Willy Gamba, Hofu, Njama, na E MUSIBA, Mnakumbuka Enzi Hizo?

Willy Gamba, Hofu, Njama, na E MUSIBA, Mnakumbuka Enzi Hizo?

jamani mbuzi mzee fanya mpango nipate nakala mm nilikua nqavyo vyote lakini vilipotea plaase
 
Vinapatikana wapi maana wengine tunaishia kupata simulizi tu, enzi hizo bado tulikuwa bado kijijini na hivi vitabu vilikuwa vinapatikana zaidi mjini.

Msaada wa kuvipata please.
 
Umenikumbusha mbali sana, enzi nikiwa primary nilipenda sana vitabu, niliakikisha kila kitabu cha willy gamba sikikosi, nilikuwa navyo karibu vyoote.
Nilikipenda sana kikosi cha kisasi.

Rip a.e. Musiba
 
Tafrija ya damu cha Jackson Kalindimya...bonge la kitabu loh

Mkuu naweza kukipata wapi hiki? Kwa kweli nilikisoma mara moja then kuna dingi yangu mdogo akanipoka ndiyo imekuwa basi tena make hata yeye aliibiwa. Any clue mkuu??
 
Asubuhi hii niliamka mapema, na baada ya kuoga na kuvaa vizuri niliamua nikastaftahi hapo Palm Beach Hoteli, kwani niliona uvivu kujipikia chai. Kama kuna kitu nachukua ni mambo ya kupikapika.

Nilikuwa mtu wa kwanza kufika Palm Beach Hoteli kwa ajili ya kusitaftahi. Kijana mmoja muuza magazeti alinifuata ndani ya chumba cha chakula na kuniuzia magazeti ya Daily News na Uhuru. Nilipitisha macho kwenye magazeti haya huku nikisubiri niletewe chemsha kinywa.

Magazeti haya yalijaa habari nyingi kama kawaida, lakini habari juu ya tukio lililokuwa limetokea katika wiki hii haikuwemo. Bila shaka ilikuwa imeachwa kwa ajili ya usalama. Nilipoletewa chemsha kinywa niliishambulia haraka haraka, nikalipa na kuondoka kuelekea ofinini. Wakati huo ilikuwa yapata saa moja na nusu.

Nilipokuwa napita karibu na nyumba yangu, mara akili ikanijia kuwa afadhali nichukua bastola yangu kwani nisingeweza kuamini tu kuwa hali ilikuwa ya usalama. Nilirudi nyumbani kwangu, nikachukua bastola moja aina ya 38mm ya kipolisi na kuiweka ndani ya shati langu kwa jinsi ambavyo isingeweza kuonekana kwa urahisi.

Nilichomeka shati vizuri, nikafunga mkanda wa suruali na kuifungia vizuri bastola chini kidogo ya kitovu. Kwa sababu kulikuwa na hali ya mawingu-mawingu nilivaa jaketi juu. Kisha nikaelekea ofisini.

Nilikuta ofisi imeshafunguliwa, nikapita nikawasalimia maofisa wangu wadogo, kisha nikaelekea ofisini kwangu. Linda alikuwa tayari ameshafika.

"Hallo bosi, umelalaje?", Linda alinisalimia nilipofungua mlango na kuingia ndani.

"Safi kabisa, je wee?".

"Mimi ndiye nimelala vizuri kabisa, hata sikuota leo ingawaje mimi ni muotaji".

"Itabidi uwe unalala si chini ya masaa sita, bado mtoto mdogo wewe".

"Sawa, lakini panapokuwa na shughuli maalum sina budi kukesha.

"Kama ndivyo hivyo naona kazi itafanyika".

"Na usiwe na shaka, itafanyika".

"Niitie Eddy aje ofisini kwangu".

"Sawa bosi".

