Wimbi kubwa la wahitimu tegemezi wanaomaliza vyuo wasioweza kujitegemea, kuna faida ya kuwa na elimu ya chuo kama huwezi kujilisha?

Wimbi kubwa la wahitimu tegemezi wanaomaliza vyuo wasioweza kujitegemea, kuna faida ya kuwa na elimu ya chuo kama huwezi kujilisha?

Hakuna system ambayo kila mtu anaweza kujiajiri hata wewe unayedhani umejiajiri ni kwamba indirectly umeajiriwa na mteja wako..., sasa kwa nchi ambayo watu hawana disposable income kutokana na kwamba hakuna sekta zenye nguvu zaidi ya madalali na wachuuzi from top to bottom ni kwamba hakuna sustainability.

In short tunatibu au kutaka kutibu symptoms badala ya ugonjwa...; Kwahio hata hawa wauguzi na wakufunzi ambao bado kama taifa hawatoshi na tumetumia pesa nyingi kuwafundisha wakimaliza tuwafundishe kuuza mihogo au wafungue shule na hospitali zao (yaani tuongeze quantity na sio quality)
 
Umeongea fact, aibu yako ndo umaskini wako
Tunawaona wahitimu wengi sana wakibaki majumbani au kwenda kwa dada zao walioolewa baada ya kuhitimu.

Speaking from experience vijana wengi baada ya kumaliza chuo huanza kuomba ajira bila mafanikio (hawana connection, hawana experience), mwaka unakatika wanaona kujitolea (volunteering) kwenye mashirika ili kupata experience ya cv ila ni kwa gharama zao hivyo wanaishi nyumbani, miaka inakatika bado bila bila familia zinawapa mitaji lakini akili bado zipo kwenye ajira hawapo serious na biashara mwisho wanafunga wanarudi from scratch, kelele zinakuwa nyingi huhamisha makazi kwa kina dada au ndugu wengine, wale wa kike kipindi hiki wanakuwa very vulnerable kuolewa iwe njia ya kuondoka.

Sababu kubwa inayopelekea hali hii ni kukosa ujuzi na uthubutu wa kufanya shughuli za kujiingizia kipato nje ya kazi walizosomea vyuoni na kuona aibu kufanya baadhi ya shughuli wanazohisi haziendani na hadhi ya elimu yao.

SOLUTION
1. Vijana wajiandae na maisha baada ya chuo, kwenye hizi likizo na weekends wawe wanajifunza na kuomba kuajiriwa kwenye mashamba, ofisi za kunyoa, kusuka, kuendesha boda, kupika, n.k.

2. waweke aibu pembeni wapige kazi, kuna stigma kwenye jamii zetu wahitimu wanahisi kuna kazi hawatakiwi kufanya kama kunyoa, kusuka, kuendesha boda, n.k.
 
Bado tunasikilizia 2025 wata achia nyingi sanaaaa
 
Back
Top Bottom