Wimbi la walimu kuhama CWT Tanzania limeshika kasi

Wimbi la walimu kuhama CWT Tanzania limeshika kasi

1683973317522.png
 
CWT ni 🚮. Hivyo walimu wahame tu. Maana tulipiga sana kelele humu lakini hawakusikia. Hivyo kama mdau wa elimu, naunga mkono walimu kukihama hiki chama ambacho kwa miaka nenda kimekuwa kikiwaibia walimu hela zao, huku kikilindwa na serikali ya ccm.

Kitendo cha kuwakata wanachama wao ada ya kila mwezi kwenye mishahara yao kwa kiasi cha 2% ni cha hovyo kupitiliza! Na pia ni kitendo cha wizi.

Maana siamini kama kuna chama hapa duniani kinachowakata wananchama wake ada kila mwezi kwa aina hii wanayofanya CWT kwa walimu.

Kama wangekuwa siyo wezi, walitakiwa kuwakata walimu ada ambayo ni sawa, badala ya kuwakata kwa %, na hivyo kutengeneza tofauti kubwa ya makato kati ya mwalimu aliyeanza kazi mapema dhidi ya yule mpya. Mfano kila mwalimu angekatwa elfu 5 tu kila mwezi. By the way, hiyo CWT sidhani kama ina faida yoyote ile kwa walimu. Na kama ipo, basi nijulishwe hapa jukwaani.
Hakina faida. LAKINI hata vingine vinavyoanzishwa Bado Nia ni kupiga Hela. Tena vimeanzishwa na wale waliokosa fursa za ulaji cwt. Kwa maoni yangu kusiwe na vyama vya walimu maana havitasaidia chochote.
 
Exactly
 
Ww ulipenda waende wapi mkuu hapa jamii forum ndio kisima cha Elimu funguka ulipenda walimu waende wapi?
Mwalimu; ilipaswa kila mtu abaki na hela wasome upepo. Ikibidi kugoma wajitokeze wagome
 
Mwalimu; ilipaswa kila mtu abaki na hela wasome upepo. Ikibidi kugoma wajitokeze wagome
Walimu wanasema hv wao waliunganishwa na hk kinaitwa cwt bila ridhaa yao yaan walidakwa juu kwa juu na kuanza kukatwa ada ya uanachama na ninaamini ni kinyume cha SHERIA.Na unaambiwa pamoja na kuwa chama kipya kinakata Tshs 5000/= tu kila mwezi tofauti na cwt bado walimu wengi wanakipenda chama cha cwt zaidi na sababu za msingi hawana.
 
Walidakwa juu kwa juu?
 
Ni tofauti mkuu.

Kwa sasa kama basic salary ya mwalimu ni 2,400,000 kila mwezi anakatwa 2,400,000*2/100 = 48,000 Tsh anakatwa Kila mwezi mara Miezi 12.= 576,000

ambapo kwa chama kipya mwalimu huyo Huyo atakatwa 5,000 kwa mwezi na kwa mwaka atakatwa 60,000.

576,000 ~ 60,000 = 516,000 mwalimu atasave kwa mwaka.

CWT ni wezi
Huwez kusema wez Kwa kuangalia Makato Maana yapo kisheria kulingana na mkataba baina ya cwt na walimu
 
Kumbe hoja ni wizi wa CWT... Mbona hata hao wengine wameanza na dalili mbaya sana 5,000! Si Kila mwaka itapanda!
Haya tuje kwenye maswali ya msingi:
Hicho Chama kipya mna uhakika kitasimamia masuala nyeti ya walimu kama nyongeza ya mishahara, posho, mafunzo kazini, n.k?

Au mkikatwa 60,000 kwa mwaka tayari mmemaliza??
Kinatambulika kisheria na wanasikilizwa
 
Hakina faida. LAKINI hata vingine vinavyoanzishwa Bado Nia ni kupiga Hela. Tena vimeanzishwa na wale waliokosa fursa za ulaji cwt. Kwa maoni yangu kusiwe na vyama vya walimu maana havitasaidia chochote.
Vyama vya wafanyakazi ni lazima viwepo. Changamoto iliyopo katika nchi yetu, ni hiki chama cha mapinduzi ccm kujimilikisha kila kitu.

Yaani kila eneo kinapenyeza mamluki wake, na ambao mwisho wa siku huishia kulinda maslahi ya serikali ya ccm, badala ya maslahi ya chama husika cha wafanyakazi.

Thats kutoka moyoni siipendi ccm.
 
Back
Top Bottom