With reference ya hii message kutoka ccm,nadhani ndugu polepole yuko sahihi kuhusu integration ya mifumo ya ccm,nida na inec.

kyanyangwe

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2018
Posts
1,511
Reaction score
4,369
Mimi ni mwanachama halali kabisa wa ccm,niliomba kubadilishiwa kadi yangu iwe katika mfumo mpya.
Mwezi july walinitumia ujumbe kuwa kadi yangu iko tayari,wakaniambia niende na kadi zangu za nida na inec.ingawa bado sijaenda kuichukua ila niliwaza mara mbilimbili hizo kadi zangu wanazitaka za nini?
Nimeambatanisha screenshot chini hapo.
 

Attachments

  • Screenshot_20250824_074441_Messages.jpg
    145.9 KB · Views: 36
Hapo mwishoni kabisa mwa meseji si naona wamekujibu kuwa ni kwa ajili ya uhakiki😁.
 
Hapa sasa ndio napata jibu kama wangekuwa wameunganisha hiyo mifumo wangeomba nida ya nini? Au kadi ya mpiga kura ya nini wakati kwenye hiyo database umo??
 
Inashangaza sana bado watu hamuoni shida kuwa wana-CCM.

Huu ni muendelezo tu wa uovu wa CCM miaka nenda miaka rudi ila bado tu hamuoni kuwa CCM haifai kuungwa mkono.
Mimi ndo maana nawatakia wahuni ushindi wa kishindo ---- watanzania sisi wenyewe ndo tatizo

Hata wale walimu, wakurugenzi, polisi wanaolalamikiwaga kwenye uchaguzi --- hawana kosa ni mfumo jinsi ulivyo


Tatizo la kwanza ninsisi wananchi kws ujumla wetu
 
Mbona kunawatu huwa hawajielewi kiasi hiki. Kwani ukishakuwa mwanachama wa chama si lazima kiwe na taarifa zako. Mi sioni dhambi yoyote. Otherwise hufai kuwa mwanachama na inabidi CCM ikuteme mara moja.

Wewe ni mwanachama na kurayako ni ya CCM kuna ubaya gani wakahakiki kadi yako ya kupiga kura? Au unataka uwe mwanachama afu kura upige kwingine?

Hii fuata mkumbo ni jambo baya sana
 
Hivi wewe ni mzima kichwani kweli?
Wana hakiki nini kwa kutumia vitambulisho vya serikali?
Kwa nini wasingemuambia aende na kitambulisho chake cha ccm cha zamani au number yake ya uanachama?
Mkuu usiwe serious sana na kila kitu utateseka sana.
Ndio maana hapo mwoshoni nimeweka emoj
 
Ingawa kila mtu ana uhuru wa kujiunga na chama chochote cha siasa.ila nyie mnaojiunga ccm recently ndio mtatuchelewesha ktk safari ya mabadiliko.
 
Hapo mwishoni kabisa mwa meseji si naona wamekujibu kuwa ni kwa ajili ya uhakiki😁.
Unataka umhakiki mwanachama wako kwa kupitia uhakiki mwingine? Si angesema passport au driving license au hata kitambulisho cha kazini? Why NIDA? Why kadi ya Mpiga kura?.
 
Hivi wewe ni mzima kichwani kweli?
Wana hakiki nini kwa kutumia vitambulisho vya serikali?
Kwa nini wasingemuambia aende na kitambulisho chake cha ccm cha zamani au number yake ya uanachama?
Nimejiuliza the same question.....kwanini wasiseme hata barua ya utambulisho wa serikali za mtaa kama suala ni uhakiki? Why iwe so specific kwa NIDA na kadi ya Mpiga kura? Yaani unamsajili Mwanachama ambaye humuamini?
 
Unataka kuwa mwanachama kuwa mwanachama.
 
Hapa sasa ndio napata jibu kama wangekuwa wameunganisha hiyo mifumo wangeomba nida ya nini? Au kadi ya mpiga kura ya nini wakati kwenye hiyo database umo??
Nini maana ya uhakiki mkuu umesoma shule au umesomewa?
Ushawahi kwenda interview?

Mbona iko wazi unapotuma maombi unatuma na copy ya vitambulisho vyako ila siku ya kwenda interview unaenda na vyeti og ili wakahakiki kama ni kweli .... huo ndo uhakiki au nikudadavulie tena...
 
Acha kufukua makaburi,we nenda kachukue kadi yako mpya tulia.
 
Mkiambiwa mh lissu ni mwana wa Mungu alie hai mnabisha, lissu alisema kazi hii ya kuikomboa nchi hii inahitaji kila mmoja kushiriki bila kujali upo chama gani na aliwakaribisha wote walio katika vyama vyote kuleta talanta zao , sasa naona talanta za kunyoosha nchi kutoka kwa wadau zimeanza pale ,polepole, Gwajima, Rc , n.k na je nyuma yao wapo wangapi , mtashangaa

Tujiandae kuanza kuongea lugha moja sasa , huu mziki ameanzishwa sio wa kitoto.

Mwaka huu hakuna uchaguzi asema Bwana ole wenu mnaolazimisha
 
Ni
Inashangaza sana bado watu hamuoni shida kuwa wana-CCM.

Huu ni muendelezo tu wa uovu wa CCM miaka nenda miaka rudi ila bado tu hamuoni kuwa CCM haifai kuungwa mkono.
Sahihi sana.

Nililazimika kuchukua kadi ya CCM kwa usalama wangu kipindi cha jiwe maana mazingira niliyokuwepo kuwekwa mtu kati lilikuwa suala la muda tu, hata hii app ya JF ingekutwa kwenye simu yangu balaa lingekolea. Tena nikaongea na yule katibu wa tawi aniandikie nimechukua miaka miwili nyuma ili likitokea la kutokea ionekane mimi ni kijani kitambo.

Sasa baada ya jiwe kuondoka zake nikasema sasa huyu mama akiendeleza ubabe wa kipuuzi ni juu yake na miungu yake, mbwai mbwai. Nikaacha kulipia ada wala kubebelea lile likadi lao, baadaye walipoleta kadi za electronic wakawa wananistua nikashughulikie nikawa nawapanga nitachukua nikienda home. Ndio kwanza nikachoma moto ile kadi niliyokuwa nayo, shughuli yangu na CCM ikaishia pale.

Binafsi naona kuwa mwana CCM kwa mtu aliye nje ya mtandao wa wala keki ni kiwango cha juu sana cha ujinga, maana mtu unayashiriki mateso yako mwenyewe pamoja na ndugu, jamaa na rafiki zako moja kwa moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…