Mchakato huu ni wa kitaifa, kwa maana unawagusa watanzania. Rasimu inayojadiliwa kinadharia inatokana na wao.
Wajumbe waliochaguliwa kuwawakilisha wanatokana na wao. Wangependa maoni na mawazo ya wajumbe wa bunge yatokane na wao.
Katika muktadha huo wangependa kuwa na democratic faith dhidi ya wajumbe wao. Democratic faith haijengwi kizani. Democratic faith haijengwi mafichoni bali hujengwa hadharani na mbele ya macho ya wengi. Kura iwe wazi. Hili ni moja.
Pili wanafalsafa wanasema binaadamu kwa asili yake ni mbinafsi. Ili kuepuka ubinafsi wa mwanadamu katika muktadha unaogusa maslahi ya wengi unatafutwa mfumo ambao uta neutralize matakwa binafsi ya mwanadamu na hatimaye tunamvisha kilemba cha matakwa ya wengi. Kura ya wazi ni kilemba sahihi.
Tatu, hoja inayotumika kuhalalisha kura ya wazi ni hoja nyepesi. Vitisho na hofu katika historia ya demokrasia duniani havijawahi kutumika kuwa nyenzo za kuhalalisha maamuzi yanayogusa maslahi ya Taifa. Hoja zinazotumika ni uwezo wa methodolojia katika kukidhi matakwa ya wengi lakini siyo hatari ya methodolojia kutoa mwanya kwa wawakilishi kutishwa na vyama vyao.
Kwa maana hiyo wanaohalalisha kura ya siri wamekosa msingi wa hoja yao.
Watu wanajaribu kuhalarisha mambo yao ya Siri kwa kutumia hoja nyepesi kwamba kura zote hupigwankwa siri. Wanashindwa kutofautisha kati ya kura ya kumchagua kiongozi na kura ya kupitisha hoja bungeni. Katika mifumo yote ya kibunge duniani utaratibu wa kupitisha hoja hufanywa kwa uwazi kwani unaenda sambamba na mjadala wa wabunge kuhusu hoja inayopitishwa.
Hata hivyo kiwango cha uwazi kiwe hivi.
Katika kupitisha kifungu kwa kifungu cha rasimu itumike kura ya wazi kwa sababu inagusa maeneo mahsusi ambayo kwa kiasi kikubwa kilemba cha matakwa ya wengi kinahitajika zaidi na wanye mchakato (watanzania) wangependa kuona ni jinsi gani matakwa yao yanawasilishwa.
Baada ya mchakato huo, katika kupitisha rasimu ya mwisho basi kura ya siri itumike kwani itakua tayari kila kipengele kimepitishwa katika mfumo wa wazi ambapo ubinafsi ulizikwa. Hivyo kama watavyofanya watanzania katika kura ya maoni basi ifanyike hivyo kuanzia bungeni kwa uwingi wa kura kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba.