Wito kwa Bunge la Katiba: Kura iwe ya Siri kwasababu Hakuna aliyetumwa na Watu Kuwawakilisha!

Wito kwa Bunge la Katiba: Kura iwe ya Siri kwasababu Hakuna aliyetumwa na Watu Kuwawakilisha!

ni ujingaaa,kura za siri ni kwa uchaguzi wa watu co mambo ya kitaifa kama bajeti ya nchi as same as katiba ya nchi.wapige wazi tujue wapi wawakilishi wa wananchi au wawakilishilishi wa vitambi...
 
ni ujingaaa,kura za siri ni kwa uchaguzi wa watu co mambo ya kitaifa kama bajeti ya nchi as same as katiba ya nchi.wapige wazi tujue wapi wawakilishi wa wananchi au wawakilishilishi wa vitambi...

ukishajua then what next.

Kujua nani kapinga nani kakubali haina tija kwenye swala nyeti kama katiba ya nchi, 4get about budget ambayo ni makadilio tu ya mapato na matumizi, katiba ni real mkuu
 
Ikiwa ya siri utasikia "KURA ZIMECHAKACHULIWA"
Bora iwe wazi wamalize kieleweke
 
ni ujingaaa,kura za siri ni kwa uchaguzi wa watu co mambo ya kitaifa kama bajeti ya nchi as same as katiba ya nchi.wapige wazi tujue wapi wawakilishi wa wananchi au wawakilishilishi wa vitambi...

kama wanataka uwazi kwanini wawazuie waandishi wa habari kuingia kwenye kamati?
 
Thibitisha kama ni kweli imepitishwa hiyo kura ya siri
 
Imepita kuwa upigaji kura ni wasiri ,kuna mtu kanibeep sasa hivi.

kama ni hivyo, hatua ya kwanza imemalizika.
Hatua ya pili ni kuhakikisha kura hazichakachuliwi.
 
Mimi nataka kuamini kuwa CCM ni ugonjwa. Haya nalazimika kuyasema baada ya kuona wanavyojitahidi kwa hoja za uongo ili kupotosha ukweli huku wakijua dhahili kuwa kinyume cha hayo wanayosema ndiyo ukweli.

Nilianza kuwastukia wakati ule wa hoja ya Mbatia na mitaala. Walikazana hoja iondolewe huku kila kitu kiko wazi kuwa elimu ya Tz inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mitaala na mihtasari kwa ujumla wake.

Nikaja kushangaa tena wakati ule wa hoja ya Mnyika na mambo ya maji kwenye jiji la Dar. Habari iko wazi kuwa mradi ule wa wachina watu wamekula hela na kupelekea kazi kutokukamilika. Wabunge wa CCM walichachamaa kuivuruga hiyo hoja kama vile wao ndiyo walioiba hizo hela. Ninaimani hawakufaidika na chochote ila kwavile wao ndiyo wenye uwezo wakupindisha ukweli kwa kutegemea uwingi wao mambo yalienda kombo na waliokula waliendelea kuwa salama.

Ukiacha hayo na mengine mengi, kuna hili suala la kura ya siri. Hivi kuna mtu asiyejua umuhimu wa kura ya siri? Hivi kama mimi ni mpiga kura na baba yangu ni mgombea, kama sitaki kumpigia kura kwasababu zangu naweza kupiga kura ya wazi? Kama Sitta atakuwa mgombea Urais kupitia CCM naamini lowasa hatampa kura, je unadhani kama kura itakuwa ya wazi CCM watamuacha salama Lowassa?

Kutokumpigia kura mwana CCM mwenzio au ndg yako ni haki yako kikatiba, kwahiyo kura inapokuwa siri humfanya mpiga kura awe huru.

Humo bungeni tunajua MaCCM ni wengi kwa kiasi kikubwa na tunajua wametumwa kwenda kutetea maslahi ya chama chao kwa tiketi ya uwingi wao. Kwakuwa inajulikana kuwa nia ya CCM si njema Wanajua kuwa kutatokea ukengeufu ndiyo maana wanapigania kura zipigwe kwa uwazi ili waone kama Lowassa anao ujasiri wa kutompigia kura Sitta hata kama hampendi kinoma.

Ukiwasikiliza watoa hoja za kupinga utagundua kuwa si wazima. Kama si matumbo yanawasumbua bac kuna tatizo jingine. Lakini ni matumbo yao. Watu hao wanatumika kama vuvuzela na malipo yao ndiyo tiba ya ugonjwa wa wa matumbo.

Mfano wa watu waliopewa dawa na wanaonyesha kupona ni Mwigulu na Muhagama. Wanaoendelea kuugua ni Serukamba, Sendeka na Kilango. Dawa zao zimekwisha hadi hapo waliopewa waziteme. Kwahiyo huku wanabwata huku wanawaza lini wale waliopewa dawa watazitema.
 
