Wimbi la ‘single mothers’, wa kulaumiwa zaidi ni Wazazi na Serikali

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Siku za hivi karibuni single mothers wamekuwa wakilaumiwa, kukejiliwa na kurushiwa maneno mengi ila ukweli ni kwamba wao ni matokeo tu na sio sahihi kuwananga wao badala ya kuangalia chanzo.

Ukweli ni kwamba chanzo kikubwa cha single mothers ni wazazi kushindwa kuwahudumia watoto wao wa kike na kuwasababisha kuwa tegemezi hata kwa vitu vidogo kama pedi na mafuta kutoka kwa vijana waganga njaa na wanaume watu wazima wenye pesa.

Jambo lingine ni hali ngumu ya kiuchumi isiyosapoti maisha ya familia inayowakabili vijana wengi na hapa serikali inawajibika moja kwa moja, vijana wengi hawana pesa za kulea familia kwa hiyo wanabaki kuhonga vipesa vidogo vidogo kufanya ngono na kuzalisha kiholela tu.

Yasiporekebishika haya mawili kelele za mabinti wanaozaa na kubaki single mothers zitaendelea kupigwa daima.
 
Wazazi mnawahusisha vipi kwenye starehe za watu wazima?

Watu mpaka wanapatana wawe wapenzi na kuanza kugusanisha vikojoleo vyao, ni watu wazima na wengi wana elimu nzuri tuu. 😊

Watu wamekutana kwenye starehe, wamepeana mimba na kukimbiana, wazazi hapo walaumiwe kwa lipi mkuu?
 
Kuna single mothers wengi sana wadogo miaka 17-22, Hawa ndio ninowazungumzia zaidi na sio single mothers wakubwa wanaojiweza wanaoamua kuwa hivyo baada ya kuchelewa kuolewa.
 
Kuna single mothers wengi sana wadogo miaka 18-22, Hawa ndio ninowazungumzia zaidi na sio single mothers wakubwa wanaojiweza wanaoamua kuwa hivyo baada ya kuchelewa kuolewa.

Kama utazungumzia chini ya 18 no sawa, lakini binti wa miaka 20,21, 22 ni mtu yupo chuo kikuu kabisa huyo, ana akili timamu kabisa. 😊
 
Daaaah hawa watu tuwapumzishe jamani
 
Serikali haihusiki haitahusika na malezi ya watoto.
Serikali ndio Ulimwengu.
Usipofunzwa na Mamaako basi mifumo ya dunia itakufunza. Serikali ni sehemu ya hiyo mifumo.

Serikali KAZI yake ni kukusanya Kodi, ulinzi, huduma za kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Mtoto usipomfunza serikali itanufaika kwa makosa na uzembe wenu.
 
Shida inafanya vipi mtu azalishwe?
Hebu elezea kidogo.

Mtu anafika chuo,
Miaka zaidi ya 10 anafundishwa uzazi wa mpango anabebaje mimba?

Serikali inatoa huduma za uzazi wa mpango bure. Inapoteza mabilioni ya pesa kusomesha, kutoa madawa na vifaa vya uzazi wa mpango bure.

Leo ianze kukimbizana na ujinga, upuuziaji, uzembe wa watoto wakaidi?
 
uko sahihi 100% kwa upande moja dhidi ya anaestahili lawama zaidi ambae ni mzazi au wazazi wa hao single mothers kwa malezi ya hovyo kwa mabinti zao.

but kwa upande wa pili you are very wrong kwa 100%,
kulaumu serikali sikivu ya CCM dhidi ya hiyo nonsense ya single mothers.

Kwa mfano,
kwani huyo single mother alipokua ana nyanduliwa alipewa kibali na serikali cha kunyanduliwa? au serikali ilikua ndio shahidi wakati ananyanduliwa?

Inafaa watu wazingatie maadili na kuhakikisha wana malengo na uwezo wa kuhudumia athari za zitakazotokana na kunyanduliwa kwao na sio visingizio useless.

kwahiyo hata ukipata U.T.I sugu unakuja kuilamu serikali, right?🐒
 

Ajabu mkuu, sisi tulikuwa tunawekewa boksi za kondomu kwenye ma hosteli...
NGO's kibao zinatoa elimu pale. Cha kushangaza watu wanapigana mimba pale afu mmoja anamwachia mwenzie mzigo wa kulea.
Tumemaliza chuo watu kibao ni wazazi. 😊
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…