Wito: Kamati Kuu ya CCM ifunguliwe Mashitaka Mahakama Kuu kwa Kumteua Mgombea Urais aliyekosa Sifa 2015

Wito: Kamati Kuu ya CCM ifunguliwe Mashitaka Mahakama Kuu kwa Kumteua Mgombea Urais aliyekosa Sifa 2015

Magufuli alisimamishwa kurudisha imani ya Lumumba na viunga vyake kwa wananchi. Kipindi kile bila yeye sijui Lumumba wangekuwa wapi.
Kwani sasa hivi wako wapi? Nasikia mama kapiga nyundo huko Marekani Mataga wametaga
 
Magufuli aliwaumiza sana wana CHADEMA mpaka leo kawaacha na makovu. Hamtamsahau, mtamkumbuka mno!
Infact aliwaondoa kwenye ramani ya siasa za Tanzania, huko mitaani hawana ushawishi kqbisa wamebaki mitandaoni tu. Hebu fikiria chama kilikua na wabunge Mia moja na ushee mpaka sasa kina mbunge mmoja tu. We unadhani kwa hali hiyo wanaweza kumpenda Magufuli? Yaani kufa tu wanaona haitoshi wanatamani wakafukue kaburi lake wamuue tena.

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
 
Miongoni mwa Mashahidi anaweza kuwa Zitto Kabwe
 
Miongoni mwa mambo ambayo nchi hii itajutia katika maisha yake yote yaliyosalia hapa duniani ni kuruhusu John Magufuli kuwa Rais wake , aliyoyatenda alipokuwa Rais kwa hiyo miaka mitano na Ushee kila mtu ameyaona , hakuna haja ya kuyarudia

Kabla ya kuwa Rais Magufuli alikuwa Waziri , kila mwenye macho aliona mambo aliyoyatenda akiwa Waziri , yalikuwemo Mazuri na Mabaya , huyu aliisababishia serikali hasara kwa kukamata meli ya uvuvi , hakuna aliyesahau hili , alipania kubomoa jengo la Tanesco Ubungo , akakatazwa na Mizengo Pinda , lakini alipotwaa madaraka akalibomoa , wala barabara iliyojengwa haikufika hata ulipokuwa ukuta wa Jengo hilo , hakuwa na sababu yoyote ya kulibomoa zaidi ya ile "UNANIJUA MIMI NI NANI"

Magufuli hakuwahi kuwa muumini wa Demokrasia kuanzia jimboni kwake , mara zote alifanya njama ili apite bila kupingwa , Uongozi ni jambo la Pamoja , yeye aliamini kwenye akili yake tu , haya yote viongozi wake wa chama waliyajua .

Ziara ya Marekani ya Rais Samia imeweka wazi yale yote tuliyokuwa tunayatilia shaka , Ripoti ya CAG imeonyesha wazi kwamba Magufuli hakuwahi kuwa Mlinzi wa rasilimali za Taifa kama tulivyodhani , alitudanganya na Ukuta wa Mererani huku madini yakiibwa !

Kwa kufupisha , Natoa wito kwa Wadau wote wenye uchungu na nchi hii KUWAFUNGULIA MASHITAKA JAKAYA KIKWETE , ABDULRAHMAN KINANA , waliokuwa viongozi wa juu wa ccm na Kamati Kuu ya Chama hicho kwa kuruhusu John Magufuli kugombea Urais wa Tanzania huku wakijua kwamba ana Mapungufu ya kutisha .

Nakala : Peter Kibatala

Jengo lilibomolewa?
 
Jiwe umepoteza na kutesa watu weee na wewe arobaini zako zikatimia.. haya hilo li uwanja lako la ndege njoo ulichukue hatulitaki sisi...umemwachia nani ?
 
Back
Top Bottom