Witness from the front line: Hili zoezi la sensa mlioko juu msiporekebisha haya kwa haraka tegemeeni taarifa mbovu kuwahi kutokea

Witness from the front line: Hili zoezi la sensa mlioko juu msiporekebisha haya kwa haraka tegemeeni taarifa mbovu kuwahi kutokea

Ardhi University kila mwaka wanatoa wataalamu wa GIS kwa nini wasitumie hao vijana kukusanya data na kutoa output...

Wale wanajua in and out jinsi ya geographical information systems zinavyofanya kazi...


Lakin cha ajabu unakuta NBS nzima hakuna GIS expert hata moja huku hao MaGIS expert wakipima viwanja

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Kabisa, jamaa ametoa alert ya jambo jema sana na Mungu ambariki kwa hilo.
Upikaji hapo lazima uwepo sababu:
1. itakuwa vigumu pia kuanza kumuhoji tena mtu ambaye ulishamuhoji kwa masaa mawili.....ataona anasumbuliwa
2. Wengi wa makarani wenyewe ni hawa vijana ambao wasio na ajira ambao kurahisisha mambo ni sifa yao kuu (rejea anuani za makazi)
Three quarters ni walimu

Nawasilisha..
 
Wakat wa wa vita ya pili ya dunia moja ya Siri kubwa Kwa USA na washirika wake kupata ushindi ni kuwasikiliza waliokuwa front line yaani kwenye uwanja wa mapambano , na maoni Yao yalisikilizwa moja Kwa moja na high command ...
Ah nilikuwa nasoma nikijua sijui nitaona kitu cha ajabu labda ambacho sisi wengine hatujakiona. Lakini uongo mtupu. Kwanza kabisa katika hoja zako hizo hakuna hoja ya ukweli hata moja, mimi pia ni karani, na nipo na wenzangu kama 7 hivi, tulivyoona hii post tukasema ngoja tufuatilie kwa undani zaidi, kiukweli umeongea kimamluki hasa, na lengo lako ni kuchafua tu, hayo yote uliyasema hayana ukweli.

Tumefundishwa na tumeambiwa kuna vitu vimewekwa kwa lengo la kufundisha lakini sio eti ndivyo program itakavyofanya kazi hata wakati wa zoezi lenyewe la sensa. Kama vile kufuta taarifa, kwanza kufuta taarifa sio eti ukikosea, taarifa zinazofutwa ni za mazoezi, kama mtu anataka kufuta aanze mazoezi (practicals) upya, lakini sio akikosea kama ulivyosema wewe.

Ikitokea mtu anataka kurekebisha alipokosea halazimiki kufuta kila kitu na kuanza upya kama unavyosema wewe, huo ni uongo, hata hivyo wakati wa zoezi lenyewe hakutakuwa na option ya kufuta kama unavyojaribu kudanganya Watanzania.

Hakuna atakayeweza kufuta, msimamizi atakuwa na details tofauti za kuingia kwenye hii program tofauti na karani, kwahiyo karani hataweza kufanya atakachofanya msimamizi. Kingine ambacho unadanganya watu ni eti kutengeneza na kupikapika taarifa, unaonekana hata uelewa wa kawaida tu huna, muda wote kuna msimamizi anakufuatilia, kiongozi wa eneo unalofanyia kazi, wajumbe na viongizi wengine, lakini pia kuna taarifa zinajirekodi bila wewe karani kujua, HUTAWEZA KUPIKA TAARIFA kama unavyojinadi, hutapata hiyo nafasi, na ukweli ni kwamba utakamatwa tu, ufuatiliaji ni mkubwa sana, kuanzia kwenye program yenyewe, viongozi na wawakilishi.

Usidanganye watu. Kuhusu kuchukua majira nukta, program ya mwisho hutaweza kudanganya kama unavyosrma wewe. Japo signals za majira nukta zina changamito zake, ila haijawa changamoto kama unavyodai, usidanganye watu.

Halafu wewe huwezi kuwa karani, wala huwezi kuwa mzalendo, kwenye mafunzo haya ya sensa, makarani wote wanao uhuru na nafasi kubwa sana ya kuongea na kutoa maoni na changamoto zote wanazokuta nazo ili kuboresha program ya kuhesabia watu, imekuwaje wewe umeshindwa kutoa hayo maoni yako kwa wahusika eti mzalendo ukaona uje kuingelea huku jamii forum? Kwenye mafunzo changamoto zite zinakusanywa zinawakikushwa kwa lengo la kuzifanyia kazi.

Wewe ulikwama wapi kuwakilisha hayo maoni yako? Wewe ni mamluki tu, una malengo yako mengine na wajinga wenzako, program iko vizuri tu, na ni rahisi sana kuitumia, duniani nchi zote zimetumia hii hii CSEntry kufanyia sensa, na zinaendelea kutumia, zikiwemo nchi kama Marekani, UK, na nchi nyingine nyingi tu pamoja na nchi za kuafrika ambazi zimeshafanya hilo zoezi, na zingine zinajipanga kufanya hilo zoezi kwa kutumia hiyo hiyo CSEntry unayoiongelea...changamoto popote hazikosekani, zipo lakini ni ndogo sana, hata wewe na mke wako mnazo changamoto zenu kwenye maisha yenu, moja wapo ni wewe kukosa nguvu za kiume za kumridhisha mke wako mpaka anaku cheat. Ila kwenye sensa mambo yanaenda vizuri, acha kudanganya watu.

