William Miller: Kama Yesu hakujua Hisabati au kutafsiri mambo bora angalikaa Kimya. Mbona siku ya mwisho wa dunia inakokotoleka kirahisi?

Ahaaa! Sisis saislaam na nabii issa wetu hatunaga haya mabo maana Qur-aan ishatueleza sikuhiyo ipo hata nabii issa(yesu)kaukataa mjadala huo sasa wasie waislaam ndo utasikia wakijihangaisha nahayo na kuhusisha wana sayansi na maandiko takatifu.
 
Ufunuo 11:19 Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi sana.

Hizi zilikuwa ndoto Mkuu na wala sio kwamba ndio uhalisia. Ukichukulia hivyo alivyoona Yohana ina maana Mbinguni kunanyeshaga mvua?
 
Kwahiyo unataka kusema mambo yote aliyoandika katika ufunuo siyo halisi ni ndoto?

Alichokuwa anakiona Yohana katika ndoto kuliashiria jambo jingine halisi. Kwa mfano anasema aliona Mwanamke amevikwa Jua,Nyota na Mwezi. Kwa hiyo huwezi kusema ni kweli kuna mtu anaweza kuvaa Jua au Nyota. Kumbe hayo maono kila moja lilikuwa na maana yake ambayo Kanisa la Mwanzo walikuwa wakielewa maana yake. Kimsingi lugha na staili aliyotumia ni lugha ya mafumbo iitwayo APOCALYPTIC. Ilikuwa ni lazima Yohana awasiliane na wanakanisa katika lugha hiyo ili kumkwepa Kaizari NERON ambaye ndiye leo wasbato mnasema ni PAPA ajaye.
 
Kwahiyo ndoto ya hekalu ilikuwa inahusu jambo gani halisi?
 
Aisee nafuatilia huu uzi kwa karibu sana ngoja niwaite wakuu hawa AROON mitale na midimu

AROON alishakuja akaishia kuporomosha matusi tu. Huyo kama hujamgundua ni mzuri sana kwa mijadala ambayo ana ready made answers. Nje ya hapo huwezi kumuona akitia mguu.Na hii ndio shida ya wenzetu. Majibu yao kwa masuala kadhaa yanafanana dunia nzima. Anaandaa mtu mmoja na kisha wengine wanafanya tu kazi ya duplication.
 
Yesu ni Mwana wa Mungu, Yesu ni Mungu!
YESU ni mtu, alikuwa muhubiri na mponyaji. Akapatwa na hatia ya uchochezi akahukumiwa kifo kwa kuwambwa msalabani. Akafa, akazikwa na mtamsubiri sana arudi na kamwe hatorudi.
 
Ndio shida yako, uongo na uzandiki,

Kuna matusi nimetukana? Nio quote hayo.matusi, au kwakuwa amri kumi kwenu ziliishia msalabani hivo ruksa kusema UONGO?

MADA YAKO NIMEONA NI YAKIPUUZI, MAANA USHAJIBIWA, SANA ILA UNAKAAGA KWA KIPIND THEN UNARUDI NA MASWALI YALE YALE

NA UTAMBUE HAKUNA ANAYEFANYA DUBLICATION, mada zangu, michango yangu 80% ni quotation za BIBLIA ,

Sinaga mbwembwe za Mapokeo kama.nyinyi waabudu masanamu
 
Kwahio Kama Yesu ni Malaika mkuu , na Yesu ni Mungu,Basi Mungu ni Malaika Mkuu! Hii inashangaza za Kuambiwa changanya na za kwako
 
Aisee nafuatilia huu uzi kwa karibu sana ngoja niwaite wakuu hawa AROON mitale na midimu
Asante mkuu. Unaweza kutoa maswali elekezi maana naona mada imekaa jumla jumla na kilawama zaidi.
Kama Day /Year principle aliyotumia miller imetumiwa hata kabla yake kuthibitisha utimilivu mwingi wa Unabii.
Kutakaswa pa patakatifu na kuja kwa Yesu alikosea. Kama wasabato hawaamini siku flani defined Yesu atakuja. Na hili likof wazi ktk Bibilia na machapisho yote ya wasabato pamoja na maandishi ya Ellen. G.White tunayeamini ni nabii wa Mungu pasipo shaka. Sabato namaanisha sda.

Cc Sanctus
 
Anaishi kukarili siyo anachojua
Mzee wa vijarida,
Nadhani alipokuwa mtoto gheto lake lilijaa magazeti ukutani asee,maana ndo ubongo wake
 
YESU ni mtu, alikuwa muhubiri na mponyaji. Akapatwa na hatia ya uchochezi akahukumiwa kifo kwa kuwambwa msalabani. Akafa, akazikwa na mtamsubiri sana arudi na kamwe hatorudi.
Hii hatorudi imekufumbua wewe ni nani
 
Siyo mada ya kipuuzi sema hauna vipisi vya magazeti vya kunukuu majibu,
Km nakuona vile unavyohangaika kutafuta pa kunukuu majibu
 
Okay naona mkuu SANCTUS ANACLETUS ameacha maswali ya kuongoza mjadala ambayo ungesaidia kuyajibu kwa faida ya wengi labda niyapaste upya

Kwa kuisoma Sadikifu (thesis) ya Miller na msimamo wa Yesu juu ya mwisho wa dunia,yafuatayo yanajitokeza:

1. Miller na wenzie walikosea wapi katika fomula yao kiasi kwamba Yesu hajawahi kuonekana toka mwaka 1843?

2. Je, wanahisabati wanaweza kuendeleza pale Miller na wenzie walipoishia katika kukokotoa mwisho wa dunia kwa kuihakiki hiyo fomula ya Kisabato juu ya kurudi kwa Yesu?

3. Je, Miller na wenzie hawakuwa wamefanikiwa kulisoma Agano Jipya ambamo msimamo wa Yesu juu ya tarehe ya mwisho wa dunia unawekwa wazi wazi kuwa tarehe husika haijulikani?

4. Je, ikiwa Miller na wafuasi wake akiwemo Mama wa “maono”,Ellen White, walikuwa wamelisoma Agano Jipya ni kwa nini wao waliamua kuasisi Fomula ya jambo ambalo Yesu alikwisha kusema hana uwezo nalo?

5. Je, kwa Yesu kusema haijui tarehe halafu Miller na Ellen White wakaja wakasema wanaifahamu tarehe ina maana Wasabato hao na wa leo mbingu ni yao kiasi kwamba wanaingia na kutoka hata wameweza kushirikishwa yanayoendelea huko Mbinguni?

6. Je, kwa Miller na Ellen kukubaliana kwamba wao walikuwa wameipata fomula ya kurudi kwa Yesu walimaanisha kwamba wao walikuwa ni wasomi sana na kwamba Yesu kusema haijui tarehe kulimaanisha Yesu alikisoma Kitabu cha Daniel na kutokikielewa au kwamba Yesu alikuwa anasoma mambo kwa kurukaruka?

7. Je, hadi sasa tumsikilize nani kati ya Yesu na wasabato juu ya mwisho wa dunia kwa sababu Ellen White ameshapewa maono yanayoonyesha kwamba Yesu ameshaanza kushuka na kwamba kwa sasa yuko katika chumba cha patakatifu pa patakatifu sana ambako anapitia majina ya wasabato na akitoka hapo moja kwa moja anatia timu hapa duniani?


Kwa yote hayo,sasa KARIBUNI kwa mjadala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…