Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Comrades,
ladies and gentlemen..
CCM hoyeee ✊
Ndugu zangu wanachama, mabalozi, viongozi wa mashina na matawi popote mlipo.
tunaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji baadae mwaka huu.
Uchaguzi huu ni muhimu sana kwetu kama chama tawala, lakini pia lengo la chama ni kupata ushindi mkubwa katika kila mtaa na kijiji, kwani huo ndio utakua msingi na chachu ya ushindi wa kishindo, katika uchaguzi mkuu ujao kwa madiwani, wabunge na Rais wa CCM, 2025.
Maelekezo muhimu ya chama yameshatolewa kote nchini. shukrani za kipekee sana ziwaendee makatibu kata wa CCM na makatibu wa matawi yote ya CCM kwa kazi nzuri sana ya kuwahamasisha na kuwasimamia mabalozi kuhakikisha wanachama wote wa CCM wanajiandikisha kwenye madaftari maalumu ya chama na panapohusika kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa baada mwaka huu..
Lakini pia wanachama wote wa CCM kama ilivyo ada yetu, tuhamasishane kwa nguvu zetu zote, tuhuishe taarifa zetu za mpiga kura ikiwa kuna ulazima wa kufanya hivyo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, wakati muafaka mazoezi haya yote haya mawili muhimu sana yatakapoanza kwenye maeneo yenu...
Hatuna sababu ya kupoteza hata mtaa moja kwenye uchaguzi huu. Chama Cha Mapinduzi na serikali sikivu ya CCM, iliyopo madarakani chini ya mwenyekiti wa CCM taifa, comrade Dr. Samia Suluhu Hassan, iliahidi waTanzania kwa maneno, na hivi sasa inatekeleza ahadi kwa vitendo..
Mungu atupatie nini tena ndrugo zangu waTanzania?
Dr. Samia Suluhu Hassan,
anakubalika, anapendwa, anaaminika na wananchi wote, kitaifa na kimataifa. kama wanachama tuna haki na wajibu wakujivunia mama huyu shupavu na madhubuti kipenzi cha waTanzania.
Dr. Samia Suluhu Hassan ndio pekee turufu muhimu na hakikisho la ushindi wa kishindo kwa CCM uchaguzi mkuu ujao.
Wakati muafaka ukifika tuungane na wanachama wengine nchi nzima kwenye kampeni ya "MITANO TENA NA DR. SAMIA SULUHU HASSAN"
Katibu wetu mkuu wa chama Taifa comrade Dr. Emanuel Nchimbi, alituelekeza mchana kweupe kwamba mwanachama wa CCM popote nchini, hahitaji kupata kibali kutoka popote kuinadi, kuielezea itikadi, sera, uelekeo na uwajibikaji wa Chama Cha Mapinduzi kwa wananchi iwe ni kijamii, kisiasa na kiuchmi...
Mwana CCM hapaswi kua mnyonge bali jasiri asie na woga, aibu wala haya kuhubiri habari njema za CCM, kwasababu mambo makubwa yanayofanywa na CCM kwa maslahi mapana ya waTanzania wote yako wazi na bayana kabisaa, hata usitumie nguvu kuyaeleza. Ukiona vyaelea, ujue vimeundwa.
Mwisho na muhimu zaidi, wale wana CCM, wenye sifa stahiki, uwezo na vigezo muafaka vinavyokidhi masharti ya kisheria na kikatiba ya kua viongozi, basi wasisite kujitokeza kugombea nafasi hizo muhimu sana serikali za mitaa na serikali za vijiji kwanmustakabali mwema wa Taifa letu..
Aidha tuendelee kumuunga mkono mh. Rais na mwenyekiti wetu wa CCM taifa kwa kazi kubwa na nzuri sana anayoendelea kuifanya ya kuwaletea waTanzania maendeleo endelevu..
Kidumu Chama Cha Mapinduzi ✊