Kwa sababu Namba mbili, tatu na namba nne walikuwa safarini huko Kusini mwa Afrika kwa shughuli maalum, ilibidi katika shughuli hii nishirikiane na kijana Eddy Kisanga, ambaye alijitokeza kuwa kijana shupavu sana katika kazi yetu hii.

Eddy alikuwa kijana mwenye umri wa miaka ishirini na mitatu, lakini alikuwa na akili za kuweza kumiliki matatizo na kujifunza mambo magumu katika kazi yetu hii kwa haraka sana.

Kitu cha kutufurahisha ni kwamba alikuwa mwanafunzi wangu mimi mwenyewe, hivyo matendo yake yalifanana na yangu, kiasi kuwa hapa ofisini aliitwa Willy mtoto.Na yeye alikuwa akifurahi sana kuitwa hivyo.Kwa hiyo nilipopeleka jina lake kwenye kamati ya upelelezi, nikawa nimeweka sifa zake kama mimi haikuwa ajabu kukuta amethibitishwa.

Baada ya kuthibitishwa ilibidi apewe kazi maaum ili kumpima na kuweza kumpa namba. Hivyo yeye na Sammy Rashid namba mbili walikuwa kwenye kazi maalum huko Johannesburg, Afrika Kusini. Kazi hiyo ilitekelezwa vizuri sana, na waliporudi namba mbili alitoa ripoti juu ya kazi hiyo na ikaonekana sehemu aliyofanya Eddy ilimshangaza hata Chifu, Eddy aipewa namba ya juu kuiko wote tuivyotegemea na kutokana na muda wake kazini; Kutoka kwenye kamati ya usalama alipewa namba 'TANO'.

"Eddy yuko hapa", Linda ainieleza kwa simu.

"Mwambie aingie", nilimjibu.

Eddy aiingia ndani nikamuonesha kwa ishara ya mkono avute kiti aketi.

"Habari za leo bosi", alisalimia Eddy.

"Nzuri, habari yako wewe?".

"Ni nzuri".

"Eddy natumaini umesikia jambo lililotokea hapa mjini siku chache zilizopita?".

"Ndio, lakini nimezisikia kwenye radio za nje, na rafiki yangu mmoja polisi wa kituo cha kati, ndiye aiyenielezea kwa kirefu kidogo. Vile vile alinieleza kuwa wao ndio wanapeleleza tukio hili lakini kufikia sasa hawajafika popote. Wanasema mpaka sasa hawajaona au kupata kitu chochote kinachohusika na tukio hilo. Hata hivyo wanasema watajitahidi".

"Kwa kutokana na hali ya namna hiyo serikali imeamua kutupa sisi jukumu hili, ingawa polisi wataendelea na upelelezi kamambe juu ya tukio hilo. Na ndio sababu nimeitwa kurudi mara moja toka likizo. Kwa hiyo toka sasa hivi ahirisha mambo yako mengine yote na tushughulikie tukio hili. Umenielewa?".

"Bila shaka".

Nilianza kumweleza jinsi nilivyoendesha mipango yangu yote nikiwatumia Sherriff na Veronika.

"Kwa hiyo Eddy, ninachotaka wewe ufanye, kwanza, nataka ukodishe magari manne kutoka kwenye kampuni mbali mbali zinazokodisha magari hapa mjini kama vile Co-cabs, Safari Toures Afrika Ltd., Takim's Agancies, nk. Gari moja kati hizi liegeshe mahali pa kuegesha magari New Afrika Hoteli na lingine liegeshe Kilimanjaro Hoteli. Magari mawili yatakayobaki nataka wewe pamoja na kijana mwingine kati yetu mtufuate kila mahali tutakapokwenda leo. Lakini mtufuate kwa siri kabisa kiasi kwamba mtu yeyote asitambue kama mnatufuata sisi. Mimi nitatumia gari langu. Nia yangu nataka muwe macho kama kuna watu wengine watakaoweza kuwa wanafuata safari yetu kwa siku ya leo. Umeelewa?".

