Wito: CHADEMA chagueni Mwenyekiti mwingine, Mbowe kutoka ni ishu ya miaka

Wito: CHADEMA chagueni Mwenyekiti mwingine, Mbowe kutoka ni ishu ya miaka

Hili ndilo lilikuwa lengo lenu
Leo nimemsikiliza mzee mmoja mstaafu kutoka Kitengo cha Kupambana na Ugaidi Tanzania.

Nimeshtuka sana pale aliponiambia kuwa ili mtu akamatwe kwa kosa la ugaidi lazima Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi atoe amri baada ya kujiridhisha na ushahidi wa mshukiwa.

Amenihakikishia kuwa trials za ugaidi si chini ya miaka 4 na mara nyingi huchukua muda zaidi na mshukiwa huweza kukaa ndani kwa kuogopa usalama wa nchi maana ugaidi ni mfumo.

Sasa nawashangaa CHADEMA badala ya kutafuta mrithi wa Mbowe wako bize na mabango wakati kule Afghanistan, Syria, Mozambique, Eritrea,Kenya na Nigeria hata Indonesia mtu akikamtwa kwa ugaidi ndio Basi tena.

Ni Bora CHADEMA kujielekeza kwenye kujenga chama badala ya kusubilia dodo chini ya mpera.

Kesi ya ugaidi sio kama kesi ya kuiba simu mitaani. Hapa Mbowe itachukua miaka kibao kutoka au kupewa dhamana.

Mashekhe wa uamsho wamekaa miaka 9 tena wao ni viogozi wa dini kwenye nchi yenye waislamu wengi na bado wamekaa. Mashekhe walitetewa na viongozi wa juu wa kitaifa na bado walikaa sana, tena Sana.

Kule USA Gwantanamo magaidi hadi leo wana miaka zaidi ya 25 wapo tu na kesi zao zipo kwenye trial, sasa ndo itakuwa Mbowe?


USSR
 
Mwenyekiti yupo korokoroni,Makamu wake yupo uhamishoni na Katibu Mkuu wa chama ni Bubu.

Hizo nafasi zote zipo wazi.
 
Kwanza nianze kwa kumshukuru Mungu juu ya nafasi ya uhai aliyotupa
Kimsingi mm ni miongoni mwa watu wakioshiriki harakati mbalimbali na naomba niwape utofauti kati ya Ccm na Chadema
Chadema wamejikita katika nguvu ya mtu wakati Ccm wamejikita katika taasisi
Na mfano ni sasa wakati Ccm wanajipambanua kama chama kilichokomaa na chenye uwezo wa kuongeza nchi Chadema ni one man show
Ccm ina mizizi Chadema ina kariba ya watu na wanaharakati ambao hubadirika kulingana na nuktadha uliopo
Ccm itaendelea kushika Dola Chadema wataendelea kutumia mitandao ya kijamii ambayo asikimia 80 ya walio kijijini hawamjui kigogo,Twitter wala jamii forum ambao kwa idadi ni wengi na wana INFLUENCE kwenye maamuzi katika upigaji kura
Sisi Ccm nini tufanye?
1. Siyo kila sauti inaashiria hatari nyingine ni soga tu
2.Tuwe na collective responsibility kwa maana chain of responsibility ianzie juu nishike chini kama ilivyo siyo kila anapewa nafasi anasema lake
Nitaendelea baadae
 
Back
Top Bottom