Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Kile kitendawili cha chaguo kati ya kura ya siri au kura ya wazi, kitapatiwa ufumbuzi wiki hii, ambapo waheshimiwa wabunge wetu, wa Bunge Maalum la Katiba, watapiga kura kuamua kama kura ziwe za wazi au za siri.
Kikawaida uchaguzi wowote unaoitwa huru na wa haki, kura hupigwa kwa siri "secret ballot" ili kulinda uhuru na haki ya mpiga kura!.
Hata hivyo kuna wenye hoja ya msingi kuhusu kura ya wazi kwa kisingizio eti kwa sababu wao ni wawakilishi wa wananchi, wanadai wanapaswa kupiga kura ya wazi, ili wale wananchi waliowatuma, wawaone na kuujua msimamo wao, wazi wazi na wengine hadi kudiriki kudai kuwa wanataka wananchi wawashuhudie wakifanya kile wananchi hao walichowatuma!.
Ukweli wa mambo ni kuwa, hoja hiyo ni uongo mtu, uongo mtakatifu! unaotumiwa ili kuhalisha ubabe na kuburutwa na CCM na vibaraka wake, wakiwemo makuwadi wa siasa za ukandamizaji!. Ukiondoa wale wawakilishi 201 ambao ni wateule wa Rais, hao angalau wametumwa/jituma kuziwakilisha taasisi zao, au vikundi vyao, na sina uhakika kama wanachama wote wa taasisi hizo, auvikundi hivyo, walikaa pamoja na kuwatuma mkifika huko mfanye hili au lile zaidi ya kuwatuma wakatetee maslahi yao!. Kwa vile hivi ni vikundi tuu vya watu, hawa ni wawakilishi wa vikundi na sio wawakilishi wa watu!, yaani wananchi kwa sababu hakuna mwananchi aliyewachagua wala kuwatuma!.
Tukija kwa waheshimiwa wabunge wetu wa bunge la JMT na BLW, hawa kweli ni wawakilishi halali wa wananchi na tumewachagua kwa kura zetu, waende kutuwakilisha ndani ya mabaraza ya kutunga sheria Bunge na BLW, tulichowatuma ni kwenda kutuwakilisha bungeni!, na sio kwenda kutuandikia katiba!.
Hivyo hakuna mbunge yoyote au mwakilishi yoyote aliyetumwana na mwananchi yoyote kwenda kule kwenye Bunge Maalum la Katiba kumwakilisha!, ila uwakilishi huo ni by proxy ya kwa kwa vile tulimtuma kihalali kwenda kutunga sheria, na miongoni mwa sheria halali waliotunga, ni ile sheria ya mabadiliko ya katiba, na kwa sheria hiyo, wakajipendekeza wao ndio wajigeuze wawakilishi wetu kwenye Bunge Maalum, then wao kuwa ni wawakilishi wa wananchi ni saawa kisheria, ila hakuna mwananchi yoyote aliyewatuma!, hivyo wapige kura za siri, na sio kusingizia eti wananchi wamewatuma!.
Wabunge hao, hawana kitu kinachoitwa "people mandate", kwa sababu hakuna mwananchi aliyepata fursa ya kumchangua mwakilishi wake hata mmoja ndani ya bunge maalum, zaidi ya huo uwakilishi by proxy, hivyo kura halali ni kura za siri!. Period!.
Kufuatia Mapendekezo ya Tume ya Warioba kupendekeza serikali 3, na Chama cha Mapinduzi, kuweka wazi msimamo wake ni wa serikali mbili, zikipigwa kura za wazi, hakuna mwana CCM yoyote atakayethubutu kupigia kura serikali tatu, hivyo kwa kuhofia kwenda kinyume cha matakwa ya chama chake, hivyo kutopiga kura kwa uhuru na haki. bali kufuata matakwa ya chama chake.
Mahakama zinapotoa uamuzi wa haki, pia huwa zinazingatia madhara yasiyorekebishika "irreparable damegge!", vivyo hivyo katika kupiga kura za wazi, yule mwana CCM mwenye kupenda serikali tatu, atapata "irrepable damegge" kama atakwenda kinyume cha msimamo wa chama chake!. Matokeo yatakuwa ni kushinda kwa hoja ya serikali mbili, hivyo kuendelea na sherikali mbili kwa ushindi wa kitisho, hivyo kukosa haki japo uhalali!.
Lakini kama CCM kimewapika vizuri makada wake kuunga mkono hoja ya serikali mbili na wote wakaikubali ndani ya mioyo yao, hata zikipigwa kura za siri, hao makada wake wote watapigia kura serikali mbili, hivyo hoja ya serikali mbili itakuwa imepita kwa kura ya huru na ya haki, hivyo kuendelea na serikali mbili kwa haki na kihalali.
Waheshimiwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Please, Don't let us down!.
Mungu Ibariki Tanzania.
Mungu wabariki Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Kuona Kweli, Kutenda Haki, na Kufanya Kweli!.
Pasco.