Wimbo huu una "nguvu" ya ajabu sana!

Wow! Hiyo ni habari njema. Ubarikiwe sana, Mkuu
 
Hayo ni mambo ya Affirmation, ila nyimbo zinatibu hadi maradhi kuna kitabu kimoja kimeelezea mambo ya kujitibu kwa kutumia nyimbo.
 
Nimetega sikio. Sema jambo lako, Mkuu
Ni ajabu sana! Kuona mdada katika Nyakati hizi kuwa na Upendo na Mungu, kwa kiwango hicho?

Naomba kujua Siri ya upendo wako kwa Mungu (what's strengthen your fellowship with the Lord?
 
Ni ajabu sana! Kuona mdada katika Nyakati hizi kuwa na Upendo na Mungu, kwa kiwango hicho?

Naomba kujua Siri ya upendo wako kwa Mungu (what's strengthen your fellowship with the Lord?
Waswahili wanasema: "Tembea, uone!" Bado hujatembea, Mkuu. Kinadada wapo wengi sana nyakati hizi wanaompenda Mungu. Umeomba nikupe siri. Sio siri: Mimi nampenda Mungu kwa sababu Yeye alinipenda kwanza hata akamtoa Mwana wake wa pekee aje kutuokoa(Yn 3:16). Nilikuwa nimefungwa katika vifungo vya dhambi, lakini sasa Yesu ameniweka huru (Am set free!); na Yesu ameniahidi uzima na raha ya milele. Nikimuomba Mungu katika Jina la Yesu, ananipa mahitaji yangu. Nikiumwa ananiponya. Nikilima shamba anabariki mazao yangu. Nikifanya biashara ananipa wateja. Nikimkemea shetani na mapepo yake wanakimbia mbiooo! Nikihubiri, watu wanaokoka. Nikisafiri, ananilinda na kuniepusha na hatari nyingi... Kwanini nisimpende Mungu???
 
Nimeona wengi tu .... Kwenye kusanyiko la PT wengi ni wadada!

Ila wadada wenye ujasiri, ufahamu na Maarifa ya Neno la Mungu ni wachache! Huwa NIKIWAONA kama nakuwa mwenye furaha sana!

Ni kweli nimekupata Mkuu! Kwa hayo anayokufanyia na kukutendea hakika lazima umpende!

Basi nami uniweke kwenye maombi yako! Au ?

Nikupe Ajenda za kuniombea?

I'm too serious
 
Nipe ajenda. Napenda sana kuombea watu. Biblia inasema: "Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii."(Yak 5:16).
Naweza kuja PM ? Ili niletee Ajenda!
 
yah wape ushauri vijana ukikosa hela , ukiachwa ,ukipata changamoto songa mbele huku ukitabasamu.

machozi ya wanaume yanachuruzika moyoni sio machoni
Utakuta mapema ukiwa unajichuruzia machozi mwenyew moyoni mixer BP +sukari jitahidi uteme nyongo mapema achana na masuala ya kizamani ww
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…