Wilson Oruma: MO anataka 67bl zitambulike kama ni deni analoidai Simba kabla hajatoa hela za usajili msimu huu

Itakuwa watu walishapita nazo sasa kuwataja ndiyo kigugumizi sasa ikisemwa ni deni watu ndiyo waamke kufunkunyua huko kunani!?
 
Watu wengi hawajui maana ya uwekezaji ndio maana wakati diamond anamdai harmonize billion moja wabongo wengi walilalamika ila investing is risky hata GSM ndio haya ya kina mzee magoma.
Two different scenarios....

Mo alitoa 20B kupata 49% ya SSC ambayo Bado anaimiliki, hizo 67B alitoa Kwa condition gani? Mkopo ah investments? Na Kwa mantiki hio Ina maana ndani ya miaka Saba Mo atakua hajawahi kupata hata a single coin kutoka Kwa Simba? Na matangazo yake yote pamoja na kanga alizotengeneza Kwa kutumia Simba kama brand anawalipa cash.....



Simba Bado asilimia 51 ni timu ya wananchi, na wananchi Wana watu wao kwenye bodi ambao wanawajibikia Kwa wanachama wa SSC sio Kwa mo, hizo pesa anatoa Kwa transparency gani? Kama wanapeana pesa uchororoni ndo itakula kwake..... Mo kashawapiga Sana Simba, Simba Leo hii si ya miaka Saba nyuma iliyopita, Ina maana Leo Simba ikisema iuze hisa zake mo hatopata faida? Simba hii ambayo kina jay rutty wanaweka b33 Kwa misimu miwili???
 
Tanzania ni nchi ya yenye uhuru uliopotiliza. Watu wanaleta uzushi na kila mtu anaamini na kutukana bila ushahidi wowote. Hata chizi anaweza kusema kitu cha kipumbavu na watu wakaamini.
 
kapuku kama huyo oruma ndio anaweza kuhoji mchango wa mo simba?
 
Usijadili kitu bila kujua hiyo habari ni authentic au la. Oruma kasema hivyo wapi? Au kila kitu mnacholetewa mnameza tu?
 
Usijadili kitu bila kujua hiyo habari ni authentic au la. Oruma kasema hivyo wapi? Au kila kitu mnacholetewa mnameza tu?
Mjadala wangu hauna uhusiano na huyo Oruma(wtf is he kwanza?)


Mjadala wangu umelenga hoja Mo alizoleta juzi, na hoja kubwa ni kwamba sawa katumia 87B siwezi kukataa, yeye kapata ngapi na mpaka Sasa thamani ya hisa 49% ni ngapi?
 
Shida unaongea kishabiki siku yakija ya GSM ndio utaona kuwekeza sio rahisi kiasi hicho tena kule ndio kumeoza kabisa sisi yetu macho wewe uliyekunywa maji ya bendera endelea kukaza shingo.
 

Huyu na aliyekuwa akijiita mwamba CDM baba mmoja mama mmoja. Wapo kifursa zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…