JPM alikuwa nabii
View attachment 2619915
Katika moja ya hotuba zake, Rais Magufuli alizungumzia michango ya 2% ambayo walimu hukatwa kwenye mishahara yao ili kuchangia Chama Cha Waalimu (CWT). Magufuli alisema michango hiyo hukipa CWT zaidi ya bilioni 3 kila mwezi, na walimu wamekuwa hawajiulizi ni kwa namna gani fedha hizo zimekuwa zikitumika.
Katika hotuba hiyo Magufuli alitoa wito kwa waalimu kulalamikia kuhusu matumizi ya michango yao kama ambavyo wamekuwa wakifanya katika kuidai serikali. Pia amezungumzia benki ya walimu ambayo amesema kwa sasa haifanyi vizuri na pia imekuwa ikinufaisha wafanya biashara badala ya walimu