Wito kwa Bunge la Katiba: Kura iwe ya Siri kwasababu Hakuna aliyetumwa na Watu Kuwawakilisha!

... Soma vizuri nguzo kuu za Demokrasia utakuta kura ya wazi (secret ballot) ni nguzo mojawapo ya demokrasia...[/QUOTE]

Samahani sijakuelewa hapo kwenye RED unaweza kunifafanulia kidogo tafadhali?
 
Mfano ni kama Prof.Safari analazimika kufuata msimamo wa CHADEMA hata kama yeye binfsi hakubaliani nao maana yeye ni mwakilishi rasmi wa CDM ila sio F.Mbowe, huyu analazimika kufuata matakwa ya wananchi wake wa Hai hata kama yeye binafsi hakubaliani nayo. Na kwenye kura ya wazi atapigia matakwa ya wananchi wake na sio msimamo wa chama chake maana anawajibika kwa wananchi moja kwa moja.
Pamoja na mawazo mazuri na nia njema hujagusa ukweli uhusiano wa vyama na wabunge wake. Kwanza kwa mfumo wetu uwakilishi huo wa wananchi haupati ila kwa idhini ya chama chake. Ndiyo maana kuna tahaluki kubwa sasa kwa sababu 2015 si mbali. Vyama vimeshika rungu na ukisikiliza kauli za vyama ni dhairi utagundua kuna vitisho vya aina fulani.

Ni kweli kabisa tungependa kupata misimamo ya wabunge wetu na nitapenda kuona hili linaingia kwenye Katiba ili kuachana na kura za kelele. Sit akin kuona mbunge niliyemchagua anakwenda kuunga mkono k.m. ndoa za jinsi moja. Lakini bahati mbaya mazingira ya sasa ili kutupa Katiba ya namna hii yenye dhamira sahihi za wawakilishi wetu, kura ya Siri nafikiri ndiyo suluhisho. Lakini whakikishe wanafuta kupitisha bungeni hoja kwa kelele.
 
Nimefuatilia sana malumbano yanayoendelea kwenye bunge maalum la Katiba kuhusu mambo mbalimbali,kama akidi,jinsi ya upigaji kura na mengine. Kwa leo nijadili kidogo tu kuhusu kura ya WAZI na SIRI.
Kwa namna yoyote ile kura ya WAZi ndio sahihi kutumika kwa sababu wajumbe ni wawakilishi wa watu wengine kwa hiyo hawapigi kura kwa dhamira zao binafsi ila kwa mujibu wa wale wanaowawakilisha. Kama mjumbe ametokana na jimbo la uchaguzi lazima apige kura kulingana na wananchi wake wanavyotaka hata kama yeye binafsi hapendi na lazima watu wake wajue kama mwakilishi wao amewawakilisha vilivyo na akienda kinyume na matakwa ya wananchi wake inabidi wananchi wamwajibishe moja kwa moja na wala sio chama chake. Kwa wale wanaowakilisha vyama vya siasa ambao ni kama 42 hivi kila mmoja anatakiwa kupiga kura ya wazi kulingana na msimamo wa chama chake na akienda tofauti anastahili kuwajibishwa bila huruma kwani kura si ya kwake binafsi bali ni ya wale waliomtuma,kwa hiyo anawajibika kupigia kura msimamao wa waliomtuma hata kama yeye binafsi hakubaliani nao. Vivyo hivyo wabunge wa viti maalum wanawajibika kwa wanawake waliowapeleka huko na si vyama vyao, utaratibu ni huo huo kwa wale wa makundi maalum wanawajibika kupiga kura kwa matakwa ya waliowawakilisha na si kwa matakwa yao binafsi.
Watu wengi kwa sasa wanaogopa kura ya wazi kwa hofu kwamba watabanwa na misimamo ya vyama vyao,huu ni "uhuni" chama kinatakiwa kuwabana wawakilishi wao rasmi tu, ambao ni kama wawili watatu kwa kila chama wengineo wanabanwa na wale wanaowawakilisha,na kama mwakilishi rasmi wa chama akienda tofauti na msimamo wa chama huyo lazima awajibishwe ila sio mwanachama wa chama fulani anawakilisha wananchi wake hata wasio na vyama alazimike kufuata matakwa au msimamo wa chama chake.
Kwa mawazo hayo kama itapigwa kura ya siri wanachi watajuaje kama matakwa yao na si matakwa binafsi ya mwakilishi wao yamezingatiwa? Hebu tutafakari pamoja kwa nguvu ya hoja...

wewe mwenyewe unajikanyaga umeshasema hawa CCM wanalazimishwa kufuata msimamo wa chama na sio wananchi na maoni ya wananchi ili kukiokoa chama., sasa bas hiyo ni sababu tosha kura iwe ya siri ili haki iliyo katika nafsi zao iweze kupatikana kwa maslahi ya taifa na wawo wawe salama wakitoka hapo bungeni
 
Kama kura itakuwa ya siri je mimi ninayewakilishwa nitajuaje mwakilishi wangu kama ameniwakilisha vilivyo au amejiwakilisha binafsi na matakwa ya familia yake, hapa nitamuwajibishaje bila ushahidi?

Mwakillishi sio Lazima atekeleze yote aliyokuahidi.Utampima kwa kutekeleza asilimia kubwa ya aliyokuahidi.Mungu Pekee ndie hutekeleza kwa Asilimia zote.
 
...

Tusidanganyane, hakuna mtu anayeweza kusema wananchi wangu wanataka kitu fulani na akawa sahihi.....hawa watu wamechaguliwa watumie judgement yao na uzoefu wao wa kutoka katika maeneo wanayoishi wananchi, lakini kusema wanawakilisha mawazo ya wananchi (kwa maana hiyo literally) ni kuongea kitu ambacho ni theory tu lakini kisicho na uhalisia ! After all hawa wabunge hawakuchaguliwa ili waandike katiba, walichaguliwa watunge sheria kwenye Bunge, ila wakajiconvert wenyewe wakawa wajumbe wa bunge la katiba !

Nakubaliana na wewe kabisa kuwa binafsi sikuwahi kuona wala kusikia mbunge au mwakilishi akikusanya maoni ila hapo kwenye RED ndipo penye swali, je kama mbunge hajaitisha mkutano si anao uzoefu wa wananchi wake wanataka nini? na kama anjua na akaenda kinyuma sisi tutajuaje kwamba katuwakilisha vibya ili tumwajibishe?
 
wewe mwenyewe unajikanyaga umeshasema hawa CCM wanalazimishwa kufuata msimamo wa chama na sio wananchi na maoni ya wananchi ili kukiokoa chama., sasa bas hiyo ni sababu tosha kura iwe ya siri ili haki iliyo katika nafsi zao iweze kupatikana kwa maslahi ya taifa na wawo wawe salama wakitoka hapo bungeni
Labda hukunielewa nimesema wawakilishi rasmi wa vya walioteuliwa kuwakilisha vyama vya siasa,lazima wasimamie msimamo wa vyama vilivyowatuma hata kama wao binafsi hawataki, na wakikiuka sharti wawajibishwe bila huruma,maana kura sio zao binafsi ila ni za wale waliowatuma. Nikasema hata wabunge kura ni za wananchi wao si zao binfsi au vyama vyao.
 
Mimi nakuunga mkono kabisa majibu yako bwana Nguvu ya Hoja, naona mawazo yetu yanashabihiana kwa kiasi kikubwa mzee!
 
Binafsi nitapiga kura ya wazi ndiyo ninayoipenda siyo vinginevyo kura ya siri ni unafiki mtupu.
 
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ilisainiwa kwa waasisi kujifunguia ndani wakayapora maoni ya wananchi wakaamua kwa Ubabe na sasa ZAIDI ya miaka 50 tunashuhudia Baadhi ya wajumbe wa Bunge maalam kupitia kamati ya kanuni kuturudisha kulekule kwa Waasisi, MAONI yangu ni haya tunahitaji Mjadala wa Wazi na Kura ya siri, Hii dhana kuwa waandishi wa habari hawana uwezo wa kuchuja na kufahamu nini au kipi ni habari ni dhana inayo wadharirisha Waandishi wa habari nchini na Kudharirisha taasisi zote nchini zinazotoa mafunzo ya Uandishi wa Habari, ninavyofahamu mimi kuna Waandishi wa habari wamesoma vyuo au taaasisi zile zile walizo soma Mainginia, Wanasheria, Walimu n.k sasa hii dhana sijui kwa kweli imetoka wapi huu ni Upuuzi usioweza kufumbiwa macho, LAZIMA UKEMEWE WAZI WAZI, Naungana na waandishi wa habari tuende Dodoma Wajumbe watueleze endapo Vikakao vya Kamati vimegeuka kuwa cc ya vyama vya siasa hasa...., kikao cha ukoo, au kikao cha baraza la Kanisa au Msikiti, Tunahitaji uwazi katika mchakato huu, mf Mjumbe mmoja wa kamati anatoa mfano kwamba itakuweje wajumbe wakikunjana, huyu amenichefua zaidi ina maana Wakunjaji, watoboa macho, wang'oa meno, wanaoswitch off majogoo, tayari wameshapangwa kwa kazi hiyo Dodoma???????? Tunahitaji kufahamu kila hatua ya mchakato huu Mwenyezi Mungu aliye iweka Tanganyika na Zanzibar hatoruhusu mjumbe yeyoyote au wakala yeyote Alete mchezo dhidi ya Watu wake, Pesa zilizotumika zilikuwa zinahitajika sana kwenye Huduma za Afya, Elimu, Miundombinu, Maji, n.k
 
Hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ilisainiwa kwa waasisi kujifunguia ndani wakayapora maoni ya wananchi wakaamua kwa Ubabe na sasa ZAIDI ya miaka 50 tunashuhudia Baadhi ya wajumbe wa Bunge maalam kupitia kamati ya kanuni kuturudisha kulekule kwa Waasisi, MAONI yangu ni haya tunahitaji Mjadala wa Wazi na Kura ya siri, Hii dhana kuwa waandishi wa habari hawana uwezo wa kuchuja na kufahamu nini au kipi ni habari ni dhana inayo wadharirisha Waandishi wa habari nchini na Kudharirisha taasisi zote nchini zinazotoa mafunzo ya Uandishi wa Habari, ninavyofahamu mimi kuna Waandishi wa habari wamesoma vyuo au taaasisi zile zile walizo soma Mainginia, Wanasheria, Walimu n.k sasa hii dhana sijui kwa kweli imetoka wapi huu ni Upuuzi usioweza kufumbiwa macho, LAZIMA UKEMEWE WAZI WAZI, Naungana na waandishi wa habari tuende Dodoma Wajumbe watueleze endapo Vikakao vya Kamati vimegeuka kuwa cc ya vyama vya siasa hasa...., kikao cha ukoo, au kikao cha baraza la Kanisa au Msikiti, Tunahitaji uwazi katika mchakato huu, mf Mjumbe mmoja wa kamati anatoa mfano kwamba itakuweje wajumbe wakikunjana, huyu amenichefua zaidi ina maana Wakunjaji, watoboa macho, wang'oa meno, wanaoswitch off majogoo, tayari wameshapangwa kwa kazi hiyo Dodoma???????? Tunahitaji kufahamu kila hatua ya mchakato huu Mwenyezi Mungu aliye iweka Tanganyika na Zanzibar hatoruhusu mjumbe yeyoyote au wakala yeyote Alete mchezo dhidi ya Watu wake, Pesa zilizotumika zilikuwa zinahitajika sana kwenye Huduma za Afya, Elimu, Miundombinu, Maji, n.k
 
Nimefuatilia sana malumbano yanayoendelea kwenye bunge maalum la Katiba kuhusu mambo mbalimbali,kama akidi,jinsi ya upigaji kura na mengine. Kwa leo nijadili kidogo tu kuhusu kura ya WAZI na SIRI.
Kwa namna yoyote ile kura ya WAZi ndio sahihi kutumika kwa sababu wajumbe ni wawakilishi wa watu wengine kwa hiyo hawapigi kura kwa dhamira zao binafsi ila kwa mujibu wa wale wanaowawakilisha. Kama mjumbe ametokana na jimbo la uchaguzi lazima apige kura kulingana na wananchi wake wanavyotaka hata kama yeye binafsi hapendi na lazima watu wake wajue kama mwakilishi wao amewawakilisha vilivyo na akienda kinyume na matakwa ya wananchi wake inabidi wananchi wamwajibishe moja kwa moja na wala sio chama chake. Kwa wale wanaowakilisha vyama vya siasa ambao ni kama 42 hivi kila mmoja anatakiwa kupiga kura ya wazi kulingana na msimamo wa chama chake na akienda tofauti anastahili kuwajibishwa bila huruma kwani kura si ya kwake binafsi bali ni ya wale waliomtuma,kwa hiyo anawajibika kupigia kura msimamao wa waliomtuma hata kama yeye binafsi hakubaliani nao. Vivyo hivyo wabunge wa viti maalum wanawajibika kwa wanawake waliowapeleka huko na si vyama vyao, utaratibu ni huo huo kwa wale wa makundi maalum wanawajibika kupiga kura kwa matakwa ya waliowawakilisha na si kwa matakwa yao binafsi.
Watu wengi kwa sasa wanaogopa kura ya wazi kwa hofu kwamba watabanwa na misimamo ya vyama vyao,huu ni "uhuni" chama kinatakiwa kuwabana wawakilishi wao rasmi tu, ambao ni kama wawili watatu kwa kila chama wengineo wanabanwa na wale wanaowawakilisha,na kama mwakilishi rasmi wa chama akienda tofauti na msimamo wa chama huyo lazima awajibishwe ila sio mwanachama wa chama fulani anawakilisha wananchi wake hata wasio na vyama alazimike kufuata matakwa au msimamo wa chama chake.
Kwa mawazo hayo kama itapigwa kura ya siri wanachi watajuaje kama matakwa yao na si matakwa binafsi ya mwakilishi wao yamezingatiwa? Hebu tutafakari pamoja kwa nguvu ya hoja...
Hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ilisainiwa kwa waasisi kujifunguia ndani wakayapora maoni ya wananchi wakaamua kwa Ubabe na sasa ZAIDI ya miaka 50 tunashuhudia Baadhi ya wajumbe wa Bunge maalam kupitia kamati ya kanuni kuturudisha kulekule kwa Waasisi, MAONI yangu ni haya tunahitaji Mjadala wa Wazi na Kura ya siri, Hii dhana kuwa waandishi wa habari hawana uwezo wa kuchuja na kufahamu nini au kipi ni habari ni dhana inayo wadharirisha Waandishi wa habari nchini na Kudharirisha taasisi zote nchini zinazotoa mafunzo ya Uandishi wa Habari, ninavyofahamu mimi kuna Waandishi wa habari wamesoma vyuo au taaasisi zile zile walizo soma Mainginia, Wanasheria, Walimu n.k sasa hii dhana sijui kwa kweli imetoka wapi huu ni Upuuzi usioweza kufumbiwa macho, LAZIMA UKEMEWE WAZI WAZI, Naungana na waandishi wa habari tuende Dodoma Wajumbe watueleze endapo Vikakao vya Kamati vimegeuka kuwa cc ya vyama vya siasa hasa...., kikao cha ukoo, au kikao cha baraza la Kanisa au Msikiti, Tunahitaji uwazi katika mchakato huu, mf Mjumbe mmoja wa kamati anatoa mfano kwamba itakuweje wajumbe wakikunjana, huyu amenichefua zaidi ina maana Wakunjaji, watoboa macho, wang'oa meno, wanaoswitch off majogoo, tayari wameshapangwa kwa kazi hiyo Dodoma???????? Tunahitaji kufahamu kila hatua ya mchakato huu Mwenyezi Mungu aliye iweka Tanganyika na Zanzibar hatoruhusu mjumbe yeyoyote au wakala yeyote Alete mchezo dhidi ya Watu wake, Pesa zilizotumika zilikuwa zinahitajika sana kwenye Huduma za Afya, Elimu, Miundombinu, Maji, n.k
 
Hakuna mtu aliyeuliza wapigakura waliomchagua. Na wengine wameteuliwa na rais. Kura ya siri ndio kura. Raais wabunge madiwani mabalozi na hata kura za kumchagua class monitor huwa ni za siri. Kama hawatafanya tunavyotaka sisi watanganyika tanganyika yetu basi kwenye kura ya kuipitisha tutaikataa.
 
Mambo hadharani ndio mpango mzima kuepuka wanafiki lakini...
 
Mimi sikubaliani na wewe kabisa !

Hili jambo la kura ya siri au wazi halipo kisheria. Kura ya siri au wazi zote zinakubalika kidemokrasia, kinachobaki ni busara tu ya kutumia aina gani ya kura kulingana na mazingira na kitu kinachoamuliwa. Tunategemea wajumbe watatumia busara ambazo tunaamini wanazo kujadiliana na kutoa maamuzi sahihi. Whether watapiga kura ya siri ya wazi cha muhimu ni maamuzi sahihi !. Ukiambiwa uchague maamuzi sahihi au uwazi (in case huwezi kuvipata vyote kwa pamoja) nadhani kama una busara utachagua maamuzi sahihi. Na kama baadhi ya wajumbe wanasema hawataweza kufanya maamuzi sahihi kama kura itakuwa ya wazi inabidi ku-wa-accomodate kwani tusipofanya hivyo definetely maamuzi yao yatakuwa sio sahihi wakati hayo haswa ndio tunayoyahitaji.

Vile vile mimi siikubali hii dhana iliyoenea kwamba hawa wabunge wameongea na wananchi wao na hapo walipo wamebeba mawazo ya wananchi wao ! Huo ni uongo wa mchana kweupe kabisa ! Hebu mkuu naomba unieleze mbunge mmoja tu....si zaidi ya hapo...MMOJA TU, ambaye alikutana na wananchi wake akakusanya maoni yao !. Hata kama itakuwa ni wachache lakini lazima kuwe na process ya hao wananchi kushiriki kwenye mjadala, hata kama watatofautiana hapa na pale lakini mwishoni wakakubaliana kwa hoja ambazo wakasema, hizi mbunge wetu nenda katusemee....HAKUNA hata mmoja aliyefanya hivyo ! Sana sana itakuwa ni watu wawili walio karibu naye wakiwemo family members, au marafiki zake au watu wawili watatu anaoweza kukutana nao..basi !. Kivipi maoni ya aina hiyo yanakuwa maoni ya wananchi wa jimbo lake ?

Tusidanganyane, hakuna mtu anayeweza kusema wananchi wangu wanataka kitu fulani na akawa sahihi.....hawa watu wamechaguliwa watumie judgement yao na uzoefu wao wa kutoka katika maeneo wanayoishi wananchi, lakini kusema wanawakilisha mawazo ya wananchi (kwa maana hiyo literally) ni kuongea kitu ambacho ni theory tu lakini kisicho na uhalisia ! After all hawa wabunge hawakuchaguliwa ili waandike katiba, walichaguliwa watunge sheria kwenye Bunge, ila wakajiconvert wenyewe wakawa wajumbe wa bunge la katiba !
Nakuunga mkono. Na hasa hii ya hao wabunge wanaposimama huko Dodoma wakidai wanawakilisha mawazo ya wananchi wao, ambao wengine wana zaidi ya mwaka hawajakutana nao. Angalau nimemwona Mh Mnyika akihamasisha watu wake wampe maoni jimboni kwake na hata nje ya jimbo lake. Ameweka hata rasmu ya kanuni kwenye blog yake na kuomba maoni. Lakini hii haimaanishi atakayoyaongea ni ya wananchi wake.

Kubwa la kukumbuka ni kuwa unapoteuliwa kuwa mwakilishi wa wananchi au kiongozi, unatakiwa uongozi na kuuwakilisha kwa hekima, siyo kama kaduku. Na ili linaweza kutenda vyama tu kwa kuongozwa na dhamira yako njema bila ya shuruti ya kimakundi au kibinafsi. Na hapa ndiyo kura ya Siri inapohitajika na hasa katika mfumo wetu tulio nao sasa.
 
Hakuna mtu aliyeuliza wapigakura waliomchagua. Na wengine wameteuliwa na rais. Kura ya siri ndio kura. Raais wabunge madiwani mabalozi na hata kura za kumchagua class monitor huwa ni za siri. Kama hawatafanya tunavyotaka sisi watanganyika tanganyika yetu basi kwenye kura ya kuipitisha tutaikataa.

Nakubaliana na wewe kabisa kuwa huenda hakuna mjumbe aliyeuliza wapigakura ila ni lazima anajua watu wake wanataka nini na kama hajui basi atapiga kura kinyume na matakwa yao na kwa vile kura itakuwa wazi hapo ndio pa kumwajibisha,pia tofautisha kura ya kumchagua rais na na hii tunayoiongelea,kwani ile ya rais ni matakwa ya mpiga kura binafsi hii ya sasa ni matakwa ya waliokutuma hata kama wewe binafsi hukubaliani nao. Kuhusu wajumbe walioteuliwa na Rais hao ni wawakilishi wa makundi maalum na wanawakilisha misimamo ya makundi yao na sio wao binfsi.
 
Mkuu, binafsi siamini kama suala hili la kura ya Siri ni la CCM. Kuna wana ccm wengi ambao wameweka msimamo wa kutopenda kura ya wazi. Pia kuna wana ccm wengi ambao hawapendi muundo wa serikali mbili. Hivyo, ingawa taasisi imetoa uamuzi huo, ila ndani yake kila mtu anawaza la kwake

Unachokiongea ndicho nisemacho. Wajumbe wengi wa CCM wamekengeuka. Wanachokitaka siyo msimamo wa chama, ndiyo maana wale mavuvuzela wamepewa kazi ya kupigania kura ya wazi ili wawadhoofishe hao walio kinyume na msimamo wa chama chao kwani ni wale majasiri tu walio tayari kwa lolote ndiyo watakaoobyesha misimamo yao katika uwazi. Na kwa ccm watu wa aina hiyo ni wachache kama nini.
 
Nimefuatilia sana malumbano yanayoendelea kwenye bunge maalum la Katiba kuhusu mambo mbalimbali,kama akidi,jinsi ya upigaji kura na mengine. Kwa leo nijadili kidogo tu kuhusu kura ya WAZI na SIRI.
Kwa namna yoyote ile kura ya WAZi ndio sahihi kutumika kwa sababu wajumbe ni wawakilishi wa watu wengine kwa hiyo hawapigi kura kwa dhamira zao binafsi ila kwa mujibu wa wale wanaowawakilisha. Kama mjumbe ametokana na jimbo la uchaguzi lazima apige kura kulingana na wananchi wake wanavyotaka hata kama yeye binafsi hapendi na lazima watu wake wajue kama mwakilishi wao amewawakilisha vilivyo na akienda kinyume na matakwa ya wananchi wake inabidi wananchi wamwajibishe moja kwa moja na wala sio chama chake. Kwa wale wanaowakilisha vyama vya siasa ambao ni kama 42 hivi kila mmoja anatakiwa kupiga kura ya wazi kulingana na msimamo wa chama chake na akienda tofauti anastahili kuwajibishwa bila huruma kwani kura si ya kwake binafsi bali ni ya wale waliomtuma,kwa hiyo anawajibika kupigia kura msimamao wa waliomtuma hata kama yeye binafsi hakubaliani nao. Vivyo hivyo wabunge wa viti maalum wanawajibika kwa wanawake waliowapeleka huko na si vyama vyao, utaratibu ni huo huo kwa wale wa makundi maalum wanawajibika kupiga kura kwa matakwa ya waliowawakilisha na si kwa matakwa yao binafsi.
Watu wengi kwa sasa wanaogopa kura ya wazi kwa hofu kwamba watabanwa na misimamo ya vyama vyao,huu ni "uhuni" chama kinatakiwa kuwabana wawakilishi wao rasmi tu, ambao ni kama wawili watatu kwa kila chama wengineo wanabanwa na wale wanaowawakilisha,na kama mwakilishi rasmi wa chama akienda tofauti na msimamo wa chama huyo lazima awajibishwe ila sio mwanachama wa chama fulani anawakilisha wananchi wake hata wasio na vyama alazimike kufuata matakwa au msimamo wa chama chake.
Kwa mawazo hayo kama itapigwa kura ya siri wanachi watajuaje kama matakwa yao na si matakwa binafsi ya mwakilishi wao yamezingatiwa? Hebu tutafakari pamoja kwa nguvu ya hoja...

Hapo penye RED unasema wananchi wamwajibishe kwa kutumia kipengere gani cha sheria? Katiba yenyewe yenye kipengere hicho ndo hiyo mnahihujumu ili wananchi tusiwe na sauti juu ya wale tuliowachagua,
Je ni majimbo mangapi wananchi hawana raha na wabunge wao lkn hawana mamlaka ya kuwawajibisha.
kama hujui mfano ni jimbo la segerea DSM,lkn kwa kuwa hakuna kipengere cha kumwajibisha mbunge inabidi msubiri uchaguzi ujao.
Jingine ni je wateule wa rais nani atawawajibisha ikiwa watafuata matakwa ya rais(m/kiti wa ccm) ambaye ndiye kawateua
na hivyo wakaogopa kumuudhi kwa sababu anawaona jinsi wanavyopiga kura,
Ukweli mimi naona kila anayepigia debe kura ya wazi ana maslahi binafsi au hajui lolote anafuata mkumbo wa watawala
wanataka nini na si yeye mwenyewe, na huu ndo nauita unafiki wa watanzania,na tutajuta kwa unafiki huu.
 
Nimefuatilia sana malumbano yanayoendelea kwenye bunge maalum la Katiba kuhusu mambo mbalimbali,kama akidi,jinsi ya upigaji kura na mengine. Kwa leo nijadili kidogo tu kuhusu kura ya WAZI na SIRI.

Kwa namna yoyote ile kura ya WAZi ndio sahihi kutumika kwa sababu wajumbe ni wawakilishi wa watu wengine kwa hiyo hawapigi kura kwa dhamira zao binafsi ila kwa mujibu wa wale wanaowawakilisha. Kama mjumbe ametokana na jimbo la uchaguzi lazima apige kura kulingana na wananchi wake wanavyotaka hata kama yeye binafsi hapendi na lazima watu wake wajue kama mwakilishi wao amewawakilisha vilivyo na akienda kinyume na matakwa ya wananchi wake inabidi wananchi wamwajibishe moja kwa moja na wala sio chama chake.

Kwa wale wanaowakilisha vyama vya siasa ambao ni kama 42 hivi kila mmoja anatakiwa kupiga kura ya wazi kulingana na msimamo wa chama chake na akienda tofauti anastahili kuwajibishwa bila huruma kwani kura si ya kwake binafsi bali ni ya wale waliomtuma,kwa hiyo anawajibika kupigia kura msimamao wa waliomtuma hata kama yeye binafsi hakubaliani nao. Vivyo hivyo wabunge wa viti maalum wanawajibika kwa wanawake waliowapeleka huko na si vyama vyao, utaratibu ni huo huo kwa wale wa makundi maalum wanawajibika kupiga kura kwa matakwa ya waliowawakilisha na si kwa matakwa yao binafsi.

Watu wengi kwa sasa wanaogopa kura ya wazi kwa hofu kwamba watabanwa na misimamo ya vyama vyao,huu ni "uhuni" chama kinatakiwa kuwabana wawakilishi wao rasmi tu, ambao ni kama wawili watatu kwa kila chama wengineo wanabanwa na wale wanaowawakilisha,na kama mwakilishi rasmi wa chama akienda tofauti na msimamo wa chama huyo lazima awajibishwe ila sio mwanachama wa chama fulani anawakilisha wananchi wake hata wasio na vyama alazimike kufuata matakwa au msimamo wa chama chake.

Kwa mawazo hayo kama itapigwa kura ya siri wanachi watajuaje kama matakwa yao na si matakwa binafsi ya mwakilishi wao yamezingatiwa? Hebu tutafakari pamoja kwa nguvu ya hoja...

...........:help: Ninajuta kupita hapa kukutana na madudu kama haya :target:
 
Back
Top Bottom