William Miller: Kama Yesu hakujua Hisabati au kutafsiri mambo bora angalikaa Kimya. Mbona siku ya mwisho wa dunia inakokotoleka kirahisi?

Kwa sababu mwishoni mleta mada amewa attack wasabato. Kwamba yesu anachambua majina ya wasabato !! Kitu ambacho hakipo ktk vitabu vyote.

Haya mambo ya ushabiki, unaoleta attacking and defensing kwa imani zetu hizi, hazimsaidii mtu yeyote mkristo kuona ufalme wa Mungu. Hata majuzi nimesikia eti wengine wamefuta Holly Bible ktk taratibu za ibada na kuiingiza wanayoyaita ya kisasa!! Lakini yoote haya, hayaleti uhalali wa dhehebu fulani dhidi ya nyingine machoni pa bwana, bali matendo yako.

Uandishi unaoamsha ushabiki wa wakristo kushambuliana, kwa namna yoyote haufai. Katika imani zetu hizi kuna mambo mengi yalikosewa, lakini ni kulingana nyakati na tamaduni za wakati huo na taathira zake.
 
Hayo ambayo hayako kwenye Biblia mimi siyajui...jambo lolote ambalo haliko kwenye biblia si mhimu kwa wokovu wetu!
ni jambo jema sana umekiri mwenyewe kuwa hayo yasioandika ambayo ni mengi zaidi wewe HUYAJUI. na sidhani kama ni kosa lako ila ni la kihistoria tu na asili zetu. hivyo kwako hakuna kilichoharibika na kwangu pia hakuna kilicho haribika isipokuwa mimi na wakatoliki tuyajuayo yalio nje ya biblia tuna Mungu MREFU na ninyi msio yajua mna Mungu MFUPI.

USHAURI
siku nyingine usirudie tena kuwaita ndugu zako katika kristo kuwa wanamafundisho ya kipagani au ni wapagani ilihali wewe mwenyewe hujui YOTE na wala huna YOTE yaliofanywa na kufundishwa na Yesu na mitume wake. na kama biblia yako inakiri kuwa yalioandikwa ni machache sio yote na wakati huohuo yesu kabla ya kupaa mbinguni aliwaagiza wanafunzi wake wakafundishe YOTE na kusema YOTE aliowaamuru na waliyo jifunza kwake. na hata yatakayo sahaulika aliwaahidia ROHO MTAKATIFU ili kuyakumbuka na kuyabeba yote.

hivyo uhalali wa kuwaita wengine wapagani sijui unautoa wapi ?? na kwa chanzo kipi ??
 
Ibada za sanamu kawafundisha nani?
 
Kipimo ni Biblia ,Yesu alifundisha Biblia , mitume walifundisha Biblia .
kabla ya biblia kupatikana walitumia kipimo gani ?? na ambako biblia hazisomwi wanatumia kipimo gani ??

kuna madhehebu zaidi ya 2000 na yote yana biblia moja je ni roho gani huyo kigeugeu anayefundisha kweli zaidi 2000 toka kwenye chanzo kimoja ?? au hajui kusoma ??

kuna mahali unakosea sana jitafakari na uchukue hatu
Wewe nae unafanya kosa kwa kufikiri kwamba elimu ya mbingu inapimwa kwa degree . Hata ukijenga chuo angani kama Roho hayupo ni bure
umetumia kipimo gani au umetumia kigezo gani kujua kuwa watu wajishughulishao kutafuta ELIMU ya mbinguni na duniani kadili ya maagizo ya kitabu cha mithali na agizo la Yesu la kumpenda Mungu kwa AKILI zako zote. hao HAWANA ROHO. ila wewe na watu wenye mawazo na mitazamo kama yako MNA ROHO ?? tueleze umetumia kipimo gani mpendwa ??
Hayo yaliyoandikwa ndiyo Mungu alikusudia tujifunze
na aliyesemama kwamba enendeni ulimwenguni kote mkawafundishe YOTE na kuwaamuru kuyashika YOTE niliowafundisheni na mliojifunza kwangu. alikuwa mwongo sio ? a wewe unaifahamu biblia kuliko yeye ?
 
Hivi unaandika nini hasa ndugu?
 
Hayo ambayo hayako kwenye Biblia mimi siyajui...jambo lolote ambalo haliko kwenye biblia si mhimu kwa wokovu wetu!

Kama ambavyo hamkufahamu baadhi ya mambo au mliyafahamu isivyo ndivyo hivyo pia mtakuja kuelewa siku moja kwamba Biblia siyo document ambayo imebeba kila jambo ambalo limetokea katika historian ya wokovu Wa mwanadamu. Iko siku mtakuja kuelewa kuwa Biblia ni mapokeo. Ellen White hakuamini katika Utatu Mtakatifu lakini leo baadhi yenu mnaamini jambo hilo tayari.
 
Biblia siyo document iliyobeba kila kitu? Maajabu! Kwahiyo hayo mengine yako kwenye kitabu gani?
 
3. Papa hatawafumusha wasabato kusali jumamosi kama ulivyodai, badala yake atawalazimisha watu wote kusali siku ya kwanza ya juma (yaani Jumapili) badala ya siku ya saba ya juma (yaani Jumamosi).

Acha uongo mkuu, Jumapili ni siku ya Pili ya Juma
na Jumamosi ni siku ya kwanza(mosi) ya Juma

mtililiko ni huu👇

1. Jumamosi
2. Jumapili
3. jumatatu
4. Jumanne
5. jumatano
6. alhamisi
7. ijumaa

kwahiyo kimahesabu na kimantiki Ijumaa ndio siku ya saba ya juma
 
Kwa hoja hii mjadala naamini ulifungwa
 
Kwahiyo huo unabii wa kwanza ulikuwa feki na mkauamini mkaishia kuwa Disappointed?

Sasa unauthibitisho gani ufunuo huo mwingine sio the Next disappointed ?
 
Kutoa unabii ni jambo moja, kukosea kutafsiri unabii ni jambo jingine
 
Mkuu uko vizuri sana kwenye mambo ya tafsiri za kibiblia
Mimi nimezaliwa kwenye familia ya kiLutheri lakini nawaelewa na kuwaheshimu sana hasa Mapadri kwenye suala la tafsri na theolojia
 
Imani na mahesabu wapi na wapi? Huyo Miller hajiulizi kwanini Newton alichapisha mambo ya mahesabu na fizikia ambayo hadi leo tunayatumia lakini mambo mengine ya imani alielewa kwamba hiyo tasnia ina namna yake, akaiheshimu na kuacha iende kiimani.
Sasa tuambie hizo hesabu za kiunabii zikoje? Au unaona hazina manana!
 
Dah! Upelelezi gani tena wakuu? Ina maana Yesu hawezi kuona madhambi yetu hadi afanye upelelezi? Je ndo hali inayochangia hukumu kuchelewa kisa upelelezi haujakamilika? Kama Yesu alitufia msalabani kuna haja gani ya yeye kujifungia chumbani tena?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…