"Nimeelewa vizuri kabisa bosi. Kazi itatekelezwa. Si ajabu hata wewe hutatuona."

"Kazi ya namna hiyo ndio nataka".

"Utapata, bosi."

"Gari zile utakazoziegesha New Afrika na Kilimanjaro Hoteli, weka swich ya gari hizi chini ya zuria kwa upande anaotoka dereva."

"Nitafanya hivyo."

"Haya sasa nenda ukashughulike na kazi hii ili saa nne muwe tayari nje ya New Afrika Hoteli ambapo ndipo tutaanza safari yetu."

"Tutakuwa hapo saa hizo, usiwe na wasiwasi".

ITAENDELEA
 
Niiegesha gari langu kwenye maegesho ya Hoteli ya New Afrika. Nikatelemka na kuzunguka ili nimfungulie Veronika. Tuliingia New Afrika Hoteli katika sehemu iitwayo duka la Kahawa tukatafuta meza tukaa.

"Ulishastafutahi?", nilimuuliza Veronika.

"Kawaida yangu huwa ninastafutahi kabla ya kufanya mazoezi kila siku, ili kujiweka katika hali nzuri".

"Ndio sababu umbo lako linapendeza namna hiyo".

"Asante".

Mtumishi wa hoteli alifika na kutuuliza mahitaji yetu.

"Mimi nitakunywa maji ya machungwa kama yapo".Veronika alisema.

"Mimi niletee maji ya ndimu". niliagiza.

Alipoondoka mtumishi huyo nilimweleza Veronika kuwa mimi nitakwenda mapokezi kumwita Sherriff, ambaye niliamini alikuwa bado chumbani.

"Habari za leo Tom?", nilimsalimia kijana wa mapokezi ambaye tunafahamiana vizuri sana.

"Aha mzee, shikamoo", alinisalimia.

"Marahaba", nilimjibu.

"Sijui nikusaidie nini mzee?".

"Kuna mgeni wangu hapa anaitwa Ahmed Sherriff, alifika usiku".

"Ndio ndio, yuko yuko namba 406, unahitaji kwenda huko au nimpigie simu".

"Mpigie simu nizungumze nae".

Alimpigia simu na alipompata akanipa.

"Hallo Sherriff habari za leo?".

"Ohoo, Willy salama?, nilikuwa ninakusubiri kwa hamu".

"Oke, telemka chini. Tuko hapa duka la kahawa pamoja na Veronika".

Oh, amekwisha wahi namna hii?".

"Sana tena".

"Oke nakuja sasa hivi".

"Haya tunakusubiri", nilimjibu na kukata simu.

"Oke Tom asante sana", nilimwambia kijana wa mapokezi.

"Asante mzee karibu", alijibu Tom.

"Asante niko hapa duka la kahawa".

Niliporudi nilikuta vinywaji tayari.

"Yupo?", aliuliza Veronika.

"Yupo, anakuja sasa hivi", nilimjibu.

ITAENDELEA...
 
Aebq2fKJt02fAAAAAElFTkSuQmCC

NJAMA
VERONIKA NA SHERRIFF II

ILIKUWA saa tatu kamili niliposimama mbele ya chumba namba 208 katika ghorofa ya pili ya hoteli ya Kilimanjaro, niligonga mlango mara mbili haraka haraka, halafu nikatulia kidogo kisha nikagonga tena. Hivi ndivyo nilivyokuwa nimeelekezwa.

"Karibu", nilisikia sauti kali ya juu ikitokea ndani ya nyufa za mlango. Nilifungua nikajikuta katika sebule ya chumba hiki ambamo Veronika alikuwa amevaa kaputula na sidiria tu akifanya mazoezi ya viungo. Alikuwa ameelekea upande mwingine na kunionesha mgongo na kuendelea na mazoezi yake kama kwamba hakuna mtu aliyeingia. Nilirudisha mlango, nikauegemea na kutazama jinsi binti huyu alivyokuwa akichukua mazoezi.

