Wimbo huu ulisababisha gumzo 'Tata' kuhusu Imani za Dini ya Kikristu na Kiislamu

Wimbo huu ulisababisha gumzo 'Tata' kuhusu Imani za Dini ya Kikristu na Kiislamu

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Kuna wakati Rais Mobutu Seseseko alianzisha sera ya "African Authentication" iliyokuwa na lengo la Afrika kujitambua.

Kama mfano aliamua kubadili jina la nchi hiyo kutoka Belgium Congo na kuiita Zaire.

Hata yeye alibadili jina lake la ubatizo la Joseph Desire na kujiita Mobutu Seseseko Kuku Ngbandu wa Nzabanga.

Pia akaamuru makanisa yote na Misikiti kuwabatiza watoto kwa majina ya kiafrika na sio yale ya kuzungu kama Peter na Joseph au Abdallah au Hassan.

Swala hili lilimletea msuguano mkubwa na Kanisa Katoliki nchini mwake, hali iliyosababisha atoe tena amri ya kuzifunga seminari zote za kanisa hilo na madrasa.

Katika sakata hilo, aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Kinshasha, Kardinali Joseph Albert Malula akapewa ultimatum awe ameondoka Kongo ndani ya masaa 48.

Askofu huyo akaenda uhamishoni Roma, Italia.

Nyuma yake ukatungwa wimbo mmoja maarufu sana na bwana Verky Kiamungana ulioitwa "NAKOMITUNAKA" yaani *"HUWA NIKIJIULIZA"*Ambao ulichochea uhasama mkubwa zaidi baina ya kanisa Katoliki na Serikali ya Mobutu Sese Seko Nkuku Ngbandu wa Nzabanga.



Nini kilikuwa ndani ya wimbo huu? yaangalie na kuyasoma mashairi yake na maana yake hapa chini👇

Aaeeh nakomitunaka
𝙃𝙪𝙖 𝙣𝙞𝙠𝙞𝙟𝙞𝙪𝙡𝙞𝙯a

Nzambe nakomitunaka ooh
𝙈𝙪𝙣𝙜𝙪 𝙢𝙞𝙢𝙞 𝙝𝙪𝙬𝙖 𝙣𝙞𝙠𝙞𝙟𝙞𝙪𝙡𝙞𝙯𝙖

Mposo mwindo ewuta nde wapi ooh
𝙉𝙜𝙤𝙯𝙞 𝙣𝙮𝙚𝙪𝙨𝙞 𝙖𝙨𝙞𝙡𝙞 𝙮𝙖𝙠𝙚 𝙬𝙖𝙥𝙞?

Nkoko na biso ya kala ye nde nani eeh,
𝘽𝙖𝙗𝙪 𝙮𝙚𝙩𝙪 𝙬𝙖 𝙠𝙬𝙖𝙣𝙯𝙖 {𝙬𝙖 𝙯𝙖𝙢𝙖𝙣𝙞} 𝙣𝙞 𝙣𝙖𝙣𝙞?

Yesu mwana nzambe ye nde mundele.
𝙔𝙚𝙨𝙪 𝙢𝙬𝙖𝙣𝙖 𝙬𝙖 𝙈𝙪𝙣𝙜𝙪 𝙣𝙞 𝙢𝙬𝙚𝙪𝙥𝙚

Adamu na Eva bango nde mindele
Basantu nionso bango nde mindele
Mpo na nini oh..
𝘼𝙙𝙖𝙢𝙪 𝙣𝙖 𝙀𝙫𝙖 𝙣𝙖𝙤 𝙣𝙞 𝙬𝙚𝙪𝙥𝙚
𝙒𝙖𝙩𝙖𝙠𝙖𝙩𝙞𝙛𝙪 𝙬𝙤𝙩𝙚 𝙣𝙖𝙤 𝙣𝙞 𝙬𝙚𝙪𝙥𝙚
𝙃𝙞𝙫𝙞 𝙣𝙞 𝙠𝙬𝙖𝙣𝙞𝙣𝙞?

Ba buku ya nzambe tomonaka boye
𝙆𝙬𝙚𝙣𝙮𝙚 𝙫𝙞𝙩𝙖𝙗𝙪 𝙫𝙮𝙖 𝙈𝙪𝙣𝙜𝙪 𝙝𝙪𝙬𝙖 𝙩𝙪𝙣𝙖𝙤𝙣𝙖 {𝙞𝙢𝙚𝙖𝙣𝙙𝙞𝙠𝙬𝙖 𝙝𝙞𝙫𝙮𝙤}

Basantu nionso photo c'est mindele..
𝙒𝙖𝙩𝙖𝙠𝙖𝙩𝙞𝙛𝙪 𝙬𝙤𝙩𝙚 𝙥𝙞𝙘𝙝𝙖𝙣𝙞 𝙬𝙖𝙣𝙖𝙤𝙣𝙚𝙠𝙖𝙣𝙖 𝙬𝙖𝙠𝙞𝙬𝙖 𝙬𝙚𝙪𝙥𝙚

