ya dini lakini hawakuyaelewa mafundisho ya Yesu au hawakutaka kubadilika kwa kiburi) au ungejua habari za SAULI /PAULO ambaye kwa elimu ya dini angekuwa na PhD lakini kabla ya kupewa roho hakuwaelewa mitume aliwatesa na kuwaua

DEGREE HAZIHITAJI HAPA
 
Husomi maandiko ...ungejua kuwa Biblia (neno la Mungu) iliandikwa na wanadamu walioongozwa na Roho wa Mungu.

Hayo yaliyoandikwa ndiyo Mungu alikusudia tujifunze

Hayo ambayo hayakuandikwa ni kitabu gani na unayajuaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…