Kuna wakati Rais Mobutu Seseseko alianzisha sera ya "African Authentication" iliyokuwa na lengo la Afrika kujitambua.
Kama mfano aliamua kubadili jina la nchi hiyo kutoka Belgium Congo na kuiita Zaire.
Hata yeye alibadili jina lake la ubatizo la Joseph Desire na kujiita Mobutu Seseseko Kuku Ngbandu wa Nzabanga.
Pia akaamuru makanisa yote na Misikiti kuwabatiza watoto kwa majina ya kiafrika na sio yale ya kuzungu kama Peter na Joseph au Abdallah au Hassan.
Swala hili lilimletea msuguano mkubwa na Kanisa Katoliki nchini mwake, hali iliyosababisha atoe tena amri ya kuzifunga seminari zote za kanisa hilo na madrasa.
Katika sakata hilo, aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Kinshasha, Kardinali Joseph Albert Malula akapewa ultimatum awe ameondoka Kongo ndani ya masaa 48.
Askofu huyo akaenda uhamishoni Roma, Italia.
Nyuma yake ukatungwa wimbo mmoja maarufu sana na bwana Verky Kiamungana ulioitwa "NAKOMITUNAKA" yaani *"HUWA NIKIJIULIZA"*Ambao ulichochea uhasama mkubwa zaidi baina ya kanisa Katoliki na Serikali ya Mobutu Sese Seko Nkuku Ngbandu wa Nzabanga.
Your browser is not able to display this video.
Your browser is not able to display this video.
Nini kilikuwa ndani ya wimbo huu? yaangalie na kuyasoma mashairi yake na maana yake hapa chini👇
Africa tozonga sima te
Ah mamaaah
𝘼𝙛𝙧𝙞𝙠𝙖 𝙩𝙪𝙨𝙞𝙧𝙪𝙙𝙞 𝙣𝙮𝙪𝙢𝙖 {𝙩𝙪𝙨𝙤𝙣𝙜𝙚 𝙢𝙗𝙚𝙡𝙚}
𝘼𝙝 𝙢𝙖𝙢𝙖𝙖𝙝
BAADA YA WIMBO HUU KUTOKA KWENYE ALBAMU ULIZUA MTAFARUKO MKUBWA DHIDI YA HIZI DINI MBILI ZA UKRISTO NA UISLAM MAANA ZILIONEKANA ZOTE NI ZA WATU WEUPE NA TASWIRA ZAKE NYINGI ZILIHUSISHA WATU WEUPE. MIJADALA KWENYE MABAA NA SEHEMU ZENYE MIKUSANYIKO YA WATU IKAWA INAZUNGUMZWA SANA NA IKAWA CHANGAMOTO KUBWA KWA MASHEHE, MAPADRE, WACHUNGAJI MAUSTADHI NK KUFAFANUA MAKANISANI NA MISIKITINI.
KWA KIASI KIKUBWA ILIRUDISHA NYUMA HARAKATI ZA DINI. HIVI SASA HOJA HIZO ZIMESHAFIFIA.
NI MUHIMU KUYAJUA MAUDHUI YA NYIMBO KABLA HUJASIKILIZA.
Mwimbaji yuko sahihi 1000% hata viongozi wa dini ukiwauliza asili ya dizi zao watasema exactly kuwa UKRISTU uliletwa na WAZUNGU Missionaries (Whites Traders) na UISLAMU uliletwa na WAARABU (Arabic Trader).
Kwa wale wabishi kasome kitabu cha zamani kitwacho "African Societies from 1880's" "Jamii za Kiafrika toka miaka ya 1880"