Changamoto zilizopo ni za kawaida sana, ambazo lazima zingekuwepo tu hata ingekyja program gani unayoijua wewe. Kajipange tena uje upya na mbinu nyingine ila hii umefeli, huo ujinga uliouongea watu wakisoma wanakuelewa wazi wazi umedanganya, tafuta uchafu mwingine wa kuchafua, lakini kijamii watu wa mlengo wa kushoto kama nyie mpo sana tu, na hamkosekani, hapo unataka kujifanya una akili nyiingii labda ni IT flani mtaalam wa mifumo, tunajua zipo program nyingi sana duniani zinafanya mambo mengi tu makubwa, ila umejisahau sehemu moja tu, sio applicable kila mahali, kwasababu za kimalengo na targets, kwa upeo wako mfupi una malengi yako, lakini sensa ina malengo yake, mengine yapo wazi kwa jamii, lakini mengine ni siri ambayo wewe huna ujuzi nayo.

CSEntry ni android version ya CSPro, kirefu cha CSPro ni Census and Surveys Program, yaani program maalum kwa ajili ya kuchakata taarifa za kitakwimu za sensa na tafiti mbalimbali, inayotumika dunia nzima. Ukiwa huelewi kuuliza ni kuelewa na sio ujinga, kama kweli wewe ni karani, umeshindwaje kuwasilisha haya maoni kwa wahusika kama sisi wengine tunavyofanya?

Eti mzalendo, mzalendo hayupo jamii forums, mzalendi anasimama na kutoa hoja kwa lengo la kusaidia au kuboresha au kuepusha hasara, na sio kushawishi kundi la watu kwa kutumia hoja za uongo, mzalendo mpaka uje jamii forums, ungesimama darasani ukawasilisha changamoto zako huo ndio uzalendo.

Nikuhakikishie wewe na wajinga wenzako kwamba HAMTAWEZA KUPIKA HIZO TAARIFA MNAZOJINADI ETI NI WAZALENDO, MRAKAMATWA TU. Wewe sio karani, sisi makarani wote mbona tunaelewa na tunafanya mafunzo na maxoezi vizuri.
 
Wakat wa wa vita ya pili ya dunia moja ya Siri kubwa Kwa USA na washirika wake kupata ushindi ni kuwasikiliza waliokuwa front line yaani kwenye uwanja wa mapambano...
Hio kazi ulioitaja hapo wala sio ya maIT...

Hio ni ya watu wa GIS ambao waspecialize kwenye Geographical information systems.

Mimi ni GIS expert.

Pale Ardhi University kuna wanafunzi wengi wa GIS kwa nini wasingewaweka hao wanafunzi wenye uelewa wa Geographical information systems.

Programme za kucollect Geographical data zipo nyingi na nzr mfan😵DK, Survey123 nk...hiz accuracy yake ni nzr na zinaleta data zinazotumika kwenye GIS software?

Hivi hapo sensani kuna wataalamu wa GIS kweli?

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Siyo sehemu moja, bali karibia nchi nzima wametoa laki mbili tu! Huku watu wanatumia gharama kubwa kila siku kwa ajili ya kujikimu...
Wakifanya hivyo watu watakula wapi,.Hivi bado hujaielewa hii nnchiiii.
 
Watu kujua kwingi!!!

Huyo mjumbe anajua sensa ni nini hata au kujua idadi ya watu kwenye kitongoji chake tu ndo inatosha

Acheni ujuaji sensa ina taratibu zake na namna yake maalumu ya kukusanya taarifa mbalimbali (tena nyingi kweli kweli) na ndio maana watu wanakula semina kwa takriban theluthi ya mwezi
Acha mbwembwe wewe,Mambo mengine yapo kwasababu yamewekwa ila hakuna chochote kipya maana zaidi yakuuliza maswali hakuna ela yoyote wanayogawa ili kufanya hilo zoezi liwe kubwa kiasi ambacho unataka kutuambia.
 
Ah nilikuwa nasoma nikijua sijui nitaona kitu cha ajabu labda ambacho sisi wengine hatujakiona. Lakini uongo mtupu. Kwanza kabisa katika hoja zako hizo hakuna hoja ya ukweli hata moja, mimi pia ni karani, na nipo na wenzangu kama 7 hivi...
Kwa jinsi ulivyoandika inaonesha wewe ndio unachuki. Unaona jamaa anataka kukuharibia ugali wako.
Jamaa anasema keshaeleza hizo changa moto kwa wasimamizi lakini wanakuwa wakali kama wewe ulivyojibu kwa ukali.
 
