Wimbi la walimu kuhama CWT Tanzania limeshika kasi

Wimbi la walimu kuhama CWT Tanzania limeshika kasi

Huwez kusema wez Kwa kuangalia Makato Maana yapo kisheria kulingana na mkataba baina ya cwt na walimu
Hakuna mkataba wowote ambao walimu waliingia na hao Cwt .Walimu wamekuwa wakiingizwa kinyemela kwenye Cwt kwa kuwatumia maafisa utumishi pasipo Mwl husika kujaza fomu ya kisheria iitwayo Tuf 15.Hao makatibu wa Cwt wajiandae kuja kuongezea ikama mashuleni .Idiots
 
Dah! aiseee hivi ndo kweli mti unaopigwa mawe mengi ndo mti wenye matunda ama?

Kila Kona dhihaka Kwa mwalimu nadhani ata akiwa darasani wanafunzi watamuona wakawaida tu maana wanafunzi nao wanapita mitandaoni na kuyaona haya.

Kwa namna hii mwalimu atshindwa kutoa matunda yake Kwa wanafunzi maana atakuwa na mengi ya msongayo

Dah! Majoblees nao wataanza kusema HERI wao kuliko walimu
MUDA UTASEMA NASI #2040....
 
Kumbe hoja ni wizi wa CWT... Mbona hata hao wengine wameanza na dalili mbaya sana 5,000! Si Kila mwaka itapanda!
Haya tuje kwenye maswali ya msingi:
Hicho Chama kipya mna uhakika kitasimamia masuala nyeti ya walimu kama nyongeza ya mishahara, posho, mafunzo kazini, n.k?

Au mkikatwa 60,000 kwa mwaka tayari mmemaliza??
Hata hivyo cwt hawajawahi kufanya haya pamoja na hela zote wanazochukua..labda kama wamefanya kwa wengine
 
Hivi ukiamua hutaki vyote ukabaki free inawezekana??
 
Hao cwt wanaushirika wakaribu wakimaslahi na waajiri. Ifike wakati waajiri waulizwe. Mtu ambayehakua na mkataba na cwt mlimkataje fedha zake. Cwt wanakauli flani hivi ya kijizi, eti tunakata ada ya uwakala. Uwakala wa nini,kwa sheria ipi? Miongoni mwa wanyonyaji na wapunguza ufanisi wa kazi ni cwt. Hata hao wanaojitoa michango yao huishia kwa nani? Kwanini wasirufishiwe f dha zao.
 
Huwez kusema wez Kwa kuangalia Makato Maana yapo kisheria kulingana na mkataba baina ya cwt na walimu
Hakuna mkataba wa kisheria kati ya cwt na walimu. Kinachotokea mwalimu akiajiriwa cwt inamkata pesa kwenye mshahara wake bila ya ridhaa yake. Yaani wanatumia mabavu kuwaibia walimu fedha zao. Walimu hawapewi fomu ya kujiunga na chama hiko kwa ridhaa yao wenyewe
 
Hakuna mkataba wa kisheria kati ya cwt na walimu. Kinachotokea mwalimu akiajiriwa cwt inamkata pesa kwenye mshahara wake bila ya ridhaa yake. Yaani wanatumia mabavu kuwaibia walimu fedha zao. Walimu hawapewi fomu ya kujiunga na chama hiko kwa ridhaa yao wenyewe
 
Walimu inajulikana walio wengi mishahara yao ni ya kawaida kabisa, nimewahi kukutana na mwl analipwa Tsh 429,990 kama basic salary hii ni pesa ya kawaida mno

Huyu anachangia kila mwezi mwaka mzima anachoambulia ni T-shirt na kofia kwenye sherehe za May mosi, CWT wao wamejikita kwenye majanga tu,, eti mwl akipata kesi tunamlipia wakili wa kusimamia kesi

Haya mwl huyu asipopata kesi mpaka kistaafu anafaidikaje na michango yake?,, Walimu hawa wanakopa kwenye mabenki kwa riba kubwa sana niliwahi kushuhudia mwl kakopa mil 7 marejesho ni mil 14 yaani riba ya 100% eti kisa mkopo ni wa mda mrefu miaka 5

Kwann CWT wasiizungushe hiyo michango ya wanachama wao kukopeshana kwa riba nafuu? Matokeo yake mwl akisha kuwa katibu ama rais wa chama anapata utajiri wa kupindukia kisha anabaki kusubiri teuzi ya uDC ama uDED kutoka kwenye mamlaka mfano kina Kassim Majaliwa, Dotto Biteko nk
 
Ki ukweli kabisa ukila na kipofu usimshike mkono. Nimeona takwimu hapo juu inasema kwa mwezi wanakusanya kiasi cha 3 B. Basi bora wangesema walimu wanapata haki ya kukopesheka kwenye benki ya walimu pasipo kutoa riba.Ili iwapunguzie ukali wa maisha. Lkn hakuna return yoyote wanayopata. Daaah hii nchi ngumu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JPM alikuwa nabii
View attachment 2619915
Katika moja ya hotuba zake, Rais Magufuli alizungumzia michango ya 2% ambayo walimu hukatwa kwenye mishahara yao ili kuchangia Chama Cha Waalimu (CWT). Magufuli alisema michango hiyo hukipa CWT zaidi ya bilioni 3 kila mwezi, na walimu wamekuwa hawajiulizi ni kwa namna gani fedha hizo zimekuwa zikitumika.

Katika hotuba hiyo Magufuli alitoa wito kwa waalimu kulalamikia kuhusu matumizi ya michango yao kama ambavyo wamekuwa wakifanya katika kuidai serikali. Pia amezungumzia benki ya walimu ambayo amesema kwa sasa haifanyi vizuri na pia imekuwa ikinufaisha wafanya biashara badala ya walimu.
Hujaelezea huo mhamo!
 
Mbona pesa ndefu 3 billions kwa mwezi
Vp inakuwaje mwalimu asipo taka kujiunga na chama chochote Kama Jambo likimkuta ajue mwenyewe
 
Ni tofauti mkuu.

Kwa sasa kama basic salary ya mwalimu ni 2,400,000 kila mwezi anakatwa 2,400,000*2/100 = 48,000 Tsh anakatwa Kila mwezi mara Miezi 12.= 576,000

ambapo kwa chama kipya mwalimu huyo Huyo atakatwa 5,000 kwa mwezi na kwa mwaka atakatwa 60,000.

576,000 ~ 60,000 = 516,000 mwalimu atasave kwa mwaka.

CWT ni wezi
Sio wezi ni wahuni na majambazi.... Ni pirates !!!
 
Kumbe hoja ni wizi wa CWT... Mbona hata hao wengine wameanza na dalili mbaya sana 5,000! Si Kila mwaka itapanda!
Haya tuje kwenye maswali ya msingi:
Hicho Chama kipya mna uhakika kitasimamia masuala nyeti ya walimu kama nyongeza ya mishahara, posho, mafunzo kazini, n.k?

Au mkikatwa 60,000 kwa mwaka tayari mmemaliza??
Lini CWT iliwahi kuyasimamia ????
 
Back
Top Bottom