Ba angelou nionso bango c'est mindele..
𝙈𝙖𝙡𝙖𝙞𝙠𝙖 𝙬𝙤𝙩𝙚 𝙥𝙞𝙘𝙝𝙖𝙣𝙞 𝙝𝙪𝙤𝙣𝙚𝙠𝙖𝙣𝙖 𝙬𝙖𝙠𝙞𝙬𝙖 𝙬𝙚𝙪𝙥𝙚

Soki zabulu photo mutu mwindo
𝙄𝙠𝙞𝙬𝙖 𝙣𝙞 𝙨𝙝𝙚𝙩𝙖𝙣𝙞/𝙥𝙚𝙥𝙤 𝙗𝙖𝙨𝙞 𝙥𝙞𝙘𝙝𝙖 𝙝𝙪𝙤𝙣𝙚𝙠𝙖𝙣𝙖 𝙮𝙖 𝙢𝙩𝙪 𝙢𝙬𝙚𝙪𝙨𝙞

Injustice ewuta nde wapi ooh.. ah Mamma
𝙐𝙙𝙝𝙖𝙡𝙞𝙢𝙪/𝙙𝙝𝙪𝙡𝙢𝙖 𝙝𝙞𝙞 𝙖𝙨𝙞𝙡𝙞 𝙮𝙖𝙠𝙚 𝙬𝙖𝙥𝙞 𝙖𝙝

Bango mpo bakanga biso mayele ooh
𝙆𝙬𝙖 𝙢𝙖𝙖𝙣𝙖 𝙝𝙞𝙮𝙤 𝙬𝙖𝙤 {𝙬𝙖𝙯𝙪𝙣𝙜𝙪} 𝙣𝙙𝙞𝙮𝙤 𝙬𝙖𝙡𝙞𝙤𝙩𝙪𝙛𝙞𝙘𝙝𝙖 𝙢𝙖𝙖𝙧𝙞𝙛𝙖 𝙝𝙖𝙮𝙖

Bikeko ya bankoko bango baboyaka
𝙈𝙖𝙨𝙖𝙣𝙖𝙢𝙪 𝙮𝙖 𝙢𝙖𝙗𝙖𝙗𝙪 𝙯𝙚𝙩𝙪 𝙬𝙖𝙤 {𝙬𝙖𝙯𝙪𝙣𝙜𝙪} 𝙬𝙖𝙣𝙖𝙮𝙖𝙠𝙖𝙩𝙖𝙖

N'kisi ya bankoko bango bandimaka te
𝙏𝙞𝙗𝙖 {𝙖𝙨𝙞𝙡𝙞} 𝙯𝙖 𝙢𝙖𝙗𝙖𝙗𝙪 𝙯𝙚𝙩𝙪 𝙬𝙖𝙤 {𝙬𝙖𝙯𝙪𝙣𝙜𝙪} 𝙝𝙖𝙬𝙖𝙯𝙞𝙖𝙢𝙞𝙣𝙞

Kasi na ndako ya nzambe biso tomonaka
𝙄𝙡𝙖 𝙠𝙬𝙚𝙣𝙮𝙚 𝙣𝙮𝙪𝙢𝙗𝙖 𝙯𝙖 𝙞𝙗𝙖𝙙𝙖 𝙝𝙪𝙬𝙖 𝙩𝙪𝙠𝙞𝙤𝙣𝙖 𝙝𝙞𝙫𝙮𝙤

Tokosambela chapele na maboko
𝙃𝙪𝙬𝙖 𝙩𝙪𝙣𝙖𝙨𝙖𝙡𝙞 𝙝𝙪𝙠𝙪 𝙧𝙤𝙯𝙖𝙡𝙞 𝙯𝙞𝙠𝙞𝙬𝙖 𝙢𝙞𝙠𝙤𝙣𝙤𝙣𝙞

Tokosambela bikeko bitondi ndako
𝙃𝙪𝙬𝙖 𝙩𝙪𝙠𝙞𝙨𝙖𝙡𝙞 𝙝𝙪𝙠𝙪 𝙢𝙖𝙨𝙖𝙣𝙖𝙢𝙪 𝙮𝙖𝙠𝙞𝙬𝙖 𝙮𝙖𝙢𝙚𝙟𝙖𝙖 𝙣𝙙𝙖𝙣𝙞 𝙮𝙖 𝙣𝙮𝙪𝙢𝙗𝙖 𝙮𝙖 𝙞𝙗𝙖𝙙𝙖

Kasi bikeko yango c'est mindeleee
Mpo na nini Nzambe?
𝙄𝙡𝙖 𝙢𝙖𝙨𝙖𝙣𝙖𝙢𝙪 𝙝𝙖𝙮𝙤 𝙣𝙞 𝙢𝙚𝙪𝙥𝙚 {𝙮𝙖 𝙠𝙞𝙯𝙪𝙣𝙜𝙪}
𝙃𝙞𝙫𝙞 𝙣𝙞 𝙠𝙬𝙖 𝙣𝙞𝙣𝙞 𝙈𝙪𝙣𝙜𝙪?

