Ningekuwa mimi, kwa hali ilivyo sasa, ningefanya press na waandishi wa habari wa kitaifa, kikanda na Kimataifa na kufanya yafuatayo:-
1. Kuwaachia wafungwa na mahabusu wote wa kesi zenye mwelekeo wa kisiasa.
2. Kupiga marufuku kali askari yeyote kuwabugudhi Watanzania na wanasiasa wa vyama vyote bila sababu za Msingi.
3. Ningetoa wiki mbili Watanzania waniseme kwa kiwango chochote kile na wasichukuliwe hatua yoyote ile, lengo likiwa ni kuwafanya wapumue na kutoa hasira zao juu yangu.
4. Ningepiga marufuku UCHAWA wa aina yoyote ile kuanzia Bungeni hadi mitaani.
5. Baada ya kufanya hayo hapo juu, ningeomba msamaha kwa Mungu na kwa Watanzania kutokana na hali ilivyo.
6. Ningewaita Commonwealth, AU, EAC nk. ili wasimamie maridhiano.
Naamini kwa kufanya hivyo nitakuwa:-
1. Nimerudisha imani kwa Watanzania na Jamii ya Kimataifa achilia mbali kwa Mungu wangu.
2. Nimepunguza sana chuki kati yangu na Watanzania na Jamii ya Kimataifa.
Kwa ujumla, ningefungua ukurasa mpya kabisa wa matumaini ambao Marais wote nyuma yangu hawajawahi kufanya.