Mkuu, binafsi siamini kama suala hili la kura ya Siri ni la CCM. Kuna wana ccm wengi ambao wameweka msimamo wa kutopenda kura ya wazi. Pia kuna wana ccm wengi ambao hawapendi muundo wa serikali mbili. Hivyo, ingawa taasisi imetoa uamuzi huo, ila ndani yake kila mtu anawaza la kwake
 
Kwa hiyo bado litabaki kuwa ni la CCM ili kuwatisha wale waoga ambao wanaotaka serikali tatu wasipige kura kuunga mkono kwa kuogopa kibano baada ya kupiga kura.
 
Kwa hiyo bado litabaki kuwa ni la CCM ili kuwatisha wale waoga ambao wanaotaka serikali tatu wasipige kura kuunga mkono kwa kuogopa kibano baada ya kupiga kura.
Hapana mkuu. Katika hili, ni wazi kuwa wana ccm watakuwa huru kuamua. Hakuna kushurutishwa
 
Mkuu, binafsi siamini kama suala hili la kura ya Siri ni la CCM. Kuna wana ccm wengi ambao wameweka msimamo wa kutopenda kura ya wazi. Pia kuna wana ccm wengi ambao hawapendi muundo wa serikali mbili. Hivyo, ingawa taasisi imetoa uamuzi huo, ila ndani yake kila mtu anawaza la kwake

Unabisha huku unatoa sababu mwenyewe!!! Ni kweli kuna CCM wengine hawapendi kura ya wazi ili wawe huru kufanya maamuzi na pia wapo wengi tu wakipinga msimamo wa chama juu ya serikali mbili... Baada ya CCM kutambua hilo ndiyo wamekuja na huo mkakati wa kura ya wazi ili iwadhibiti wanachama wake wanye msimamo tofauti.... Hilo liko wazi CCM tena n viongozi wachache sana wenye kulinda maslahi yao ndiyo wanaharibu mchakato mzima wa Katiba
 
Kuna hoja zilizo ndani ya Bunge Maalumu la katiba, Eti wananchi tuliowatuma tunataka tuone kura za aina gani wajumbe mmepiga , HUU NI UONGO na ni hoja isiyo na mashiko, hivi ninyi wajumbe kabla ya kwenda huko Dodoma mlikutana nasi wapi ? Sisi HATUKUWATUMA hata kidogo, tulishatoa hoja zetu kwenye mabaraza na wala hatukutoa maagizo ya kura ya wazi, MSITUGAWE, Hatutaki kujua misimamo ya Viongozi wetu wa kiimani/kidini na baadhi ya wajumbe wetu tunaowaheshimu kupitia kura ya wazi. SISI WANANCHI TULIO WENGI TUNATAKA MPIGE KURA ZA SIRI kama mnataka kudhibiti suala la serikali 3 tafuteni njia nyingine, lakini pia kiongozi wetu alituambia TUJIANDAE KISAIKOLOJIA
 
maneno magumu hayo
 
Kaka ccm hawaitaki katiba mpya mbona hamuwaelewi? Kusoma hatujui hata picha tunashindwa zitambua?
 
Tatizo ni CCM kushindwa kuleta serikali moja, sasa hakuna mbadala wa serikali tatu maana CCM inamsimamo mmoja ili hali wanaCCM wana msimamo mwingine; Kura ni za Siri hata iweje ili CCM waumbuke mchana kweupe. Je kuna mtu anaakili ni kiongozi wa CCM haoni kuwa CCM serikali 2 ni ya viongnzi na CCM serikali 3 ni ya wanachama???
 
Sisi na nani? we umekuwa msemaji wa wote? nani amekutuma utusemee?
 
Hapana mkuu. Katika hili, ni wazi kuwa wana ccm watakuwa huru kuamua. Hakuna kushurutishwa

Wameshashurutishwa mkuu. Kwani anaposimama Nape na kusema msimamo wa CCM ni serikali mbili na wamewatuma wabunge wao kulitetea hilo anamaanisha nini? Mwana CCM yeyote atakae enda kinyume na msimamo wa chama atatakiwa kujieleza kama sio kufukuzwa kabisa. Njia pekee ya kuwalinda wale wana CCM wenye mawazo tofauti ambao naamini wako wengi sana waliochoka kuburuzwa ni kura ya siri.
 
Well stated mkuu
 
Kura ya siri naunga mkono. Wanaotaka kura ya wazi ni kutojiamini, wanataka kujua nani yuko upande wao nani yuko kinyume na wao.
 
Back
Top Bottom