Ba prophete mindele biso tondimaka
𝙈𝙖𝙣𝙞𝙗𝙞𝙞 𝙬𝙚𝙪𝙥𝙚 𝙨𝙞𝙨𝙞 𝙝𝙪𝙬𝙖 𝙩𝙪𝙣𝙖𝙬𝙖𝙖𝙢𝙞𝙣𝙞

Kasi ya bato muindo bango bandimaka te
𝙄𝙡𝙖 {𝙢𝙖𝙣𝙖𝙗𝙞𝙞} 𝙬𝙖 𝙬𝙖𝙩𝙪 𝙬𝙚𝙪𝙨𝙞 𝙬𝙖𝙤 {𝙬𝙖𝙯𝙪𝙣𝙜𝙪} 𝙝𝙪𝙬𝙖 𝙝𝙖𝙬𝙖𝙬𝙖𝙖𝙢𝙞𝙣𝙞

Mpo na nini nzambe osala biso boye
𝙆𝙬𝙖 𝙣𝙞𝙣𝙞 𝙈𝙪𝙣𝙜𝙪 𝙪𝙢𝙚𝙩𝙪𝙛𝙖𝙣𝙮𝙞𝙖 𝙝𝙞𝙫𝙞?

Africa miso efungwani..
𝘼𝙛𝙧𝙞𝙠𝙖 𝙩𝙪𝙢𝙚𝙖𝙢𝙠𝙖

Africa tozonga sima te
Ah mamaaah
𝘼𝙛𝙧𝙞𝙠𝙖 𝙩𝙪𝙨𝙞𝙧𝙪𝙙𝙞 𝙣𝙮𝙪𝙢𝙖 {𝙩𝙪𝙨𝙤𝙣𝙜𝙚 𝙢𝙗𝙚𝙡𝙚}
𝘼𝙝 𝙢𝙖𝙢𝙖𝙖𝙝

BAADA YA WIMBO HUU KUTOKA KWENYE ALBAMU ULIZUA MTAFARUKO MKUBWA DHIDI YA HIZI DINI MBILI ZA UKRISTO NA UISLAM MAANA ZILIONEKANA ZOTE NI ZA WATU WEUPE NA TASWIRA ZAKE NYINGI ZILIHUSISHA WATU WEUPE. MIJADALA KWENYE MABAA NA SEHEMU ZENYE MIKUSANYIKO YA WATU IKAWA INAZUNGUMZWA SANA NA IKAWA CHANGAMOTO KUBWA KWA MASHEHE, MAPADRE, WACHUNGAJI MAUSTADHI NK KUFAFANUA MAKANISANI NA MISIKITINI.

KWA KIASI KIKUBWA ILIRUDISHA NYUMA HARAKATI ZA DINI. HIVI SASA HOJA HIZO ZIMESHAFIFIA.

NI MUHIMU KUYAJUA MAUDHUI YA NYIMBO KABLA HUJASIKILIZA.
 
Safi sana, nami nataman tuwatimue hawa Matapeli na dini zao za Kisanii aidha tubaki wapagani au turud kwenye dini zetu za asili.
 
Kwenye tafsiri naona vibox tu,,,,ila nimependa vokali ni tamu sana
 
Na kufuata mkumbo sio kuzuri aminini unachoamini ata kama utaabudu mjusi ndio mungu wko huyo
Hapo sawa umenena, ila tusiaminishane kwamba dini za Wazungu na warabu ndizo sahih pekee. Ni sahih kwao wenye nazo.
 
Mwimbaji yuko sahihi 1000% hata viongozi wa dini ukiwauliza asili ya dizi zao watasema exactly kuwa UKRISTU uliletwa na WAZUNGU Missionaries (Whites Traders) na UISLAMU uliletwa na WAARABU (Arabic Trader).

Kwa wale wabishi kasome kitabu cha zamani kitwacho "African Societies from 1880's" "Jamii za Kiafrika toka miaka ya 1880"
 
Hata Mtume Muhamad alitumia mfano wa mtumwa wake mweusi kuwaonyesha watu rangi ya shetani.

Afrika hizi dini tuzifate kwa tahadhari, Nae Papa Francis kiongozi wa kanisa la waroma haoni taabu kubariki mapenzi ya jinsia moja
 
Uzuri dini taratibu zinapoteza ushawaishi,wamebaki wajinga wachache
 
Back
Top Bottom