Pre GE2025 Wito kwa wanachama wa CCM wote humu jukwaani kuelekea uchaguzi mkuu 2025

Pre GE2025 Wito kwa wanachama wa CCM wote humu jukwaani kuelekea uchaguzi mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kimekuwa "KIGUMU CHAMA CHA MAPINDUZI".
Wewe umepitwa na wakati siku nyingi.

Ajabu ni kuwa bado unategemea waTanzania wataendelea kuvumilia upumbavu milele?
Imani potofu ni mzigo na utumwa mbaya sana aise,
achana na ushirikina na ramli zisizo na kichwa wala kiuno..

Amini na kutegemea Mungu pekee...

Dr Samia Suluhu Hassan Mwenyekiti wa CCM taifa, ni kipenz cha waTanzania wote 🐒
 
Hakuna mwenye akili timamu awe upande wa CCM siku zote uchafu ni wa shetwani na CCM ni mashetwani
 
Imani potofu ni mzigo na utumwa mbaya sana aise,
achana na ushirikina na ramli zisizo na kichwa wala kiuno..

Amini na kutegemea Mungu pekee...

Dr Samia Suluhu Hassan Mwenyekiti wa CCM taifa, ni kipenz cha waTanzania wote 🐒
Kamwe siwezi kumwamini huyo 'mungu' aliyeko akilini mwako hata siku moja.
Upande mmoja unakimbilia kwenye imani uhadae watu; wakati huo huo matendo yakiwa kinyume kabisa na hiyo lugha mnayoiita ya 'staha'! Nyinyi watu kweli akili zenu ni sufuri kabisa.
 
Nape pamoja na kwamba katumbuliwa ila mawazo yake yasipuuzwe - uwezo wa kushinda uchaguzi haki bin haki Hatunao.
zingatia wito na maelekezo ya msingi kwa wanaCCM hapo juu, itakusaidia sana 🐒
 
Comrades,
ladies and gentlemen..

CCM hoyeee ✊

Ndugu zangu wanachama, mabalozi, viongozi wa mashina na matawi popote mlipo.
tunaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji baadae mwaka huu.

Uchaguzi huu ni muhimu sana kwetu kama chama tawala, lakini pia lengo la chama ni kupata ushindi mkubwa katika kila mtaa na kijiji, kwani huo ndio utakua msingi na chachu ya ushindi wa kishindo, katika uchaguzi mkuu ujao kwa madiwani, wabunge na Rais wa CCM, 2025.

Maelekezo muhimu ya chama yameshatolewa kote nchini. shukrani za kipekee sana ziwaendee makatibu kata wa CCM na makatibu wa matawi yote ya CCM kwa kazi nzuri sana ya kuwahamasisha na kuwasimamia mabalozi kuhakikisha wanachama wote wa CCM wanajiandikisha kwenye madaftari maalumu ya chama na panapohusika kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa baada mwaka huu..

Lakini pia wanachama wote wa CCM kama ilivyo ada yetu, tuhamasishane kwa nguvu zetu zote, tuhuishe taarifa zetu za mpiga kura ikiwa kuna ulazima wa kufanya hivyo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, wakati muafaka mazoezi haya yote haya mawili muhimu sana yatakapoanza kwenye maeneo yenu...

Hatuna sababu ya kupoteza hata mtaa moja kwenye uchaguzi huu. Chama Cha Mapinduzi na serikali sikivu ya CCM, iliyopo madarakani chini ya mwenyekiti wa CCM taifa, comrade Dr. Samia Suluhu Hassan, iliahidi waTanzania kwa maneno, na hivi sasa inatekeleza ahadi kwa vitendo..
Mungu atupatie nini tena ndrugo zangu waTanzania?

Dr. Samia Suluhu Hassan,
anakubalika, anapendwa, anaaminika na wananchi wote, kitaifa na kimataifa. kama wanachama tuna haki na wajibu wakujivunia mama huyu shupavu na madhubuti kipenzi cha waTanzania.

Dr. Samia Suluhu Hassan ndio pekee turufu muhimu na hakikisho la ushindi wa kishindo kwa CCM uchaguzi mkuu ujao.

