- Source #1
- View Source #1
Video moja iliyowekwa kwenye mtandao wa Facebook inadai kuwa Naibu Rais wa Kenya William Ruto "ameichochea" jamii yake ya Wakalenjin dhidi ya Wakikuyu wakati wa mkutano wa kampeni kabla ya uchaguzi wa Agosti 9 2022.
Katika kipande hicho cha video kilichochapishwa tarehe 29 Julai, Ruto anazungumza kwa Kiswahili na Kiingereza, akimwambia rais aache kutaja jina lake.
Katika video hiyo Ruto anasema "Zungumza kuhusu mgombea wako,"Nilikuunga mkono ulipohitaji mtu wa kukusaidia. Ikiwa hutaki kuniunga mkono, niache peke yangu.”
Ruto alitofautiana na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na yeye akamuunga mkono kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuwania urais.
Katika video hiyo, Ruto anaendelea kuhutubia rais: “Sasa eti wewe unaanza kuni-threaten mimi. Ati utanifanya nini? Bora usiuwe watoto wangu, lakini mimi na wewe tafadhali tuheshimiane.”
Lakini je, kweli Ruto alichochea jamii ya Wakalenjin, kama inavyodaiwa kwenye nukuu ya video?
- Tunachokijua
- Ukiitazama video nzima hakuna ushahidi wa kuwa Ruto anachochea Wakalenjin dhidi ya Wakikuyu.
Katika video hiyo, Ruto anawasihi watu wasigawanywe na wale wanaopenda kutumia uadui wa kihistoria wa kikabila kati ya jamii hizo mbili.
Hivyo basi, kichwa cha video hiyo kinaonekana kulenga kupotosha muktadha wa video.