Wimbo wa Taifa ufupishwe

Wimbo wa Taifa ufupishwe

Wimbo wetu uimbwe full hizo nyingine waachane nazo.

Beti la pili la wimbo wetu unazibariki nchi zote za Africa na watu wake.
 
Basi na melody ibadilike maana inafanana na ya Africa Kusini
 
Afu na wazee tukumbukwe kwenye wimbo, make unaimbwa hivi [emoji445]Dumisha uhuru na umoja, wake kwa waume na watoto[emoji444][emoji445] yaani wazee hatutajwi kabisa.
 
Afu na wazee tukumbukwe kwenye wimbo, make unaimbwa hivi [emoji445]Dumisha uhuru na umoja, wake kwa waume na watoto[emoji444][emoji445] yaani wazee hatutajwi kabisa.

Kwani wazee wana jinsia yao ya kitofauti? Yaani sio wanawake wala wanaume? Mbona vijana hawajatajwa
 
Ni kweli halafu hicho kipande cha Mungu ibariki Afrika, wabariki viongozi wake, kina dosari, tunamwomba Mungu kuwabariki viongozi ambao ni majizi na wauaji kwa nia ya kujitajirisha wao.

Kuna members walishauri wimbo sahihi uwe ule wa Tazama ramani utaona nchi nzuri... ambao kimsingi ni mzuri na maudhui yake ni nzuri
Huo wimbo wa tazama ramani ni bonge la wimbo.
 
Ni kweli halafu hicho kipande cha Mungu ibariki Afrika, wabariki viongozi wake, kina dosari, tunamwomba Mungu kuwabariki viongozi ambao ni majizi na wauaji kwa nia ya kujitajirisha wao.

Kuna members walishauri wimbo sahihi uwe ule wa Tazama ramani utaona nchi nzuri... ambao kimsingi ni mzuri na maudhui yake ni nzuri
Unaposema wabariki viongozi wake ina maana unabariki hata wale wasioipenda Tanzania, madikteta, walioiba kura, wanaong'ang'ania madarakani na wale waliopindua viongozi halali kupata uongozi.

Tufikirie upya kuhusu wimbo huu kama tuna nia ya dhati ya kuujenga uzalendo wa taifa letu. Wimbo huu haujengi uzalendo bali umekaa kijumlajumla sana.
 
Huu wimbo ni mrefu unachosha sana kusimama kuuimba. Ubaki ubeti mmoja tu wa kuiombea Tanzania. Basi. Mtu unasimama mpaka miguu inakaribia kudumbukia tumbonin
 
Na bendera ipunguzwe rangi! Toa rangi ya blue maana tayari bahari inaonekana kwenye ramani!

Unganisha Mwanza, Geita, kagera, shinyanga, simiyu ita KANDA YA ZIWA Dar, lindi,Mtwara, Moro na pwani yenyewe ita MWAMBAO WA PWANI...
😂😂😂
 
Mi nafikiri watoa huo ubeti Wa Afrika ba badala yake kionhezwe kipande kitakachokuwa kinawataja Job na Paramagamba
 
Ni kweli halafu hicho kipande cha Mungu ibariki Afrika, wabariki viongozi wake, kina dosari, tunamwomba Mungu kuwabariki viongozi ambao ni majizi na wauaji kwa nia ya kujitajirisha wao.

Kuna members walishauri wimbo sahihi uwe ule wa Tazama ramani utaona nchi nzuri... ambao kimsingi ni mzuri na maudhui yake ni nzuri
Kwenye majizi mbona hata hapa ni majizi sana!? Tena kuanzia waliopo madarakani na wanaopambania kushika dola. Kwa kifupi hakuna Wa kmsema mwenzake!
 
Wimbo wa kizalendo kabisa ambao hata unapoimba unajisikia kuwa emotional ni ule Wa Tanzania,Tanzania
 
Rangi ya blue iachwe maana imeshaanza kuwa kama ndio nembo ya taifa. Air Tanzania, national team, udart, etc. Tutoe rangi ya kijani na njano maana zinafanana na club moja ya mpira hapa nchini iliyopoteza mwelekeo. Ni aibu kuwa na rangi zao kwenye bendera. Rangi nyeusi pia itolewe haina maana sana, bara zima ni watu weusi tu [emoji23][emoji23]
Rangi nyeusi iraondolewa tu kwa ubaguzi wake wa rangi!
 
Time management, tuokoe muda wa kuimba wimbo mrefu bila sababu.

Afrika (AU) ina wimbo wake, SADC ina wimbo wake na East Africa ina wimbo wake pia hivyo Tanzania hatuna sababu ya kurudia kuimba wimbo wa kuiombea Africa kwenye wimbo wetu.

Kufanya hivi ni kurudia bila sababu kile kinachofanywa na Wimbo wa African Union na kusababisha wimbo wetu kuwa mrefu bila sababu.

Nashauri kile kipande cha Mungu ibariki Afrika tuachane nacho kwenye wimbo wetu wa Taifa ili kibakie kipande cha Mungu ibariki Tanzania ili mambo mengine yabakie kwenye nyimbo za EA, SADC na AU ambazo pia tunahusika nazo.
Ukiwa kidogo umetembea katika nchi za Afrika ( labda tu uwe hujatembea kwa bahati mbaya yako ) utagundua ya kwamba Tanzania kwa 75% imehusika katika Kupigania Uhuru wa nchi nyingi za Afrika.

Hata ukijaribu Kuzisikiliza Hotuba mbalimbali za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere utagundua ya kwamba Mwalimu hakuishia tu Kuipenda Tanzania yake bali alilipenda Bara zima la Afrika na nchi zake husika.

Kuwepo Ubeti wa Kuiongelea Afrika katika Wimbo wetu wa Taifa ni Hitimisho tosha na tukuka kuwa Watanzania siyo Wabinafsi, ni Watu wa Upendo na Ukarimu ndiyo maana hata ukiwakuta Watanzania nje ya nchi bado hubaki Kupendana kiasi kwamba hata Watu wa Mataita mengine yanatuiga na Kutupongeza kwa hilo.

Watanzania tunaheshimika sana huko Kwingineko ( hasa Barani Afrika ) hivyo ni vyema Watu ambao Kusafiri kwenu hasa ( sana sana ) ni kutoka Gairo hadi Nachingwea au Ikupilipa Nkoba na Mbwinde na kama mkisafiri nje ya Tanzania basi ni kwa Msaada tu wa ITV Habari au Tamthilia mkalijua hili.

Yaani kabisa 'Intellectual' wa Kitanzania anaacha Kuzungumzia Vitu vya Msingi ambavyo vina 'consume time' au Kushauri Mambo ya maana yenye Tija ya haraka kwa Maendeleo ya nchi Ubongo wako 'Uliosindikwa' unakutuma uzungumzie Wimbo wa Taifa ambao kwa 'Upopoma' wako uliokutukuka hujui kuwa nao hata Kikatiba tu ni sehemu ya 'Tunu' yako.

Watanzania mkikubali Kuubadilisha huu Wimbo wa Taifa mzuri ambao nahisi hata aliyeutunga hatujamtendea Haki katika Kumlipa na Kumuenzi pia GENTAMYCINE nitawadharau kuliko Maelezo. Usibadilishwe Kitu chochote tafadhali kwani Binafsi hata nikiuimba kwa dakika 30 najawa na 'Morale' Kubwa huku hata 'Uzalendo' wangu kwa Mama Tanzania ukiongezeka maradufu.
 
Mleta mada anauelewa mdogo katika historia ya tz na Afr.

Nionavo mimi na asamehewe
 
Back
Top Bottom