Wimbi la walimu kuhama CWT Tanzania limeshika kasi

Wimbi la walimu kuhama CWT Tanzania limeshika kasi

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
JPM alikuwa nabii

Katika moja ya hotuba zake, Rais Magufuli alizungumzia michango ya 2% ambayo walimu hukatwa kwenye mishahara yao ili kuchangia Chama Cha Waalimu (CWT). Magufuli alisema michango hiyo hukipa CWT zaidi ya bilioni 3 kila mwezi, na walimu wamekuwa hawajiulizi ni kwa namna gani fedha hizo zimekuwa zikitumika.

Katika hotuba hiyo Magufuli alitoa wito kwa waalimu kulalamikia kuhusu matumizi ya michango yao kama ambavyo wamekuwa wakifanya katika kuidai serikali. Pia amezungumzia benki ya walimu ambayo amesema kwa sasa haifanyi vizuri na pia imekuwa ikinufaisha wafanya biashara badala ya walimu.
 
CWT ni 🚮. Hivyo walimu wahame tu. Maana tulipiga sana kelele humu lakini hawakusikia. Hivyo kama mdau wa elimu, naunga mkono walimu kukihama hiki chama ambacho kwa miaka nenda kimekuwa kikiwaibia walimu hela zao, huku kikilindwa na serikali ya ccm.

Kitendo cha kuwakata wanachama wao ada ya kila mwezi kwenye mishahara yao kwa kiasi cha 2% ni cha hovyo kupitiliza! Na pia ni kitendo cha wizi.

Maana siamini kama kuna chama hapa duniani kinachowakata wananchama wake ada kila mwezi kwa aina hii wanayofanya CWT kwa walimu.

Kama wangekuwa siyo wezi, walitakiwa kuwakata walimu ada ambayo ni sawa, badala ya kuwakata kwa %, na hivyo kutengeneza tofauti kubwa ya makato kati ya mwalimu aliyeanza kazi mapema dhidi ya yule mpya. Mfano kila mwalimu angekatwa elfu 5 tu kila mwezi. By the way, hiyo CWT sidhani kama ina faida yoyote ile kwa walimu. Na kama ipo, basi nijulishwe hapa jukwaani.
 
Fomu hii hapa
Screenshot 2023-05-14 at 13-58-47 TUF15.pdf.png
 

Attachments

CWT walijinunulia magari na kujenga majimbo ya kifahari sasa wamelala kuti kavu
C1F5FD8A-2D35-4747-84C0-3BB1FF3654B0.jpeg
 
Wahamie chap huko chakuwahata kisha watabadili katiba makato yatakuwa 20k badala ya hiyo 5k!
But hivi hata hao chakuwahata wanafaida gani??
 
Kwahali ilivyo Sasa hata baba wa Taifa The late J.k. Nyerere 😔🇹🇿🇹🇿 asinge weza kua proud na UALIMU wake kwenye zama hizi.............
Jamaan
Sasa wanakotoka na wanakoenda si ni kitu kile kile!
Walimu bhana... Sijui wakoje
 
Sasa wanakotoka na wanakoenda si ni kitu kile kile!
Walimu bhana... Sijui wakoje
Ni tofauti mkuu.

Kwa sasa kama basic salary ya mwalimu ni 2,400,000 kila mwezi anakatwa 2,400,000*2/100 = 48,000 Tsh anakatwa Kila mwezi mara Miezi 12.= 576,000

ambapo kwa chama kipya mwalimu huyo Huyo atakatwa 5,000 kwa mwezi na kwa mwaka atakatwa 60,000.

576,000 ~ 60,000 = 516,000 mwalimu atasave kwa mwaka.

CWT ni wezi
 
Ni tofauti mkuu.

Kwa sasa kama basic salary ya mwalimu ni 2,400,000 kila mwezi anakatwa 2,400,000*2/100 = 48,000 Tsh anakatwa Kila mwezi mara Miezi 12.= 576,000

ambapo kwa chama kipya mwalimu huyo Huyo atakatwa 5,000 kwa mwezi na kwa mwaka atakatwa 60,000.

576,000 ~ 60,000 = 516,000 mwalimu atasave kwa mwaka.

CWT ni wezi
Kumbe hoja ni wizi wa CWT... Mbona hata hao wengine wameanza na dalili mbaya sana 5,000! Si Kila mwaka itapanda!
Haya tuje kwenye maswali ya msingi:
Hicho Chama kipya mna uhakika kitasimamia masuala nyeti ya walimu kama nyongeza ya mishahara, posho, mafunzo kazini, n.k?

Au mkikatwa 60,000 kwa mwaka tayari mmemaliza??
 
Back
Top Bottom