"Karibu Willy Gamba, kaa kwenye kiti upumzike", alinielekeza bila kugeuka na huku akiendelea na mazoezi yake. Kisha akaanza kusema kana kwamba anajizungumzia yeye peke yake.

"Willy Gamba anayejiita mfanyabiashara huku ni mpelelezi mashuhuri wa Afrika. Afadhali ningejua mapema naamini ingekuwa furaha kubwa kuonana na mtu huyu mashuhuri nyumbani kwetu. Lakini nimekuja kujua mjini London katika ofisi za gazeti la 'Afrika', hasa ni hii teknolojia iliyoingia ulimwenguni maana tumeelekezwa na komputa ya pale ofisini. Sherriff aikuwa na mashaka kuwa amewahi kusikia jina la Willy Gamba mahali. Hivyo kufika tu London akailisha komputa hiyo jina la Willy Gamba. Maana komputa hiyo imeweka kwenye ubongo wake waandishi wote maarufu wa habari, wapelelezi wote maarufu ulimwenguni, wakubwa wote wa serikali mbali mbali na watu wote maarufu katika nyanja mbali mbali.

"Lo! alipoilisha jina hili ndipo ikatutolea maajabu. Ilionyesha kuwa Willy Gamba mwenye umri wa miaka ishirini na tisa, mwenye urefu wa futi tano na inchi kumi na mwenye umbo la kupendeza sana ni mpelelezi maarufu ulimwengu mzima. Iliendelea kusema kuwa Willy Gamba amehitimu katika chuo kikuu cha Dar es Salaam na kupata shahada katika sheria. Baada ya kutoka chuo kikuu moja kwa moja aliteuliwa kwenda kujifunza mambo ya upelelezi kwa kutokana na sifa zake alizoandikiwa na wakubwa wa Jeshi la Kujenga Taifa, wakati akiwa katika Jeshi hilo".

"Komputa ilieleza kuwa Willy Gamba anasemekana amepata mafunzo katika nchi mbali mbali kama vile Uingereza, Cuba, Urusi, Marekani, China na Japan. Kutokana na mafunzo haya amejulikana kama mtu hatari katika kutumia aina yoyote ya silaha. Vile vile anajua karate na Kung-fu ya hali ya juu kwani wakati akiwa Japan aliwahi kushindana na Inoki na kutoka sare naye. Watu wanashangaa kwanini hakuendelea maana bila shaka sasa angekuwa bingwa wa dunia. Zaidi ya yote anaaminika kuwa amehitimu mafunzo ya kikomandoo. Komputa ilizidi kuonesha kuwa Willy Gamba ana I.Q ya hali ya juu sana, hivi sasa ni mtu anayeweza kusokoroa matatizo yaliyojisokota sana. Na iliendelea kuonyesha kuwa ameifanyia 'OAU' kazi nzuri sana hasa kuhusiana na Ukombozi wa Afrika Kusini".

Alipofika hapa alinyamaza, kisha kama umeme alikatisha mazoezi yake na kunigeukia na kurukia kifuani pangu kwani bado nilikuwa nimesimama mlangoni nikisikiliza kwa makini.

"Kwanini usinieleze toka mwanzo Willy mpenzi, kwanini?".

