kaangwa
JF-Expert Member
- Jan 30, 2011
- 644
- 193
Mara nyingi nimesikia watu wakisema wabunge wa bunge hili ni watu wazima ,na rais kachagua wanasiasa wa zamani
na wasomi kwa misingi ya hekima zao na kama ni wabunge wa majimbo tayari waliishachaguliwa na wananchi wao
na wale wa makundi maalum wametumwa na makundi hayo kwa kuamini kwamba watawawakilisha vema
sasa huu woga wa kusema tunataka kura ya wazi ili tuone wanachokifanya unatoka wapi?
Hii inanipa maswali kama vile,wamewekwa kwa makusudi na hivyo aliyewaweka ana wasiwasi kwamba wanaweza mtosa endapo hawatafanya kwa wazi, hivyo anataka uwazi ili aweze kuwabana au hatuna uhakika na uwezo wao wa kimaamuzi maana wamezoeshwa kuendeshwa kama roboti.Vinginevyo tuamini kwamba watafanya maamuzi kama tulivyowaamini.
Kama hoja ni kuwaona wakituwakilisha,Kura ya wazi itawanufaisha waliomijini ni asilimia ndogo huku asilimia kubwa ya watanzania ipo vijijini ambako hakuna umeme na sehemu zenye umeme ni wachache wenye vingamzi kuona runinga
Hivyo dhana hii ya uwazi naona imewalenga wenye maslahi binafsi wanaoishi mijini ili kufanikisha malengo yao.