Wakat wa wa vita ya pili ya dunia moja ya Siri kubwa Kwa USA na washirika wake kupata ushindi ni kuwasikiliza waliokuwa front line yaani kwenye uwanja wa mapambano , na maoni Yao yalisikilizwa moja Kwa moja na high command ...
Ah nilikuwa nasoma nikijua sijui nitaona kitu cha ajabu labda ambacho sisi wengine hatujakiona. Lakini uongo mtupu. Kwanza kabisa katika hoja zako hizo hakuna hoja ya ukweli hata moja, mimi pia ni karani, na nipo na wenzangu kama 7 hivi, tulivyoona hii post tukasema ngoja tufuatilie kwa undani zaidi, kiukweli umeongea kimamluki hasa, na lengo lako ni kuchafua tu, hayo yote uliyasema hayana ukweli.
Tumefundishwa na tumeambiwa kuna vitu vimewekwa kwa lengo la kufundisha lakini sio eti ndivyo program itakavyofanya kazi hata wakati wa zoezi lenyewe la sensa. Kama vile kufuta taarifa, kwanza kufuta taarifa sio eti ukikosea, taarifa zinazofutwa ni za mazoezi, kama mtu anataka kufuta aanze mazoezi (practicals) upya, lakini sio akikosea kama ulivyosema wewe.
Ikitokea mtu anataka kurekebisha alipokosea halazimiki kufuta kila kitu na kuanza upya kama unavyosema wewe, huo ni uongo, hata hivyo wakati wa zoezi lenyewe hakutakuwa na option ya kufuta kama unavyojaribu kudanganya Watanzania.
Hakuna atakayeweza kufuta, msimamizi atakuwa na details tofauti za kuingia kwenye hii program tofauti na karani, kwahiyo karani hataweza kufanya atakachofanya msimamizi. Kingine ambacho unadanganya watu ni eti kutengeneza na kupikapika taarifa, unaonekana hata uelewa wa kawaida tu huna, muda wote kuna msimamizi anakufuatilia, kiongozi wa eneo unalofanyia kazi, wajumbe na viongizi wengine, lakini pia kuna taarifa zinajirekodi bila wewe karani kujua, HUTAWEZA KUPIKA TAARIFA kama unavyojinadi, hutapata hiyo nafasi, na ukweli ni kwamba utakamatwa tu, ufuatiliaji ni mkubwa sana, kuanzia kwenye program yenyewe, viongozi na wawakilishi.
Usidanganye watu. Kuhusu kuchukua majira nukta, program ya mwisho hutaweza kudanganya kama unavyosrma wewe. Japo signals za majira nukta zina changamito zake, ila haijawa changamoto kama unavyodai, usidanganye watu.
Halafu wewe huwezi kuwa karani, wala huwezi kuwa mzalendo, kwenye mafunzo haya ya sensa, makarani wote wanao uhuru na nafasi kubwa sana ya kuongea na kutoa maoni na changamoto zote wanazokuta nazo ili kuboresha program ya kuhesabia watu, imekuwaje wewe umeshindwa kutoa hayo maoni yako kwa wahusika eti mzalendo ukaona uje kuingelea huku jamii forum? Kwenye mafunzo changamoto zite zinakusanywa zinawakikushwa kwa lengo la kuzifanyia kazi.
Wewe ulikwama wapi kuwakilisha hayo maoni yako? Wewe ni mamluki tu, una malengo yako mengine na wajinga wenzako, program iko vizuri tu, na ni rahisi sana kuitumia, duniani nchi zote zimetumia hii hii CSEntry kufanyia sensa, na zinaendelea kutumia, zikiwemo nchi kama Marekani, UK, na nchi nyingine nyingi tu pamoja na nchi za kuafrika ambazi zimeshafanya hilo zoezi, na zingine zinajipanga kufanya hilo zoezi kwa kutumia hiyo hiyo CSEntry unayoiongelea...changamoto popote hazikosekani, zipo lakini ni ndogo sana, hata wewe na mke wako mnazo changamoto zenu kwenye maisha yenu, moja wapo ni wewe kukosa nguvu za kiume za kumridhisha mke wako mpaka anaku cheat. Ila kwenye sensa mambo yanaenda vizuri, acha kudanganya watu.
Changamoto zilizopo ni za kawaida sana, ambazo lazima zingekuwepo tu hata ingekyja program gani unayoijua wewe. Kajipange tena uje upya na mbinu nyingine ila hii umefeli, huo ujinga uliouongea watu wakisoma wanakuelewa wazi wazi umedanganya, tafuta uchafu mwingine wa kuchafua, lakini kijamii watu wa mlengo wa kushoto kama nyie mpo sana tu, na hamkosekani, hapo unataka kujifanya una akili nyiingii labda ni IT flani mtaalam wa mifumo, tunajua zipo program nyingi sana duniani zinafanya mambo mengi tu makubwa, ila umejisahau sehemu moja tu, sio applicable kila mahali, kwasababu za kimalengo na targets, kwa upeo wako mfupi una malengi yako, lakini sensa ina malengo yake, mengine yapo wazi kwa jamii, lakini mengine ni siri ambayo wewe huna ujuzi nayo.
CSEntry ni android version ya CSPro, kirefu cha CSPro ni Census and Surveys Program, yaani program maalum kwa ajili ya kuchakata taarifa za kitakwimu za sensa na tafiti mbalimbali, inayotumika dunia nzima. Ukiwa huelewi kuuliza ni kuelewa na sio ujinga, kama kweli wewe ni karani, umeshindwaje kuwasilisha haya maoni kwa wahusika kama sisi wengine tunavyofanya?
Eti mzalendo, mzalendo hayupo jamii forums, mzalendi anasimama na kutoa hoja kwa lengo la kusaidia au kuboresha au kuepusha hasara, na sio kushawishi kundi la watu kwa kutumia hoja za uongo, mzalendo mpaka uje jamii forums, ungesimama darasani ukawasilisha changamoto zako huo ndio uzalendo.
Nikuhakikishie wewe na wajinga wenzako kwamba HAMTAWEZA KUPIKA HIZO TAARIFA MNAZOJINADI ETI NI WAZALENDO, MRAKAMATWA TU. Wewe sio karani, sisi makarani wote mbona tunaelewa na tunafanya mafunzo na maxoezi vizuri.