Wanasisiemu walio wengi wanaenda kupiga kura, wasiokuwa wanasisiemu wengi wanahudhuria mikutano ya kampeni siku ya kupiga kura hawaendi kupiga kura.
Kama kweli watanzania tunataka kuiondoa sisiemu madarakani ni lazima tabia hii tuiache bila kujali ni lini matokeo tunayoyataka yatapatikana.
Serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar haikuja tu kwa kushuka toka mbinguni, ilikuwa ni hatua kwa hatua bila kuchoka. Wengi ambao sio wanasisiemu walihakikisha wanaenda kupiga kura kiasi ambacho kiliwabana hata hao wanasisiemu kushindwa kuiba kura kwakuwa hazikuibika tena.......stepu inayofuata ipo siku sisiemu itang'olewa pale Zanzibar.
Kuna suala la uimara wa wagombea wa vyama vinavyokinzana na sisiemu ni la msingi sana na muhimu. Hii tabia ya wagombea wa vyama mbadala kununulika kirahisi na sisiemu linawakatisha sana tamaa watanzania wenye nia thabiti ya kutaka mabadiliko. Mgombea ni lazima awe na misimamo inayoeleweka na isiyoyumba Wala kuyumbishwa.
Mabadiliko ya kiuongozi ni mchakato wa hatua kwa hatua na yanahitaji uvumilivu na kutokata tamaa
Sent using
Jamii Forums mobile app