Wito Kwa Viongozi Wetu: Unapokosea, hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge utamaduni wa kuwajibika ili kumuepushia Rais wetu kubeba mzigo wa karma

Wanabodi, kwenye issue za uwajibikaji, hoja za bandiko hili bado ziko valid.
P
 

Majaliwa anataka aondoke kwa kelele za kina Msukuma asubirie November 1, 2022.
 
Majaliwa anataka aondolewe kwa kelele nyingi kabisa. Mtu mzima akivuliwa nguo huchutama.
 
Kiongozi
kiongozi kama Waziri Mkuu hupaswi kuwa na makandokando ya kutajwa kwenye Rushwa.

Hii imekuwa ni mazoea na wakati wote hutishia watu na wengine huagiza waitwe ofisini kwake.

Alitajwa na mfanyabiashara wa Pembejeo feki kuwa ni zake.

Alitajwa kwenye uuzaji wa magogo yaliyozuiwa Tabora.

Alitajwa kwenye ulanguzi wa Biashara ya korosho na kingpin wa ka ng’ombe.
Alitajwa kwenye Biashara ya Magendo ya vitenge.

Kwanini anatajwa yeye tu…???
 
Mkuu MWALLA , Hiki ndicho nilichozungumzia hapa!.
P
 
Bandiko hili liko valid, kumhusu huyu kiongozi fulani mwingine wa serikali anayutuhumiwa kutumia gari la serikali kwenye mambo yake binafsi na kusababisha ajali.

Kama tuhuma hizi zina ukweli wowote, mhusika awajibike mwenyewe tuu na asisubiri kuwajibishwa!.
P
 
Watanzania kuwajibika ni shuguli

Ova
 
Mkuu Pascal mayalla heshma yako,maoni yako ni yapi ili kuweza kutibu swala zima la uadilifu na kuwajibika kwa viongozi wa umma?
Mkuu Emmanuel Mkwama , hili la uadilifu na uwajibikaji wa viongozi wa umma, niliisha shauri sana humu tangu kitambo mfano mzuri ni mabandiko haya matatu
  1. Wito Kwa Viongozi Wetu: Unapokosea, hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge utamaduni wa kuwajibika ili kumuepushia Rais wetu kubeba mzigo wa karma
  2. Viongozi wetu wanapofanya makosa ya wazi waishie tu kuomba msamaha kisha 'life as usual', au tujenge utamaduni wa kuwajibika kama enzi za Nyerere?
  3. TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!
Ukipata muda tembelea pia ujifunze jinsi awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere ilipokuwa very seriously na issues za uadilifu na uwajibikaji.

P
 
Hoja hii ndio imejibiwa leo
P
 
Wanabodi,
Naanzisha updates ya feedback ya baadhi ya mabadiliko yangu, nilishauri nini na hatimaye ushauri huo umesikilizwa?, umefanyiwa kazi?, na matokeo ya ushauri huo.

Huu ni ushauri wa siku nyingi, lakini hatimaye leo angalau umepata sikio la kuusikia na sasa unakwenda kufanyiwa kazi
“Sasa hivi tufumbe macho anayevurunda kazini akae pembeni, hakuna haja ya kumpoza kumpeleka kwenye ubalozi.
Duh....!. Sasa leo ndio nimeelewa!. Kwa muda mrefu nimekuwa najiuliza, imekuwaje kwa mfano tuu ya mtu mwenye level ya DGIS, anateuliwa ubalozi na kupostiwa nchi insignificant tuu?!. Sasa nimeanza kupata majibu!.

Tuliwahi kushauri Wito Kwa Viongozi Wetu: Unapokosea, hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge utamaduni wa kuwajibika ili kumuepushia Rais wetu kubeba mzigo wa karma

Kisha tukashauri tena, Viongozi wetu wanapofanya makosa ya wazi waishie tu kuomba msamaha kisha 'life as usual', au tujenge utamaduni wa kuwajibika kama enzi za Nyerere?

Sasa ushauri huu umepata sikio la kuusikia, sasa unakwenda kufanyiwa kazi, kiongozi anayevurunda mahali, hata awe nani, hakuna tena kupoozwa kwa kupewa ubalozi!, atupishe kazi iendelee!.

Ila Mama nae...!, ameanza kuwa mkweli wa type ya JPM, hakopeshi!. Kumbe kuna watu huwa wanavurunda, ila kwa vile post zao ni nyeti sana!, wanaondolewa hapo walipovurunda na kupoozwa kwa kutupwa ubalozini!.

Naunga mkono hoja, wanaovurunda, wasipoozwe na ubalozi, watupishe!.
P
 
Ni katika kikumbushana tuu!.
Hukuna jinsi, ni kuwajibika tuu!.
P
 
Ni katika kikumbushana tuu!.
Hukuna jinsi, ni kuwajibika tuu!.
P
Tulishauri, haikusaidia, sasa jana Mama ametumbua!. Watanzania tufike mahali tu demand the right to information wakati wa utumbuzi, mfano mpaka leo, sijawahigi kujua, kwanini Balozi Liberata Mulamula alitumbuliwa, sasa January Makamba nae ametumbuliwa, natamani kujua sababu. Sihitaji kujua sababu ya Nape kutumbuliwa itakuwa ni mdomo umemponza kwa ile kauli ya Waswahili ya "mzaha mzaha, hutumbua usaha", lakini kwa Byabato ana kosa gani?.

Nashauri tumsaidie Rais Samia, asifanye kitu kinachoitwa " bad karma accumulation" bila kujijua, japo uteuzi na utenguzi is at the pleasure of the appointing authority, ukimtumbua mtu bila haki, kwa namna inayomdhalilisha, huyo mtumbuliwa akiumia, ana develop bad karma ya maumivu yake, hiyo bad karma inahifadhiwa katika akiba ya karma accumulation ya aliyesababisha maumivu hayo!, hivyo hii accumulation ina pile up, ikifikia kuwa the pile is big enough hadi furushi hilo la karma likawa halibebeki, then hilo zigo la karma, litamuelemea mbebaji sometimes linaweza kumponza na ... ndio maana nimewashauri viongozi wetu wateuliwa Wito Kwa Viongozi Wetu: Unapokosea, hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge utamaduni wa kuwajibika ili kumuepushia Rais wetu kubeba mzigo wa karma
P
 
Nashauri kwa negligence iliyofanywa na Jeshi letu la polisi kuhusu kadhia hii ya kifo cha Mzee Ali Mohamed Kibao, Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu , kukutwa ameuwawa na mwili wake kutupwa eneo la Kunduchi Ununio,
watu wanne wawajibike!.
1. Waziri - kwa ajali kazini
2. IGP - kwa negligence ya RPC wake
3. RPC -DSM - negligence
4. OCD Kinondoni - negligence, na hawa wawili wa mwisho RPC na OCD wanaweza kufikishwa kwa Pilato!.
Ni wakati sasa Rais Samia kukasirika kama enzi za Nyerere!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…