Nilimkumbatia kifuani kwangu na badaa ya kujibu swali lake nilisema. "Veronika Amadu".
Aliinua macho akaniangalia usoni, mimi bila kusita niliendelea. "Mwandishi maarufu wa gazeti la "Afrika", Veronika Amadu mwenye umri wa miaka ishirini na sita, mwenye urefu wa futi tano na inchi tano, mwenye macho na umbo la kupendeza la vipimo 38'-22'-36'. Alihitimu katika Chuo Kikuu cha Ibadani nchini Nigeria na kupata shahada katika uandishi, baada ya kuhitimu aiajiriwa na gazeti la 'Newsweek' la Marekani, akiwa mwandishi wao katika Afrika Magharibi. Kwa vile gazeti lilitaka kumtumia mwandishi huyu kupata habari zingine ambazo kuzipata kwake itabidi uhatarishe maisha yake, lililazimika kumpeleka Japan kujifunza namna ya kujikinga kwa mikono, hatari yoyote itokeapo, hivyo mwandishi huyu amehitimu katika Judo na Karate na kupata mkanda mweusi. Baada ya kuwa na gazeti hili kwa muda mrefu aliacha na kujiunga na gazeti a Afrika. Anajuikana kuwa msichana mwandishi jasiri sana, amewahi kusafiri na majeshi ya Chama cha wapigania uhuru wa Sahara Magharibi kiitwacho "The Popular Front for the Liberation of Saguiet el-Hamara na Rio de Oro" yaani "POLISARIO", katika mapambano yao dhidi ya majeshi ya Morocco ambayo yameshika sehemu hiyo, inasemekana mwandishi huyu alikaa na majeshi haya na kuandamana nayo katika uwanja wa mapambano kwa muda wa miezi sita na kuwa mwandishi wa kwanza kuandika habari kamili za mapambano haya akiwa shahidi wa macho. Je unasemaje Veronika Amadu".

"Sasa naamini kabisa wewe ndiye Willy Gamba, maana mimi nilifikiri tumekutangulia kumbe wewe ndiye umetutangulia zaidi. Naamini hata Sherriff sasa umamfahamu kama nyuma ya kiganja chako hebu nieleze".

Nilimweleza. "Ahmed Sherriff mwandishi mashuhuri wa gazeri la Afrika hasa juu ya mapambano ya Kusini mwa Afrika. Ahmed Sherriff mwenye umri wa miaka thelathini na mbili, mwenye urefu wa futi tano na inchi kumi na moja na mwenye masharafa mengi, alihitimu katika Chuo kikuu cha Patrick Lumumba mjini Moscow, Urusi. Baada ya kuhitimu kwake alipotea isijulikane aliko kwa muda wa mwaka mmoja. Lakini habari za kuaminika zinasema kwamba alikuwa akichukua mafunzo ya kijeshi katika kambi za kijeshi za Wapalestina huko Mashariki ya Kati. Baada ya kuonekana alipatiwa kazi moja kwa moja na gazeti la Afrika ambalo linaaminika lilipata fununu juu ya mafunzo ya kijeshi ya Sherriff huko Mashariki ya Kati. Kwani baada ya kumwajiri tu alipelekwa moja kwa moja Kusini mwa Afrika ambako aliandamana na majeshi ya wapigania uhuru wa Frelimo, MPLA na siku hizi anaandamana na majeshi ya SWAPO katika uwanja wa mapambano huko Namibia.

"Vile vile kuna habari zinazosema kuwa alikuwepo katika mkasa uliotokea Soweto na ndiye aliyeandika habari za kuaminika juu ya tukio hilo. Hivyo ujasiri wake huu umemfanya kuwa mwandishi maarufu sana anayechukiwa sana nan tawala dhalimu za Afrika Kusini na Rhodesia na nchi zote zinazopinga mapinduzi ya Afrika na harakati zake za kujikomboa kutokana na ubeberu. Umeridhika sasa."

"Sasa naamini ukiambiwa mtu ana I.Q ya hali ya juu, lazima utambue kuwa kwa kila jambo unalotaka kufanya yeye yuko hatua nyingi mbele yako", Veronika alijibu na kuanza kunibusu huku midomo yake ikiwa ya chumvi chumvi sababu ya mazoezi.

"Ngoja nioge mara moja ili tukaonane na Sherriff tukaanze mazungumzo yetu ya kwanza."

"Sawa". Aliniacha na kwenda maliwatoni. Mimi nikabaki katika mawazo makali jinsi ya kuanza kulishambulia tatizo hili.

INAENDELEA
 
Umenikumbusha mbali sana, nilikisoma kitabu hiki kitambo sana, hata sikumbuki kama nilikuwa Form one au Primary; ni miongoni mwa vitabu vyangu vya mwanzo kuvisoma mfululizo bila kupitisha siku, maana hata njaa haikuuma zaidi ya kutetemeka kwa hisia za kizalendo zilizoonyeshwa na mwandishi. Nilkuwa nikijua ni stori ya kweli kabisa. Ubaya wa vitabu vya Willy Gamba, ni kwamba ukimuazima mtu ujue kimepotea, ndivyo vilivyopote vitabu vyangu vya huyu jamaa. Nilipokisoma kitabu hiki nilitetemeka mwili mzima na nililia alipokufa Veronika Hamadu maskni. Ajabu ni kwamba, niliposoma hizi page ulizoweka still natetemeka na naikumbuka Tanzania iliyokuwa ikiogopa fedheha na Tanzania ya leo ya wapelelezi kina R. Ighondu. Nadhani juhudi zifanyike ya kurudisha vitabu vya zamani kuliko hivi wanavyosoma watoto wa leo vya akina Nyangwine. Thanks mleta mada
 
Vinapatikana wapi maana wengine tunaishia kupata simulizi tu, enzi hizo bado tulikuwa bado kijijini na hivi vitabu vilikuwa vinapatikana zaidi mjini.

Msaada wa kuvipata please.
Pole ndugu yangu, sjui ni nani aliyefanya hivi vitabu visiwepo sokoni. Ni miongoni mwa vitabu vinavyojenga uzalendo wa hali ya juu na kujumuisha masuala mengi ya kiujumla. Ungana na mbuzi mzee naona kama utafarijika kidogo japo ilipendeza kuvisoma wakati majukumu hayajaanza na nchi haijaharibika kama leo, otherwise jiandae kupata stroke
 
Ahsante Mkuu kwa kutukumbusha hizi tamthilia, kasheshe ilikuwa KUFA NA KUPONA jamaa anakupeka na kukupa ramani ya Nairobi hata kama hujawahi kwenda huko!!!!

Na sidhani kama kulikuwa teknolojia kubwa ya google map or whatever kama hivi leo
 
Aebq2fKJt02fAAAAAElFTkSuQmCC

NJAMA
VERONIKA NA SHERRIFF II

ILIKUWA saa tatu kamili niliposimama mbele ya chumba namba 208 katika ghorofa ya pili ya hoteli ya Kilimanjaro, niligonga mlango mara mbili haraka haraka, halafu nikatulia kidogo kisha nikagonga tena. Hivi ndivyo nilivyokuwa nimeelekezwa.

"Karibu", nilisikia sauti kali ya juu ikitokea ndani ya nyufa za mlango. Nilifungua nikajikuta katika sebule ya chumba hiki ambamo Veronika alikuwa amevaa kaputula na sidiria tu akifanya mazoezi ya viungo. Alikuwa ameelekea upande mwingine na kunionesha mgongo na kuendelea na mazoezi yake kama kwamba hakuna mtu aliyeingia. Nilirudisha mlango, nikauegemea na kutazama jinsi binti huyu alivyokuwa akichukua mazoezi.

"Karibu Willy Gamba, kaa kwenye kiti upumzike", alinielekeza bila kugeuka na huku akiendelea na mazoezi yake. Kisha akaanza kusema kana kwamba anajizungumzia yeye peke yake.

"Willy Gamba anayejiita mfanyabiashara huku ni mpelelezi mashuhuri wa Afrika. Afadhali ningejua mapema naamini ingekuwa furaha kubwa kuonana na mtu huyu mashuhuri nyumbani kwetu. Lakini nimekuja kujua mjini London katika ofisi za gazeti la 'Afrika', hasa ni hii teknolojia iliyoingia ulimwenguni maana tumeelekezwa na komputa ya pale ofisini. Sherriff aikuwa na mashaka kuwa amewahi kusikia jina la Willy Gamba mahali. Hivyo kufika tu London akailisha komputa hiyo jina la Willy Gamba. Maana komputa hiyo imeweka kwenye ubongo wake waandishi wote maarufu wa habari, wapelelezi wote maarufu ulimwenguni, wakubwa wote wa serikali mbali mbali na watu wote maarufu katika nyanja mbali mbali.

"Lo! alipoilisha jina hili ndipo ikatutolea maajabu. Ilionyesha kuwa Willy Gamba mwenye umri wa miaka ishirini na tisa, mwenye urefu wa futi tano na inchi kumi na mwenye umbo la kupendeza sana ni mpelelezi maarufu ulimwengu mzima. Iliendelea kusema kuwa Willy Gamba amehitimu katika chuo kikuu cha Dar es Salaam na kupata shahada katika sheria. Baada ya kutoka chuo kikuu moja kwa moja aliteuliwa kwenda kujifunza mambo ya upelelezi kwa kutokana na sifa zake alizoandikiwa na wakubwa wa Jeshi la Kujenga Taifa, wakati akiwa katika Jeshi hilo".

"Komputa ilieleza kuwa Willy Gamba anasemekana amepata mafunzo katika nchi mbali mbali kama vile Uingereza, Cuba, Urusi, Marekani, China na Japan. Kutokana na mafunzo haya amejulikana kama mtu hatari katika kutumia aina yoyote ya silaha. Vile vile anajua karate na Kung-fu ya hali ya juu kwani wakati akiwa Japan aliwahi kushindana na Inoki na kutoka sare naye. Watu wanashangaa kwanini hakuendelea maana bila shaka sasa angekuwa bingwa wa dunia. Zaidi ya yote anaaminika kuwa amehitimu mafunzo ya kikomandoo. Komputa ilizidi kuonesha kuwa Willy Gamba ana I.Q ya hali ya juu sana, hivi sasa ni mtu anayeweza kusokoroa matatizo yaliyojisokota sana. Na iliendelea kuonyesha kuwa ameifanyia 'OAU' kazi nzuri sana hasa kuhusiana na Ukombozi wa Afrika Kusini".

Alipofika hapa alinyamaza, kisha kama umeme alikatisha mazoezi yake na kunigeukia na kurukia kifuani pangu kwani bado nilikuwa nimesimama mlangoni nikisikiliza kwa makini.

"Kwanini usinieleze toka mwanzo Willy mpenzi, kwanini?".

Nilimkumbatia kifuani kwangu na badaa ya kujibu swali lake nilisema. "Veronika Amadu".
Aliinua macho akaniangalia usoni, mimi bila kusita niliendelea. "Mwandishi maarufu wa gazeti la "Afrika", Veronika Amadu mwenye umri wa miaka ishirini na sita, mwenye urefu wa futi tano na inchi tano, mwenye macho na umbo la kupendeza la vipimo 38'-22'-36'. Alihitimu katika Chuo Kikuu cha Ibadani nchini Nigeria na kupata shahada katika uandishi, baada ya kuhitimu aiajiriwa na gazeti la 'Newsweek' la Marekani, akiwa mwandishi wao katika Afrika Magharibi. Kwa vile gazeti lilitaka kumtumia mwandishi huyu kupata habari zingine ambazo kuzipata kwake itabidi uhatarishe maisha yake, lililazimika kumpeleka Japan kujifunza namna ya kujikinga kwa mikono, hatari yoyote itokeapo, hivyo mwandishi huyu amehitimu katika Judo na Karate na kupata mkanda mweusi. Baada ya kuwa na gazeti hili kwa muda mrefu aliacha na kujiunga na gazeti a Afrika. Anajuikana kuwa msichana mwandishi jasiri sana, amewahi kusafiri na majeshi ya Chama cha wapigania uhuru wa Sahara Magharibi kiitwacho "The Popular Front for the Liberation of Saguiet el-Hamara na Rio de Oro" yaani "POLISARIO", katika mapambano yao dhidi ya majeshi ya Morocco ambayo yameshika sehemu hiyo, inasemekana mwandishi huyu alikaa na majeshi haya na kuandamana nayo katika uwanja wa mapambano kwa muda wa miezi sita na kuwa mwandishi wa kwanza kuandika habari kamili za mapambano haya akiwa shahidi wa macho. Je unasemaje Veronika Amadu".

