Uchaguzi 2020 Wito: Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na timu yake yote wajiuzulu

Hilo lijamaa tangu lijiunge na JF enzi zilee bado tu linaongea bla blah hadi leo. Sijui lini litabadilika kuendana na muda, manaake miaka inakwenda na mambo yanabadilika.
 
Hahahahaaaaaa....
 
Hahahahaaaaaa....
Unacheka mkuu?

Kwa nini? Nimeongea pumba ama?

Ni kweli Mkapa alikuwa Rais. Tena kwa mihula miwili.

Alinufaika na mfumo huu uliopo sasa hivi.

Mwaka jana au sijui mwaka juzi eti akadai kuwa tunahitaji tume huru ya uchaguzi.

Sasa swali ibuka ni: alikuja kutambua lini kuwa tunahitaji tume huru ya uchaguzi?

Angetuachia taasisi huru kama hiyo hakika angekumbukwa vizuri sana na watu walio wengi....

Sijui ni nini tu kilichomshinda kutuachia hiyo taasisi....
 
Kweli kabisa mkuu, asilimia 99 vyama vilivyobaki ni mapandikizi labda mzee Rungwe tu ndio unaweza ukamuona muona ni mpinzani. Ndio sababu ukiacha chadema na act wengine wote walikuwa wanaunga mkono kauli ya "ukishapiga kura rudi nyumbani". Angalia malalalimiko kwa Lissu hadi nec kumsimamisha Lissu kufanya kampeni yaliwekwa na mgombea wa ccm na yule Leopold Mahona, sasa huyu Mahona atakuwa ni mpinzani kweli?
 

Sasa kama tume ndo iliyotoa hizo karatasi za kura kwa CCM unadhani itasemaje itasema ni kweli karatasi za kura zimekamatwa sasa kwanini tuhangaike kusikiliza wakosaji waliotifikisha hapa tulipo. Ni vema wakajihuzulu kwa hiyari yao kuliko kusubiri vurugu kwanza la nguvu za wananchi.
 
Hajapiga, haya ni maajabu, mimi sijawahi kusikia kwamba Mgombea Uraisi hajipigii kura halafu anawaambia wengine wajitokeze kumpigia kura? Huyu jamaa tundu kichwani hazimtoshi aisee, ...

Mbona mnakuwa wajinga hivo kama hufuatilii habari ni bora kukaa kimya hajapiga vipi alioneshwa tangu akiwa airport kwenda singida na akaoneshwa Twitter akipiga kura na akaongea na vyombo vya habari na ITV kwenye taarifa ya habari wamemuonesha akiongea baada ya kupiga kura, mtakuwa mnaangalia TBC ndiyo maana
 
Samahani kwa jibu la kuchelewa. Sijui haya maoni yako yalifichwa? Sikuyaona.

Huyo mkapa hana tofauti na marais wengine. Nadhani ndio alikuwa Rais fisadi kuliko wote waliomtangulia.

Hata hako kakitabu chake cha maungamo alichokaandika ni vile dhamiri ilikuwa inamsuta tu kwa madhambi aliyoyafanya dhidi ya watanzania.

Wakiwa kwenye mfumo wa mamlaka huwa wanalewa sana na wanazungukwa na genge la mafisi ambao wako tayari kufanya lolote kulinda utawala.

Wakishaondoka madarakani ndio akili zinarudi kichwani.

Mkapa hastahili sifa yoyote, na maungamo yake hayana msaada wowote.

Alikuwa fisi kama mafisi wenzake waliomfuatia.

Lakini sishangai, maana kuna watu wanamsifu Kikwete leo hii. Hata magufuli akiondoka watamsifu pia.

Tutakuwa tunazunguka pale pale bila kujua tatizo ni nini.
 
Mkuu awajibikaji wa staili hiyo bado haujafika huko bara Giza labla 2080 hukooo hawa wakiwa marehemu. Tuombe Mungu
 
Mashujaa wa election 2020, masaa 9 tuu majibu Jimbo la Hai tayari.
 
Chui leo umevaa ngozi ya Mbuzi na ujichanganya na Mbuzi kwenye zizi lao ili uwatafune kwa raha yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…