Wimbi la ‘single mothers’, wa kulaumiwa zaidi ni Wazazi na Serikali

Wimbi la ‘single mothers’, wa kulaumiwa zaidi ni Wazazi na Serikali

Kama utazungumzia chini ya 18 no sawa, lakini binti wa miaka 20,21, 22 ni mtu yupo chuo kikuu kabisa huyo, ana akili timamu kabisa. 😊
Fikiria binti wa miaka 18-22 yuko chuo hana boom na wazazi wake kumpa pesa za matumizi ni kwa kuungaunga sana halafu anakutana na mume wa mtu anamuhudumia kila kitu, kuanzia vipodozi, chakula, gesi mpaka kodi ya nyumba
 
Uzazi wa mpango si upo, kwanini umbebe mimba mwanaume ambaye hana uwezo wa kutunza mke na watoto

Condomu ni gharama, sawa vipi Kalenda nayo hamjui kutumia??

Kumwaga nje nayo vijana hamuwezi?? Mimi nimetumia njia hii na bibi yenu kwa watoto wote tuliozaa
Serikali siku hizi tangu jiwe aingie madarakani iliacha kuhamasisha uzazi wa mpango, huwezi kusikia tena hizo habari kwenye redio au mashuleni. Mabinti wengi sana hawajui jinsi ya kupanga uzazi wa mpango au wana elimu mbalimbali potofu kuhusu uzazi wa mpango.
 
Tamaa na Mawazo Panzi ya kuwaza vitu vinapatikana kizembe na mambo yanakuwaga kama vile wanavyowish kwenye Muvi zao vichwani.

Hapo ni suala la mtu na akili yake binafsi kama Intelijensia mbovu inasapoti Tabia mbovu ambazo hata wazazi waliamua kuanzisha vita na bado jitu likabinda kuelewa.
Nini kumhusisha mzazi.

Acha vijana wasio wavumilivu na ujanja ujanja wa kipuuzi wainjoi matunda ya Uwekezaji wao.
 
Serikali siku tangu jiwe aingie madarakani iliacha kuhamasisha uzazi wa mpango, huwezi kusikia tena hizo habari kwenye redio au mashuleni. Mabinti wengi sana hawajui jinsi ya kupanga uzazi wa mpango au wana elimu mbalimbali potofu kuhusu uzazi wa mpango.
Kwa haya masimango wanayopewa masingle mom, kuna haja tuwape elimu ya uzazi wa mpango vijana wetu

Haiwezekani binti wa miaka 23 asijue kuhusu uzazi wa mpango wakati njia za kutumia zipo nyingi

Miaka ya zamani, wakati kondomu ghali, hakuna sindano wala vimti, mabinti wengi wa miaka ile walikuwa wakitumia majivu kujilinda na mimba

Familia nyingi wanatumia Mkaa kupika, ina maana watashindwa hata hayo kutumia
 
Shida inafanya vipi mtu azalishwe?
Hebu elezea kidogo.
binti anafika chuo, mahitaji yanakuwa mengi, wazazi hawajali tena, saa nyingine hawana cha kucontribute, binti anakomaa inafika muda anazidiwa sasa hapo ni either ajiunge na kundi la wadangaji na kuchoropoa mimba, au kwa ushamba wake apate ki-bf cha kawaida wadate kwa kuahidiana ndoa, hapa mara nyingi wanaishia kuishi pamoja kupunguza cost of living,hapo ndipo binti atabeba mimba kwa kuendekeza mapenzi chuoni au baada ya masomo! Akiamini kumfanyia hivyo bwana mdogo ndio kutazidisha mapenzi! Ndio matokeo yake anakuja kubumburuka sio hivyo adhahaniavyo!
 
Siku za hivi karibuni single mothers wamekuwa wakilaumiwa, kukejiliwa na kurushiwa maneno mengi ila ukweli ni kwamba wao ni matokeo tu na sio sahihi kuwananga wao badala ya kuangalia chanzo.

Ukweli ni kwamba chanzo kikubwa cha single mothers ni wazazi kushindwa kuwahudumia watoto wao wa kike na kuwasababisha kuwa tegemezi hata kwa vitu vidogo kama pedi na mafuta kutoka kwa vijana waganga njaa na wanaume watu wazima wenye pesa.

Jambo lingine ni hali ngumu ya kiuchumi isiyosapoti maisha ya familia inayowakabili vijana wengi na hapa serikali inawajibika moja kwa moja, vijana wengi hawana pesa za kulea familia kwa hiyo wanabaki kuhonga vipesa vidogo vidogo kufanya ngono na kuzalisha kiholela tu.

Yasiporekebishika haya mawili kelele za mabinti wanaozaa na kubaki single mothers zitaendelea kupigwa daima.
Umeandika vizuri ILA umesahau moja
Shinikizo la kuoa mke moja, nalo limechangia pakubwa tu
Mwaka juzi; kenya walifanya reseach na kugundua kuwa, Mombasa ambapo walio wengi ni Waislam wanao oa wake wengi; Idadi ya single mother na watoto wa mtaani ni wachache sana
ILA miji mingine kama Kisumu, nk ambapo madhehebu mengine ndio wapo wengi takriban 95%, single mother na watoto wa mtaani ni wengi sana; Nairobi pia ilionesha takwimu hizo hizo hadi baadhi ya wabunge (wanawake) wakawa wanashawishi bunge lipitishe sheria ya kuoa wake wengi.....
 
Unawatukana wanawake, unasema kwamba;

1. Wanawake ni wajinga mno mpaka wanajirahisisha kubeba mimba ili kuepuka njaa.

2. Wanawake wanajipa umuhimu sana, wanaona hawastahili kuteseka na hivyo hawataki kuvumilia shida.

Aisee waombe msamaha sasa hivi kabla hawajakasirika😆
Njaa ni mbaya sana isikie tu! Kushindia mkate mchezo! Ulishawahi kunywa uji na nyanya chungu wewe?
 
Back
Top Bottom