"Sasa naamini kabisa wewe ndiye Willy Gamba, maana mimi nilifikiri tumekutangulia kumbe wewe ndiye umetutangulia zaidi. Naamini hata Sherriff sasa umamfahamu kama nyuma ya kiganja chako hebu nieleze".

Nilimweleza. "Ahmed Sherriff mwandishi mashuhuri wa gazeri la Afrika hasa juu ya mapambano ya Kusini mwa Afrika. Ahmed Sherriff mwenye umri wa miaka thelathini na mbili, mwenye urefu wa futi tano na inchi kumi na moja na mwenye masharafa mengi, alihitimu katika Chuo kikuu cha Patrick Lumumba mjini Moscow, Urusi. Baada ya kuhitimu kwake alipotea isijulikane aliko kwa muda wa mwaka mmoja. Lakini habari za kuaminika zinasema kwamba alikuwa akichukua mafunzo ya kijeshi katika kambi za kijeshi za Wapalestina huko Mashariki ya Kati. Baada ya kuonekana alipatiwa kazi moja kwa moja na gazeti la Afrika ambalo linaaminika lilipata fununu juu ya mafunzo ya kijeshi ya Sherriff huko Mashariki ya Kati. Kwani baada ya kumwajiri tu alipelekwa moja kwa moja Kusini mwa Afrika ambako aliandamana na majeshi ya wapigania uhuru wa Frelimo, MPLA na siku hizi anaandamana na majeshi ya SWAPO katika uwanja wa mapambano huko Namibia.

"Vile vile kuna habari zinazosema kuwa alikuwepo katika mkasa uliotokea Soweto na ndiye aliyeandika habari za kuaminika juu ya tukio hilo. Hivyo ujasiri wake huu umemfanya kuwa mwandishi maarufu sana anayechukiwa sana nan tawala dhalimu za Afrika Kusini na Rhodesia na nchi zote zinazopinga mapinduzi ya Afrika na harakati zake za kujikomboa kutokana na ubeberu. Umeridhika sasa."

"Sasa naamini ukiambiwa mtu ana I.Q ya hali ya juu, lazima utambue kuwa kwa kila jambo unalotaka kufanya yeye yuko hatua nyingi mbele yako", Veronika alijibu na kuanza kunibusu huku midomo yake ikiwa ya chumvi chumvi sababu ya mazoezi.

"Ngoja nioge mara moja ili tukaonane na Sherriff tukaanze mazungumzo yetu ya kwanza."

"Sawa". Aliniacha na kwenda maliwatoni. Mimi nikabaki katika mawazo makali jinsi ya kuanza kulishambulia tatizo hili.

INAENDELEA

Hapa kama umechanganya kidog, hiki kitabu nakijua vyema nadhani hii ilitakiwa iwe mwanzo kabla ya kuegesha gari kwani baada ya kutoka Kilimanjaro ndipo wakaenda New Afrika Hotel alikokuwa amefikia Ahmed Shariff, ndipo Willy Gamba alipoenda kumuulizia na kumwambia kuwa wao wamekwishafika lol!
 
Enzi hizi ndo zilikua enzi hasaa. Kusoma lazima kama hutaki ngojea kuhadithiwa riwaya matata

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom