Wito kwa Bunge la Katiba: Kura iwe ya Siri kwasababu Hakuna aliyetumwa na Watu Kuwawakilisha!

Wito kwa Bunge la Katiba: Kura iwe ya Siri kwasababu Hakuna aliyetumwa na Watu Kuwawakilisha!

Nimefuatilia sana malumbano yanayoendelea kwenye bunge maalum la Katiba kuhusu mambo mbalimbali,kama akidi,jinsi ya upigaji kura na mengine. Kwa leo nijadili kidogo tu kuhusu kura ya WAZI na SIRI.

Kwa namna yoyote ile kura ya WAZi ndio sahihi kutumika kwa sababu wajumbe ni wawakilishi wa watu wengine kwa hiyo hawapigi kura kwa dhamira zao binafsi ila kwa mujibu wa wale wanaowawakilisha. Kama mjumbe ametokana na jimbo la uchaguzi lazima apige kura kulingana na wananchi wake wanavyotaka hata kama yeye binafsi hapendi na lazima watu wake wajue kama mwakilishi wao amewawakilisha vilivyo na akienda kinyume na matakwa ya wananchi wake inabidi wananchi wamwajibishe moja kwa moja na wala sio chama chake.

Kwa wale wanaowakilisha vyama vya siasa ambao ni kama 42 hivi kila mmoja anatakiwa kupiga kura ya wazi kulingana na msimamo wa chama chake na akienda tofauti anastahili kuwajibishwa bila huruma kwani kura si ya kwake binafsi bali ni ya wale waliomtuma,kwa hiyo anawajibika kupigia kura msimamao wa waliomtuma hata kama yeye binafsi hakubaliani nao. Vivyo hivyo wabunge wa viti maalum wanawajibika kwa wanawake waliowapeleka huko na si vyama vyao, utaratibu ni huo huo kwa wale wa makundi maalum wanawajibika kupiga kura kwa matakwa ya waliowawakilisha na si kwa matakwa yao binafsi.

Watu wengi kwa sasa wanaogopa kura ya wazi kwa hofu kwamba watabanwa na misimamo ya vyama vyao,huu ni "uhuni" chama kinatakiwa kuwabana wawakilishi wao rasmi tu, ambao ni kama wawili watatu kwa kila chama wengineo wanabanwa na wale wanaowawakilisha,na kama mwakilishi rasmi wa chama akienda tofauti na msimamo wa chama huyo lazima awajibishwe ila sio mwanachama wa chama fulani anawakilisha wananchi wake hata wasio na vyama alazimike kufuata matakwa au msimamo wa chama chake.

Kwa mawazo hayo kama itapigwa kura ya siri wanachi watajuaje kama matakwa yao na si matakwa binafsi ya mwakilishi wao yamezingatiwa? Hebu tutafakari pamoja kwa nguvu ya hoja...
 
Mfano ni kama Prof.Safari analazimika kufuata msimamo wa CHADEMA hata kama yeye binfsi hakubaliani nao maana yeye ni mwakilishi rasmi wa CDM ila sio F.Mbowe, huyu analazimika kufuata matakwa ya wananchi wake wa Hai hata kama yeye binafsi hakubaliani nayo. Na kwenye kura ya wazi atapigia matakwa ya wananchi wake na sio msimamo wa chama chake maana anawajibika kwa wananchi moja kwa moja.
 
Unachokifanya hapa ni kuongeza UJINGA tumeshuhudia CCM wakitoa vitisho kwa wale wanaopingana na mapendekezo ya CCM na hadi sasa kuna orodha ya wabunge 90 ambayo yameorodheshwa kwani wanaonekana kupingana na kauli ya CCM. Kama CCM wasingeingilia mchakato wa Katiba na kuwaacha Wabunge watoe mapandekezo na maoni yao binafsi hiki ulichokiandika ni sahihi lakini kwa hali ilivyo hakiwezekani na kama kura itakuwa ni ya wazi hatutapata KATIBA tunayoitaka bali itakuwa ni KATIBA kupitia matakwa ya CCM na sio wananchi wote kwa ujumla wetu.
 
nimesoma nikaishia njiani nikachoka ngoja nitafakari nimalizie kusoma thread yako au niache
 
Mfano ni kama Prof.Safari analazimika kufuata msimamo wa CHADEMA hata kama yeye binfsi hakubaliani nao maana yeye ni mwakilishi rasmi wa CDM ila sio F.Mbowe, huyu analazimika kufuata matakwa ya wananchi wake wa Hai hata kama yeye binafsi hakubaliani nayo. Na kwenye kura ya wazi atapigia matakwa ya wananchi wake na sio msimamo wa chama chake maana anawajibika kwa wananchi moja kwa moja.

Hata kama ni mfano, je umeishawahi kusikia viongozi wa CHADEMA wakitoa vitisho kwa wajumbe wao juu ya hili?tatizo hapa ni CCM kwani kauli zao zimejionyesha wazi kuanzia mwenyekiti wao na wale viongozi wengine. na labda kwa nyongeza nikuulize katika mwendelezo wa vikao hivi je kuna chama chochote kingine kiliingiza rasimu katiba ya mapendekezo yake ndani ya kikao cha Bunge hili maalum tofauti na CCM?
 
Unachokifanya hapa ni kuongeza UJINGA tumeshuhudia CCM wakitoa vitisho kwa wale wanaopingana na mapendekezo ya CCM na hadi sasa kuna orodha ya wabunge 90 ambayo yameorodheshwa kwani wanaonekana kupingana na kauli ya CCM. Kama CCM wasingeingilia mchakato wa Katiba na kuwaacha Wabunge watoe mapandekezo na maoni yao binafsi hiki ulichokiandika ni sahihi lakini kwa hali ilivyo hakiwezekani na kama kura itakuwa ni ya wazi hatutapata KATIBA tunayoitaka bali itakuwa ni KATIBA kupitia matakwa ya CCM na sio wananchi wote kwa ujumla wetu.

Kwa mfano hao wabunge 90 waamue kupigia kura matakwa ya wananchi wao ambayo si lazima yaendane na msimamo wa chama chao wewe unadhani kuna madhara gani kwa wabunge na wananchi waliowatuma?
 
Ww ni moja waliotumwa na ccm, unafikiri hatujui wajumbe wa ccm wameambiwa wapige kura za sawaz ili yeyote atakaekuwa tofaut na chama chao awajibishwe!! Kusudio la ccm na unjanya wa kizaman ndo huo, imefikia hatuja hata wanapitisha vifungu visivyokuwa na maana kama hiki cha kuzuia waandishi wa habar kutokuingia,
Kura ya siri ni lazima ili kumpa uhuru mpiga kuwa apige kura anayemtaka!!
 
Hata kama ni mfano, je umeishawahi kusikia viongozi wa CHADEMA wakitoa vitisho kwa wajumbe wao juu ya hili?tatizo hapa ni CCM kwani kauli zao zimejionyesha wazi kuanzia mwenyekiti wao na wale viongozi wengine. na labda kwa nyongeza nikuulize katika mwendelezo wa vikao hivi je kuna chama chochote kingine kiliingiza rasimu katiba ya mapendekezo yake ndani ya kikao cha Bunge hili maalum tofauti na CCM?

Kuhusu vitisho siwezi kulisemea sana maana hao CCM wamekanusha hilo kupitia kwa Nape kwenye gazeti la leo la Mwananchi, swali, je kama kura itakuwa ya siri huoni wajumbe watapiga kura kwa matakwa yao binafsi na si matakwa ya wanaowawakilisha?
 
Kwa mfano hao wabunge 90 waamue kupigia kura matakwa ya wananchi wao ambayo si lazima yaendane na msimamo wa chama chao wewe unadhani kuna madhara gani kwa wabunge na wananchi waliowatuma?
Muulize Furikunjombe na Nkono ni nini kiliwakuta hadi sasa hivi hawapo upande wa wananchi wamebaki na amri za CCM.
 
Ukweli ni kwamba hakuna Mbunge hata Mmoja aliyepita Jimboni kwake kuwauliza wanataka waseme nini kwenye Bunge la Katiba.Waliopita ni Tume ya Warioba na waliambiwa na Wananchi wengi kwamba wanataka Serikali tatu.
Cha Msingi ni kwamba walishaaminiwa na wananchi ndio maana wakapewa Ubunge,Swala la Upigaji kura za Wazi ni Kuwalaghai Wananchi.
Mbona wanalipwa 300,000/= na Wanataka kuongezewa zaidi kama kweli wanawajali wananchi?.Mbunge anayejali Matakwa ya Wananchi hawezi kupokea Tshs.300,000/= kwa siku wakati Kima cha chini ni Tshs.180,000/= kwa Mwezi.Hakuna Mbunge hata Mmoja aliyetumwa kudai Posho nono kama hiyo.
Tuache unafiki,Kura ya Wazi ina Malengo ya Kudhibiti Wabunge wa CCM wanaotaka uwepo wa Serikali tatu.
Siku zote kura Zinazotoa Uhuru wa Mpigaji kura ni za Siri.
 
Kuhusu vitisho siwezi kulisemea sana maana hao CCM wamekanusha hilo kupitia kwa Nape kwenye gazeti la leo la Mwananchi, swali, je kama kura itakuwa ya siri huoni wajumbe watapiga kura kwa matakwa yao binafsi na si matakwa ya wanaowawakilisha?

Nimeeleza wazi kura ya wazi ingekuwa nzuri kama CCM wasingeingilia huu mchakato wa KATIBA lakini kwa kuwa wameingilia ni vema kura ikawa ya Siri ili wajumbe ambao ni wanaCCM wakapiga kura kwa uhuru pasipo woga wowote.
 
Ww ni moja waliotumwa na ccm, unafikiri hatujui wajumbe wa ccm wameambiwa wapige kura za sawaz ili yeyote atakaekuwa tofaut na chama chao awajibishwe!! Kusudio la ccm na unjanya wa kizaman ndo huo, imefikia hatuja hata wanapitisha vifungu visivyokuwa na maana kama hiki cha kuzuia waandishi wa habar kutokuingia,
Kura ya siri ni lazima ili kumpa uhuru mpiga kuwa apige kura anayemtaka!!

Hapo penye RED hasa ndio kwenye swali langu,hii kura ni ya mjumbe binafsi au ni ya wale anowawakilisha hata kama yeye biafsi hakubaliani nao? Namaaninsha wananchi wajimbo husika kwa wabunge na wawakilishi .
 
Mkuu mimi naona hoja zako si za msingi katika kutetea kura ya Wazi hasa katika mazingira yaliyopo kwenye bunge maalum kwa sasa. Soma vizuri nguzo kuu za Demokrasia utakuta kura ya siri (secret ballot) ni nguzo mojawapo ya demokrasia. Kwa sababu kama unatetea hiyo kura ya siri ukumbuke ni CCM hao hao ambao tayari wameshapitisha Kanuni ya kuzuia Waandishi wa habari wasifuatilie yanayojadiliwa kwenye kamati ndogo ndogo za bunge maalumu. Lakini wakati huo huo wanataka kura ziwe za wazi na sio za siri. Hii maana yake nini? Ndio maana mimi nadhani ni vizuri mchakato (process) wa majadiliano ndio uwe wazi ili wananchi wajue ni kwa jinsi gani wawakilishi wao wanawasilisha maoni yao kwenye kamati za bunge maalumu? Harafu baada ya hapo kura hata ikiwa ya siri mimi sioni shida yoyote. Mchakato ndio uwe wazi na sio matokeo. Sasa km hawataki mchakato wenyewe uwe wazi harafu wanapigania kura ya siri, huko sio kujikanganya?

Mimi nafikiri kura ya wazi mnayoipigia debe ni dhahiri haina malengo mema kwa watanzania bali ni kwa ajili ya kutekeleza zaidi matakwa ya kisiasa. Wananchi tayari walishapaza sauti zao kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Kwa hiyo, wala haikutakiwa kuwe na ubishano mkubwa kiasi hicho kwa mambo ambayo yako wazi na wananchi wameshatoa sauti zao.

Kwa hiyo, mimi naona kuendelea kubishania swala la kura ya siri au ya wazi ni kupoteza tu muda na pia kupoteza malengo yaliyowapeleka kule. Huu ni uhuni kabisa kwani katiba inayotungwa sio ya chama, taasisi au kikundi fulani bali ni katiba ya nchi kwa ajili ya Wananchi wote. Vyama vyenyewe vinavong'a2nia kupitisha matakwa yao badala ya Wananchi vinatakiwa kutambua kuwa Watanzania tuko milioni 45 mpaka sasa, na katika hao vyama vyote vya siasa havina wanachama zaidi ya milioni 12. Kwa mantiki hiyo, sisi wananchi tusio na vyama ndio wengi zaidi kuliko wanachama wa vyama vya siasa. Kwa maoni yangu kura ya wazi ni uhuni wa CCM katika kupanga njama za kupitisha matakwa yao kwenye katiba na kuhujumu zoezi zima la katiba. Kama hawaamini kuwa ni maoni ya Wananchi si waache tu kama sio kweli ukifika wakati wa kupiga kura ya maoni, Wananchi si wataikataa katiba kuwa sio maoni yao? Kwa nini wanalazimisha?
 
...
Siku zote kura Zinazotoa Uhuru wa Mpigaji kura ni za Siri.

Kama kura itakuwa ya siri je mimi ninayewakilishwa nitajuaje mwakilishi wangu kama ameniwakilisha vilivyo au amejiwakilisha binafsi na matakwa ya familia yake, hapa nitamuwajibishaje bila ushahidi?
 
Mimi sikubaliani na wewe kabisa !

Hili jambo la kura ya siri au wazi halipo kisheria. Kura ya siri au wazi zote zinakubalika kidemokrasia, kinachobaki ni busara tu ya kutumia aina gani ya kura kulingana na mazingira na kitu kinachoamuliwa. Tunategemea wajumbe watatumia busara ambazo tunaamini wanazo kujadiliana na kutoa maamuzi sahihi. Whether watapiga kura ya siri ya wazi cha muhimu ni maamuzi sahihi !. Ukiambiwa uchague maamuzi sahihi au uwazi (in case huwezi kuvipata vyote kwa pamoja) nadhani kama una busara utachagua maamuzi sahihi. Na kama baadhi ya wajumbe wanasema hawataweza kufanya maamuzi sahihi kama kura itakuwa ya wazi inabidi ku-wa-accomodate kwani tusipofanya hivyo definetely maamuzi yao yatakuwa sio sahihi wakati hayo haswa ndio tunayoyahitaji.

Vile vile mimi siikubali hii dhana iliyoenea kwamba hawa wabunge wameongea na wananchi wao na hapo walipo wamebeba mawazo ya wananchi wao ! Huo ni uongo wa mchana kweupe kabisa ! Hebu mkuu naomba unieleze mbunge mmoja tu....si zaidi ya hapo...MMOJA TU, ambaye alikutana na wananchi wake akakusanya maoni yao !. Hata kama itakuwa ni wachache lakini lazima kuwe na process ya hao wananchi kushiriki kwenye mjadala, hata kama watatofautiana hapa na pale lakini mwishoni wakakubaliana kwa hoja ambazo wakasema, hizi mbunge wetu nenda katusemee....HAKUNA hata mmoja aliyefanya hivyo ! Sana sana itakuwa ni watu wawili walio karibu naye wakiwemo family members, au marafiki zake au watu wawili watatu anaoweza kukutana nao..basi !. Kivipi maoni ya aina hiyo yanakuwa maoni ya wananchi wa jimbo lake ?

Tusidanganyane, hakuna mtu anayeweza kusema wananchi wangu wanataka kitu fulani na akawa sahihi.....hawa watu wamechaguliwa watumie judgement yao na uzoefu wao wa kutoka katika maeneo wanayoishi wananchi, lakini kusema wanawakilisha mawazo ya wananchi (kwa maana hiyo literally) ni kuongea kitu ambacho ni theory tu lakini kisicho na uhalisia ! After all hawa wabunge hawakuchaguliwa ili waandike katiba, walichaguliwa watunge sheria kwenye Bunge, ila wakajiconvert wenyewe wakawa wajumbe wa bunge la katiba !

Nimefuatilia sana malumbano yanayoendelea kwenye bunge maalum la Katiba kuhusu mambo mbalimbali,kama akidi,jinsi ya upigaji kura na mengine. Kwa leo nijadili kidogo tu kuhusu kura ya WAZI na SIRI.
Kwa namna yoyote ile kura ya WAZi ndio sahihi kutumika kwa sababu wajumbe ni wawakilishi wa watu wengine kwa hiyo hawapigi kura kwa dhamira zao binafsi ila kwa mujibu wa wale wanaowawakilisha. Kama mjumbe ametokana na jimbo la uchaguzi lazima apige kura kulingana na wananchi wake wanavyotaka hata kama yeye binafsi hapendi na lazima watu wake wajue kama mwakilishi wao amewawakilisha vilivyo na akienda kinyume na matakwa ya wananchi wake inabidi wananchi wamwajibishe moja kwa moja na wala sio chama chake. Kwa wale wanaowakilisha vyama vya siasa ambao ni kama 42 hivi kila mmoja anatakiwa kupiga kura ya wazi kulingana na msimamo wa chama chake na akienda tofauti anastahili kuwajibishwa bila huruma kwani kura si ya kwake binafsi bali ni ya wale waliomtuma,kwa hiyo anawajibika kupigia kura msimamao wa waliomtuma hata kama yeye binafsi hakubaliani nao. Vivyo hivyo wabunge wa viti maalum wanawajibika kwa wanawake waliowapeleka huko na si vyama vyao, utaratibu ni huo huo kwa wale wa makundi maalum wanawajibika kupiga kura kwa matakwa ya waliowawakilisha na si kwa matakwa yao binafsi.
Watu wengi kwa sasa wanaogopa kura ya wazi kwa hofu kwamba watabanwa na misimamo ya vyama vyao,huu ni "uhuni" chama kinatakiwa kuwabana wawakilishi wao rasmi tu, ambao ni kama wawili watatu kwa kila chama wengineo wanabanwa na wale wanaowawakilisha,na kama mwakilishi rasmi wa chama akienda tofauti na msimamo wa chama huyo lazima awajibishwe ila sio mwanachama wa chama fulani anawakilisha wananchi wake hata wasio na vyama alazimike kufuata matakwa au msimamo wa chama chake.
Kwa mawazo hayo kama itapigwa kura ya siri wanachi watajuaje kama matakwa yao na si matakwa binafsi ya mwakilishi wao yamezingatiwa? Hebu tutafakari pamoja kwa nguvu ya hoja...
 
Swala la kujua kama mjumbe amekuwakilishaje hapo, halina mantiki sana kwa sababu sina uhakika nyie kama Wananchi wote mlikaa vikao na mbunge wenu mkampa maagizo ya vitu gani akatetee mle bungeni. Tunachokiona tu ni misimamo ya vyama hasa chama cha mapinduzi (CCM) ambao kama mnavyofahamu Wabunge wengi wa CCM walishaonekana kujali maslahi zaidi ya chama chao kuliko wapiga kura wao au wananchi. Hata sheria ya Mabadiliko ya Katiba mliona ilivyokuwa ikichakachuliwa na Wabunge wa CCM bungeni. Na mpk sasa sheria ile ni moja ya sheria mbaya sana kuwahi kupitishwa na bunge kama lile.

Kwa hiyo, tunachotaka sisi wale wajumbe ni watu wazima na wenye akili timamu. Binafsi naamini wakiwemo mle bungeni watasikiliza hoja zote za kwao na kinzani na kupima wao wenyewe hoja ipi ina mashiko au mantiki na kisha kufanya uamzi kwa kutumia utashi na uhuru wao binafsi bila kuingiliwa na misimamo ya vikundi, taasisi au vyama vyao hasa pale ambapo misimamo hiyo sio sahihi au hawaiungi mkono.

Kwa hiyo, hoja hapo sio swala la wewe kujua unawakilishwaje bungeni maana hata Wananchi hamkufanya vikao vyovyote na wajumbe au wabunge wenu. Aidha, bado hata kule majimboni wananchi wana mawazo na misimamo tofauti. Nafikiri swala la kuamua bado liko kwenye mjumbe mwenyewe binafsi. Hiyo, unayoisema mzee ni demokrasia tu bandia na ni ngumu kutekelezeka katika mazingira ya demokrasia ya uwakilishi (indirect demokracy)!
 
Nimefuatilia sana malumbano yanayoendelea kwenye bunge maalum la Katiba kuhusu mambo mbalimbali,kama akidi,jinsi ya upigaji kura na mengine. Kwa leo nijadili kidogo tu kuhusu kura ya WAZI na SIRI.
Kwa namna yoyote ile kura ya WAZi ndio sahihi kutumika kwa sababu wajumbe ni wawakilishi wa watu wengine kwa hiyo hawapigi kura kwa dhamira zao binafsi ila kwa mujibu wa wale wanaowawakilisha. Kama mjumbe ametokana na jimbo la uchaguzi lazima apige kura kulingana na wananchi wake wanavyotaka hata kama yeye binafsi hapendi na lazima watu wake wajue kama mwakilishi wao amewawakilisha vilivyo na akienda kinyume na matakwa ya wananchi wake inabidi wananchi wamwajibishe moja kwa moja na wala sio chama chake. Kwa wale wanaowakilisha vyama vya siasa ambao ni kama 42 hivi kila mmoja anatakiwa kupiga kura ya wazi kulingana na msimamo wa chama chake na akienda tofauti anastahili kuwajibishwa bila huruma kwani kura si ya kwake binafsi bali ni ya wale waliomtuma,kwa hiyo anawajibika kupigia kura msimamao wa waliomtuma hata kama yeye binafsi hakubaliani nao. Vivyo hivyo wabunge wa viti maalum wanawajibika kwa wanawake waliowapeleka huko na si vyama vyao, utaratibu ni huo huo kwa wale wa makundi maalum wanawajibika kupiga kura kwa matakwa ya waliowawakilisha na si kwa matakwa yao binafsi.
Watu wengi kwa sasa wanaogopa kura ya wazi kwa hofu kwamba watabanwa na misimamo ya vyama vyao,huu ni "uhuni" chama kinatakiwa kuwabana wawakilishi wao rasmi tu, ambao ni kama wawili watatu kwa kila chama wengineo wanabanwa na wale wanaowawakilisha,na kama mwakilishi rasmi wa chama akienda tofauti na msimamo wa chama huyo lazima awajibishwe ila sio mwanachama wa chama fulani anawakilisha wananchi wake hata wasio na vyama alazimike kufuata matakwa au msimamo wa chama chake.
Kwa mawazo hayo kama itapigwa kura ya siri wanachi watajuaje kama matakwa yao na si matakwa binafsi ya mwakilishi wao yamezingatiwa? Hebu tutafakari pamoja kwa nguvu ya hoja...

jibu lake ni rahis sana: kwasababu wamelazimika kufuata msimamo wa chama na siyo wananchi ndio tunasema iwe siri ili ile haki iliyo katika nafsi zao waweze kuitumia, kama kusingekuwa na vitisho basi wazi ni nzuri zaidi.,
 
Hakuna mwenye uwezo wa kuzuia kufufuka kwa TANGANYIKA ,WEWE PIGA KELELE LAKI TANGANYIKA NI LAZIMA .
 
Back
Top Bottom