Ah nilikuwa nasoma nikijua sijui nitaona kitu cha ajabu labda ambacho sisi wengine hatujakiona. Lakini uongo mtupu. Kwanza kabisa katika hoja zako hizo hakuna hoja ya ukweli hata moja, mimi pia ni karani, na nipo na wenzangu kama 7 hivi...
Umeandika ujinga mwingi alafu umekuja kukubali kua kuna changamoto,sasa alichokosea mtoa mada nini au nyie ndo ambao hamtaki jambo linalotumia kodi zetu likiwa na madudu tusijue.

Mtoa mada katoa changamoto aliziona yeye sio lazima wewe uzione kama ni kilaza na kashauri zifanyiwe kazi ili zoezi liwe na tija wewe badala yakumjibu vizuri kwa hoja umekalia kujibu ujinga tu.Kama nawewe ni karani ni sehemu ya changamoto pia.
 
Bora zoezi lifeli tu wanajua finally watakuja na population ya watu 65milioni, kinachoendelea na matumizi ya bajeti yakamilike tu, Projections tunazo , the population doubles after a certain time, roughly 60-70 Million population
 
Posho ni 50 ukitoa 10 ya chakula inabak 40k,nyie Bunda hesabu zenu zikoje
achana na kitu inaitwa BUNDA DC na BUNDA TC yaan hata majengo ya Halmashauri yameezekwa na Mirunda. Mtafute popote Ally Hapi akwambie Halmashauri iliyomchania mkeka atakwambia. Bunda ni uozo mtupu.
 
Wewe ni mzalendo ila kwa bahati mbaya hawatakusikiliza sababu lengo la serikali yetu si ufanisi wa kazi bali kumaliza kazi, data zingine wataenda kuzipika na kuzichekecha wenyewe huko...
Hilo li application la bwana Rostam hilo
 
Mimi nishajiandaaa kupika data mwanzo mwisho nichukue changu nisepe full stop

Uzalendo wabaki nao wenyewe kwenye viyoyozi huko.....
Wewe uko na akili nyingi ...japo kuwa mimi siyo muhuni hila kwa hili naunga mkono UHUNI
 
Ah nilikuwa nasoma nikijua sijui nitaona kitu cha ajabu labda ambacho sisi wengine hatujakiona. Lakini uongo mtupu...
Watu tunatengeneza ID mpya kusaka wachumba na fuvkmates humu ndani, ila wewe umetengeneza ID mpya kuja kukanusha changamoto za sensa?

Who are you mr, wewe ndo ulopewa tender hii ya kushughulikia CSEntry sio? Na sasa unapambana kukanusha changamoto ili uonekane unaperform vizuri sio?

Au wewe ndiye mkuu wa NBS, umeona sensa inaenda kuborongeka ndiyo na kibarua chako kitaota nyasi sasa umeamua kuingia mwenyewe ulingoni ili kujipambania! Eti, naongea na wewe boya usiyekuwa na akili.

Au wewe ndiye mama makenda mwenyewe? Au utakuwa waziri husika wa sensa? Au IT mkuu wa wizara husika? Wewe nani?

Alichoeleza mleta uzi kina ukweli, hata mimi mke wangu yupo huko kwenye sensa kama karani ila naona siku hadi siku anatamani kuachana na hili zoezi maana ni zito kuliko walivyotegemea!

Wewe kwa limwandiko lako lisilo na aya wala indents wala spacing unaonekana ni lizee flani linalohusika pakubwa na sensa. Kwa kuwa jamaa ka-hit the painful area sasa mmepaniki mnajaribu kuingia wenyewe ulingoni kukanusha.

Mimi nikuhakikishie tu sensa hii huenda data za sensa ndizo zikapikwa kushinda sensa zingine zote. Sababu kubwa ni kwamba mnatumia digital technology, na bahati mbaya nasikia wasimamizi wa maudhui mmewekana mijimama na mijibaba ambayo teknolojia kwao ni tatizo kwenye matumizi. Imagine msimamizi wa maudhui anapata shida kwenye kuconnect bluetooth na location ya kishikwambi chake, mpaka makarani wanawasaidia. Yani wasimamizi ni vilaza kushinda wanaowasimamia, halafu unasema data hazitapikwa?
 
Kwa namna sensa inavyoendeshwa nchi hii, ni mradi wa upigaji. Tuna wajumbe wa kazi gani kama hawajui idadi ya kaya zilizopo kwenye maeneo yao pamoja na idadi ya watu kwa kila kaya?

Badala ya kutumia billions of taxpayers ' money, kwanini wasingepewa wajumbe wa nyumba kumi hii kazi wakaifanya taratibu hata kwa miezi kadhaa huku wakipewa posho?

Wizi mtupu!
Wajumbe ndiyo wanajua vizuri watu wao mitaani huo ndiyo ukweli ...pia swala la wanao ishi mtaani ilitakiwa liwe la kudumu na liusishe polisi sikuzote mpangaji akija kuishi mtaani ilitakiwa asajiliwe kwa mjumbe yeye na familia yake na majina kuingizwa kwenye system za polisi automatic....mambo ya waamiaji haramu ,panya road, ujambazi , vibaka yangepungua maana kila mtu angejulikana anaishi wapi na katokea wapi siyo sasa hivi tunaishi mpaka na wakimbizi bila ya kujua.
 
Back
Top Bottom