Wanabodi,
Karibu, Nipashe ya leo
View attachment 2074235
Kufuatia Watanzania wengi kuwa ni waumini wa dini kuu mbili, Ukristo na Uislamu, hivyo sii wengi wanaijua "karma" ni nini, kwasababu "karma" ni neno la lugha ya ki Hindi "Hindu" na linafundishwa kwenye dini ya Hinduism na Buddhism, mimi nilijifunza kuhusu "karma" wakati nikiishi jiji la New Delhi nchini India.
Huu ni wito kwa viongozi wetu, unapokosea hata kwa kujikwaa tuu ulimi, tujenge tabia ya kuwajibika kwa makosa yetu, tujitokeze kuomba radhi, na ikibidi kuwajibika!.
Kwa vile mimi ni mtu wa mastory story, na sii watu wote ni wapenda mastory, wengine ni wavivu tuu wa kusoma vitu virefu, wanapenda vitu vifupi short and clear, wengine ni just wako too busy hawana muda kusoma vitu virefu, ili kuwatendea haki nisiwachoshe wengine, hii mada nimeikata vipande vipande with sub headings, ili wewe usome only what will interest you!, kwa kusoma kile tuu utakachokuwa na interest nacho.
Tuanze kwa Kuijua Karma, ni Nini na Inafanyaje Kazi
anzia hapa
Kuijua karma
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!
Karma Kwenye Uongozi wa Umma
Njoo hapa
Tuacheni ramli chonganishi: Tusihukumu tusije tukahukumiwa. Karma ndio pekee hutoa hukumu ya haki hapa duniani!
My True Story ya Kuzushiwa, Uongo, Fitna na Majungu na Karma Yake.
Karma Yangu, Karma Yao!.
Baada ya kutimuliwa kazi TVT, ndipo nikaenda shule UDSM kusomea fani nyingine kabisa ili niachane na uandishi wa habari na utangazaji!. Wale walionitenda, kila mmoja yalimkuta ya kwake, ila nikijifanyia tathmini ya life yangu ilivyo sasa na kama ningeendelea kuwa TBC, kiukweli majanga mengine ni a blessing in disguise!. Mwinyi alijiuzulu uwaziri tuu wa mambo ya ndani, akaja kuwa rais wa JMT!, hivyo kuna waliotemwa jana, Uspika au Uwaziri tuu, kumbe urais unawasubiri!. Japo kwa CCM, tayari tunaye mgombea wetu wa 2025 ila ...
Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! ila pia kuna hii sauti kuhusu 2025,
Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke, japo mambo ya voices from within, sio mambo ya kuzingatia sana, ila pia sio mambo ya kupuuzia!.
Kujiuzulu Kwa Spika Kama ni Kwa Haki, Ni Uwajibikaji, Kama Ameonewa Karma Itamfidia.
Uwajibikaji Enzi za Nyerere, Mwinyi Kujiuzulu na Kisa cha Mzee Mayalla (RIP)
Huu uwajibikaji wa enzi za Mwalimu, umepotelea wapi?. Mahabusu wangapi siku hizi wanakufa mikononi mwa polisi na hakuna uchunguzi wowote wala hatua zozote zinazochukuliwa, na hakuna mtu yeyote anayewajibika?!
Msamaha wa Spika JYN Ulikuwa ni Msamaha Batili, Kajiuzulu Shingo Upande Kwa Shinikizo!
Kwenye Hotuba ya Rais, Kuna Kiongozi Ametajwa, Anasubiri Nini?
Mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, Sio Wote Walioachwa ni Wametumbuliwa, Wengine Ni...
Rais Mama Samia Sio Malaika, Naye Ni Binaadamu, Hivyo Anaweza Kukosea, Tumsaidie!
Angalia hapa
Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda
Hitimisho
Ni lini uwajibikaji kwa viongozi wa umma utarejeshwa kwa kiwango cha uwajibikaji wa enzi za Mwalimu?. Yaani kiwango cha uadilifu wa mke wa Kaisari?. Kiongozi wa umma ni mpaka afanye kosa kubwa kiasi gani ndipo awajibike?.
Wito kwa Viongozi Wetu
Viongozi wetu, cheo ni dhamana, ikitokea ukatuhumiwa tuu, tuhuma za wazi, hata bila uthibitisho, ama kanusha ama wajibika, hata mkapishana tuu kauli na mamlaka yako ya uteuzi, ukiona tuu hamko wamoja, jikalie pembeni, usisubiri kuwekwa pembeni!, msimponze bure mama yetu Samia kwa kumtwisha mzigo wa karma zenu, kama mlivyomponza yule mwingine na karma ikafanya mambo yake!.
Ukibebwa kwa mbeleko bebeka kwa kujiachia, lakini ikitokea mbeleko iliyokubeba imelegea, sasa wewe lazima ujibebe mwenyewe, danda na kushikilia kwa nguvu zako zote ili usianguke, na ikitokea wewe umeishiwa nguvu huwezi kushikilia tena, achia mwenyewe udondoke taratibu usiumie, hiyo maana yake ni umefikia kiwango chako cha mwisho cha kubebeka hivyo sasa wewe ni zigo, lisilobebeka tena, ni busara kuachia mwenyewe usipoachia, utabwagwa chini kama zigo na utaumia!, ukiumia karma inamrudia aliyekuumiza!, hivyo kujijutia kwako na maumivu ya kubwebwa, mtatuponzea bure na huyu!, wajibikeni wenyewe msituponzee bure Mama yetu kwa mi karma yenu!.
Safari bado ni ndefu.
Jumapili njema.
Wasalaam,
Paskali.