Wimbo wa Hainaga ushemeji umenishangaza

Kuna dereva nilimpa teksi afanyie kazi lakini siku nilikuta anapiga mnanda nikamyang'anya kwani nilijua huyu ataishia kupata pesa ya fegi hawezi kufikiria mbali na kujikwamua.
 
kaka kwenye verse ya kwanza wewe umeelewa nini?

Man Fongo natamba,
Mtaalamu wa kuulamba,
Nguo za mitumba,
Nitaendelea kutamba January mpaka December,
Natamba natamba we mwenyewe si unajua,
Na kama nyota haing'ai si unajua,
Wanapakaziana maneno wanaponda,
Maneno maneno hanizushii vidonda,
Napata misaa na dili za uswazi,
Naamini kigodoro hii ndo yangu kazi,
Na binadamu bwana,
Ukikaa nao hawaishi kukusifia,
Ukiwapa kichogo kwa nyuma wanakandia,
Kwani bado hujajua,
Kama unajua na inabidi kuwazoea,
Kama unajua na inabidi kuwazoeaaaa.



Mimi nilivyoelewa jamaa hapo anabrag, kwa nini leo ni zamu yake!
 
Umesikiliza Salome (Diamond ft. Rayvanny) lakini? Huo wa Man Fongo una afadhali kidogo..
Wametumia tafsida , wangetumia maneno yanayoeleweka waziwazi ingekuwa tatizo. Kama ww umefanikiwa kuelewa ni ww, ila wengi sana hawajaelewa wanafurahia midundo. Punguza munkari kijana[emoji3]
 
Uwepo wa shilole(shishi baby) kwenye video umesaidia sana kupromote nyimbo ya hainaga ushemeji
 
Wametumia tafsida , wangetumia maneno yanayoeleweka waziwazi ingekuwa tatizo. Kama ww umefanikiwa kuelewa ni ww, ila wengi sana hawajaelewa wanafurahia midundo. Punguza munkari kijana[emoji3]
Nimeuelewa ndo maana nikasema huu wa Man Fongo una afadhali.. Aliyeelewa kama mimi atajua namaanisha nini [emoji1][emoji1]
 
Duh ndio sound zote hizo?😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…