Wimbi la ‘single mothers’, wa kulaumiwa zaidi ni Wazazi na Serikali

Wimbi la ‘single mothers’, wa kulaumiwa zaidi ni Wazazi na Serikali

binti anafika chuo, mahitaji yanakuwa mengi, wazazi hawajali tena, saa nyingine hawana cha kucontribute, binti anakomaa inafika muda anazidiwa sasa hapo ni either ajiunge na kundi la wadangaji na kuchoropoa mimba, au kwa ushamba wake apate ki-bf cha kawaida wadate kwa kuahidiana ndoa, hapa mara nyingi wanaishia kuishi pamoja kupunguza cost of living,hapo ndipo binti atabeba mimba kwa kuendekeza mapenzi chuoni au baada ya masomo! Akiamini kumfanyia hivyo bwana mdogo ndio kutazidisha mapenzi! Ndio matokeo yake anakuja kubumburuka sio hivyo adhahaniavyo!

Sawa, mimi naona bado tupo pale pale kwa binti kudanganywa. Wazazi hapo mnawaingiza tuu kwa mlango wa nyuma. Ila hat hivyo naheshimu mawazo yenu. 😊
 
Siku za hivi karibuni single mothers wamekuwa wakilaumiwa, kukejiliwa na kurushiwa maneno mengi ila ukweli ni kwamba wao ni matokeo tu na sio sahihi kuwananga wao badala ya kuangalia chanzo.

Ukweli ni kwamba chanzo kikubwa cha single mothers ni wazazi kushindwa kuwahudumia watoto wao wa kike na kuwasababisha kuwa tegemezi hata kwa vitu vidogo kama pedi na mafuta kutoka kwa vijana waganga njaa na wanaume watu wazima wenye pesa.

Jambo lingine ni hali ngumu ya kiuchumi isiyosapoti maisha ya familia inayowakabili vijana wengi na hapa serikali inawajibika moja kwa moja, vijana wengi hawana pesa za kulea familia kwa hiyo wanabaki kuhonga vipesa vidogo vidogo kufanya ngono na kuzalisha kiholela tu.

Yasiporekebishika haya mawili kelele za mabinti wanaozaa na kubaki single mothers zitaendelea kupigwa daima.
Mawazo mafupi
 
Unawatukana wanawake, unasema kwamba;

1. Wanawake ni wajinga mno mpaka wanajirahisisha kubeba mimba ili kuepuka njaa.

2. Wanawake wanajipa umuhimu sana, wanaona hawastahili kuteseka na hivyo hawataki kuvumilia shida.

Aisee waombe msamaha sasa hivi kabla hawajakasirika😆
Afute uzi kabla kikundi fulani chenye Hasira kali hakijawasha Data.
 
Kila mtu na mtazamo wake, mimi ndio nilichoshuhudia siandiki kufurahisha umma..
Unaweza ukawa upo sahihi ila tabia hiyo inakua influenced na malezi mabovu,

Ni sawa na kwenye issue ya wizi,kijana aliyelelewa kwenye maadili mazuri,hawezi kuiba hata kama atakua na shida,kuiba kwa kisingizio cha kua na shida sio sababu ya msingi,wizi ni tabia,unaweza ukawa na milioni ila ukaja kuiba buku.
 
Hebu ngoja kwanza, malezi mabovu ndio yakoje hayo? Kumbe kuna wazazi wanafundisha watoto wizi au kuzaa zaa tu?
 
Sasa kijina ana soma na binti anasoma , hakuna mwenye uwezo wa kiuchumi kwa nini mpeane mimba ? Au inaingia bahati mbaya?
Ni vicious cycle ya umasikini.
Utafiti duniani unaonyesha watoto wanaotoka kwenye familia zenye uwezo mzuri kiuchumi wanakuwa na elimu kubwa, nzuri, maarifa na taarifa sahihi za mambo ya sex na afya ya uzazi kwa ujumla kushinda wanaotoka familia masikini. Ukichanganya na uwezo wao kiuchumi ndio unakuta ni nadra kupata mimba za utotoni au kuwa single mothers.
 
Hebu ngoja kwanza, malezi mabovu ndio yakoje hayo? Kumbe kuna wazazi wanafundisha watoto wizi au kuzaa zaa tu?
Mara nyingi mtoto hua ana copy lifestyle au malezi aliyo lelewa,mtoto anakua anamuona Mama yake anakua na tabia za ajabu ajabu tu,kuchepuka na mengineyo,

Mtoto anaenda kucheza na wenzake na anarudi home ameiba michezo ya wenzake,wala humkemei,anakua na kuona kua kumbe kuchukua/kuiba kitu ambacho sio chako ni jambo la kawaida tu,hapo ndipo mazowea yanapojenga tabia .
 
Ooh hapo nimekuelewa duhh! Factors ni nyingi sana, hakuna sababu ya kuzipinga maana tunatoka katika jamii tofauti tofauti!
 
Unawatukana wanawake, unasema kwamba;

1. Wanawake ni wajinga mno mpaka wanajirahisisha kubeba mimba ili kuepuka njaa.

2. Wanawake wanajipa umuhimu sana, wanaona hawastahili kuteseka na hivyo hawataki kuvumilia shida.

Aisee waombe msamaha sasa hivi kabla hawajakasirika😆
1. Hawajirahisishi kubeba mimba, wengi wa single mothers wanaobeba mimba hata hawakupanga bali ni kama ni nilivyoeleza hapo kuhusu hali za uchumi za familia pamoja na mazingira ya ushwawishi, pia elimu ya afya ya uzazi iko chini sana kwa mabinti wengi.

2. Wanawake hawajipi umuhimu bali mahitaji yao ni tofauti sana na wanaume. Mwanaume atanyoa kwa elfu tatu wakati mwanamke atasuka nywele kwa elfu thelathini, mwanaume utakuta hata mafuta hapaki ila mwanamke anahitaji mafuta kama ya aina tatu, hapo bado kuna pedi kila mwezi n.k
 
Back
Top Bottom