Wakati muafaka ukifika tuungane na wanachama wengine nchi nzima kwenye kampeni ya "MITANO TENA NA DR. SAMIA SULUHU HASSAN"

Katibu wetu mkuu wa chama Taifa comrade Dr. Emanuel Nchimbi, alituelekeza mchana kweupe kwamba mwanachama wa CCM popote nchini, hahitaji kupata kibali kutoka popote kuinadi, kuielezea itikadi, sera, uelekeo na uwajibikaji wa Chama Cha Mapinduzi kwa wananchi iwe ni kijamii, kisiasa na kiuchmi...

Mwana CCM hapaswi kua mnyonge bali jasiri asie na woga, aibu wala haya kuhubiri habari njema za CCM, kwasababu mambo makubwa yanayofanywa na CCM kwa maslahi mapana ya waTanzania wote yako wazi na bayana kabisaa, hata usitumie nguvu kuyaeleza. Ukiona vyaelea, ujue vimeundwa.

Mwisho na muhimu zaidi, wale wana CCM, wenye sifa stahiki, uwezo na vigezo muafaka vinavyokidhi masharti ya kisheria na kikatiba ya kua viongozi, basi wasisite kujitokeza kugombea nafasi hizo muhimu sana serikali za mitaa na serikali za vijiji kwanmustakabali mwema wa Taifa letu..

Aidha tuendelee kumuunga mkono mh. Rais na mwenyekiti wetu wa CCM taifa kwa kazi kubwa na nzuri sana anayoendelea kuifanya ya kuwaletea waTanzania maendeleo endelevu..

Kidumu Chama Cha Mapinduzi ✊
CCM OYEEEEEE , SAMIAAAAAA OYEEEEE , NCHIMBIIIII OYEEEEEE , MAKALAAAAA OYEEEEEEE , KIDUMU CHAMA TAWALA , KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI. Ndugu kada mwenzangu nimefurahi sana kusoma uzi wako hapa , hakika wewe ni kada mtiifu na mpenda chama na ahsante kwa kuwakumbushia watu wakaribie ccm na wajaribu bahati zao kwenye nafasi mbalimbali za chaguzi ndani ya chama chetu pendwa. Ninapenda sana kuona upendo huu ukienea kila sehemu ya jamii zetu. Mama Samia anaongoza vyema gurudumu la nchi yetu ya Tanzania , tuna imani nae na uongozi mzima wa ccm, hakika safari ya ccm ni KIJANI njia zote za 2024 NA 2025 . CCM OYEEEEEEE . MJITOKEZE KWA WINGI NDUGU ZANGU . 2024 NA 2025 CCM NI MBELE KWA MBELE. TANZANIA YA KIJANIIIIIIII

ADAM MAGESA EKINGO
MJUMBE CCM KIVUKONI
MJUMBE CCM ILALA
iamwangdamin ( ALL PLATFORMS)
 
Msigwa aliibiwa na majambazi ya kura akatoroka bana dah, sijui yuko wap saiv 🐒
Haya sasa, na kabla hajatimkia huko ulisha sahau alisemaje vile kuhusu mhusika wa vurugu za uchaguzi ule?

Unakumbuka, lakini wewe ni mtu wa 'mungu'!
 
Chama chakavu mbele kwa mbele
Chama Cha Mapinduzi ndiyo pekee msingi wa amani, utulivu na upendo miongoni mwetu kama Taifa 🐒

Na Kiongozi wetu wa kitaifa Dr.Samia Suluhu Hassan, kipenz cha waTanzania ndioyo dira na uelekeo wa nchi yetu kuelekea uchaguzi mkuu ujao 2025🐒
 
Machawa mchinjwe xmas nyie ndio mnachangia uharibifu wa kuwajaza viongozi ujinga.!!
 
Chama Cha Mapinduzi ndiyo pekee msingi wa amani, utulivu na upendo miongoni mwetu kama Taifa 🐒

Na Kiongozi wetu wa kitaifa Dr.Samia Suluhu Hassan, kipenz cha waTanzania ndioyo dira na uelekeo wa nchi yetu kuelekea uchaguzi mkuu ujao 2025🐒
Mmewadharau sana waTanzania katika miaka ya hivi karibuni, na kugeuza hiyo "amani" kuwa silaha ya kuwatishia nayo.
Mnawafanyia ushenzi, halafu mnakimbia kupiga kelele..."Amani"!
Uvumilivu una mwisho.
 
Machwa mchinjwe xmas nyie ndio mnachangia uharibifu wa kuwajaza viongozi ujinga.!!
kwanza ulikua wap wewe mtumishi mbona uliadimika? au uliadimishwa kidogo 🐒

jambo muhimu zaidi kama waTanzania ni kuelewa maana ya uhuru na haki ya kutoa maoni na mtazamo juu ya masuala mbalimbali kitaifa na kimatafa 🐒

na jambo la maana zaidi ni ungwana na utashi katika kukubaliana kutokukubaliana 🐒

hii habari ya mimi au wewe kuona jambo fulani kwa mtazamo wako halafu mtu ana kasirika, si sawa hata kidogo,

ni vizuri kuheshimu maoni na mtazamo wa wengine kistaarabu,
habari ya sijui Fulani ni nyumbu au chawa ni useless na nonsense kwenye uwanda wa demokrasia 🐒
 
Mmewadharau sana waTanzania katika miaka ya hivi karibuni, na kugeuza hiyo "amani" kuwa silaha ya kuwatishia nayo.
Mnawafanyia ushenzi, halafu mnakimbia kupiga kelele..."Amani"!
Uvumilivu una mwisho.
kwa uwekezaji aliyoufanya Dr Samia Suluhu Hassan Mwenyekiti wa CCM taifa katika kuijenga na kuilinda Amani ya waTanzania, hayupo wa kuidhoofisha wala kuiteresha amani thabiti iliyojengwa ndani ya mioyo ya waTanzania 🐒

hakuna viashiria wala vitisho katika Amani ya Tanzania..
Na kwa upendo mkubwa sana miongoni mwa waTanzania ndio maana uzi huu ni wito kwa wanaCCM Lakini wachangiaji wengi sio wanaCCM na wanamkubali sana Dr Samia Suluhu Hassan 🐒
 
kwanza ulikua wap wewe mtumishi mbona uliadimika? au uliadimishwa kidogo 🐒

jambo muhimu zaidi kama waTanzania ni kuelewa maana ya uhuru na haki ya kutoa maoni na mtazamo juu ya masuala mbalimbali kitaifa na kimatafa 🐒

na jambo la maana zaidi ni ungwana na utashi katika kukubaliana kutokukubaliana 🐒

hii habari ya mimi au wewe kuona jambo fulani kwa mtazamo wako halafu mtu ana kasirika, si sawa hata kidogo,

ni vizuri kuheshimu maoni na mtazamo wa wengine kistaarabu,
habari ya sijui Fulani ni nyumbu au chawa ni useless na nonsense kwenye uwanda wa demokrasia 🐒
Nipo baba mtumishi nilikuwa na ban

Sasa mbona umenitolea povu?
Huu unaoufanya ni nini?
Kwanini usiwashauri viongozi wako watatue matatizo ya wananchi?
 
Nipo baba mtumishi nilikuwa na ban

Sasa mbona umenitolea povu?
Huu unaoufanya ni nini?
Kwanini usiwashauri viongozi wako watatue matatizo ya wananchi?
kumbe uongozi wa humu ulikubananisha 🤣
ulizidisha uchawa sio?

hapana,
ni muda mrefu sana sijaona povu kabisa kama zamani, halafu siku hizi hamna mapovu sijui kwanini aise..

inchi hii mama itajengwa na wenye moyo. wenye hofu ya Mungu mioyoni mwao.
Neema na Baraka za Mungu ziendelee kuambatana na kuandamana na Dr Samia Suluhu Hassan kwani anaonyesha mfano mzuri, nasi tunaiga huo katikati kuwatumikia waTanzania...

dosari na kasoro ndogo ndogo uongozini tutaendelea kunishughulikia kadiri tuwezavyo,

kidumu Chama Cha Mapinduzi ✊
 
Basi sawa kaka yake Luca 😹
 
Back
Top Bottom