Uchaguzi 2020 Wito: Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na timu yake yote wajiuzulu

Uchaguzi 2020 Wito: Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na timu yake yote wajiuzulu

Kupitia akaunti ya twitter ya Tundu Lissu,nimeona video (bila shaka ni huko Kawe, Dar-es-salaam) inayoonyesha rundo la kura zinazidaiwa kuwa ni feki huku Polisi wakishirikishwa kuzitambua/ kushuhudia karatasi hizo za kura ambazo zimepigiwa kura mgombea wa CCM.

Video hii ni tofauti na ile inayoonyesha wananchi wakichoma moto kura walizozikamata.

Ukiacha huko Kawe, kuna video nyingine mtandaoni(twitter), inaonyesha wananchi(mkoani Kigoma) wakivamia kituo cha kupigia kura baada ya kubaini uwepo wa kura feki kwenye mfuko huku mwenye mfuko akigoma kuutoa /kukaguliwa na kusababisha vurugu kituoni hapo.

Kwakuwa hali hii inaripotiwa katika maeneo mengi nchini ,ni wazi Tume ya Uchaguzi imeshindwa kutimiza wajibu wake na hivyo inapaswa kujiuzulu yote kuanzia mwenyekiti, mkurugenzi na watendaji wengine wote waliohusika kusimamia huu uchaguzi unless watuthibitishie kuwa madai haya ni ya uongo.

Mwisho, uchaguzi huu wote ufutwe iwapo tuhuma/ madai haya yathibitika kuwa ni ya kweli.
They are there like figureheads
 
RAIS TUNDU LISSU ATUPE TU GREEN LIGHT TUINGIE MTAANI TUMECHOKA NASEMA TUMECHOKA. SIOGOPI KUFA KWA AJILI YA TAIFA LANGU DHIDI YA MKOLONI MWEUSI NIMESEMA TUMECHOKA NASEMA BAAS MAAMAE.

Hahaha skia hii mbuzi ingine uku
 
Hadi hapa huu uchaguzi ni invalid, tunarudia, hatukubali matokeo yoyote yale, kura zimekamatwa kibao je ambazo zishapitishwa ni ngapi? na majimbo mangapi?
Huu uchaguzi tushau-cancel tunarudia mwingine tukiwa na tume huru sio hii ya sasa hivi.

Naona una usingizi,
 
Hiyo si solution dhidi ya hawa wahuni wa ccm. Hawajali maslahi ya Nchi hawa zaidi ya maslahi yao binafsi.

Maccm yanajua fika hayapendwi na yamechokwa na asilimia kubwa ya Watanzania ndiyo sababu yanahofia chaguzi huru na za haki kwa kujua kwamba ndiyo itakuwa kaburi lao

Baada ya huu uhuni wao mimi naona vikwazo vya kiuchumi labda vinaweza kutusaidia ili kuwatia adabu hawa wahuni wasiwe na jinsi zaidi ya kukubali uwepo wa katiba mpya na tume huru ya Uchaguzi ili kuhakikisha chaguzi zetu ni HURU na za HAKI.

Kama Nchi nyingi za Afrika wapinzani wanashinda na kuingia madarakani bila machafuko yoyote sioni kwanini hilo lishindikane kwenye Nchi yetu. Tanzania bila maccm INAWEZEKANA KABISA.

Ebu lala kwanza
 
Viongozi ni watu wenye vision, nadhani viongozi wa upinzani wanazingua.
Cha msingi viongozi ingizeni watu road kuanzia kesho
 
Ngojeni dawa iwaingie vizuri naona mnaanza kuwashwawashwa. Khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Billions za pesa za walipa kodi wamezitumia hawa wahuni kufanya hiki kituko cha hali ya juu ili tu kuiba chaguzi kwa haya maccm ambayo yamechokwa na Watanzania kila kona Nchini lakini kwa uroho wao wa madaraka yanatumia tumeccm/tume FAKE na polisiccm ili kuiba chaguzi kila mara.

Sasa basi imetosha Charles Wilson Mahera na Kaijage na tume yetu wajiuzulu haraka sana na ikiwezekana wafunguliwe mashtaka kwa kuvuruga uchaguzi kwa makusudi.
Mkuu kujiuzulu kwao (japo ni jambo lisilowezekana kabisa) sidhani kama kutarejesha haki zinazochezewa na wapuuzi wachache.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Baada ya uchaguzi huu hawa watendaji wa tume waanze kushikishwa adabu mmoja mmoja kimya kimya
Yaani unahamasisha wauwawe. Je, unajuwa ni jinai kuunda mbinu au kuhamasisha murder/assassination?
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] BAVICHA tuliwambia piganieni Tume huru ya uchaguzi toka 2015, nyie mkaishia kujadili kingereza cha Magu
 
Kila uchaguzi mambo yaleyale yanajirudia kila upande(state na opposition)hawachukui hatua.

Hapa wakulaumiwa ni wote, sio tume ya uchaguzi tu
Sio kweli, mwaka huu hayajajirudia nafikiri mwaka huu ni hovyo kuliko miaka yote!
 
Tukiwaambia msusie chaguzi, hamsikii.

Sasa mnalialia nini? Kwani hamkujua zitakuwepo figisu?
Kususia Uchaguzi haiwezi kuwatisha CCM hata kidogo.

Wamesajili vyama vingi bandia vya upinzani kama mbadala endapo CHADEMA wataleta mambo ya kususa na kukacha.

CHADEMA ndio tegemeo pekee la wananchi kwa sasa.

Ni juu ya wananchi wenyewe kupambana na hawa maharamia wa kijani, la sivyo CHADEMA itakufa na ndio utakuwa mwisho wa demokrasia nchini. Tutabaki na maigizo ya hawa makachero uchwara wenye wafuasi watano.

Bila wananchi kuamka na kuchukua mamlaka yao, naona giza kubwa sana mbele. CCM itatawala miaka mia hamsini ijayo.
 
Hawana akili kabisa hao.
Mkuu kwa hili hapana. Sikubaliani na wewe.

Mchakato wa kupata tume huru hauwezi kufanywa na chadema pekee. Haiwezekani.

Mfumo wa sheria ya kubadili na kutengeneza Katiba, unampa Rais mamlaka yote ya kuamua Katiba mpya itungwe ama isitungwe.

Tume ya uchaguzi ni Taasisi iliyoundwa na Katiba. Kutaka kuibadili mfumo wake, lazima mchakato wa kubadili Katiba au kutunga Katiba mpya ufanywe.

Rais akisema hakuna katiba mpya, hakutakuwa na katiba mpya hata mfanye nini.

Na hata wakijaribu kufanya mabadiliko ya Katiba kupitia bunge, bado akidi yao ni ndogo hawatoshi.

Narudia tena, nchi hii bila WANANCHI WENYEWE kuamka na kupambana na hawa maharamia, ccm haiwezi kutoka madarakani abadani.

Hapa tutawaonea chadema bure. Wanaostahili lawama ni hawa maharamia wanaoharibu nchi na kutawala kidhalimu kinyume na matakwa ya wananchi.
 
Mkuu kwa hili hapana. Sikubaliani na wewe.

Mchakato wa kupata tume huru hauwezi kufanywa na chadema pekee. Haiwezekani.

Mfumo wa sheria ya kubadili na kutengeneza Katiba, unampa Rais mamlaka yote ya kuamua Katiba mpya itungwe ama isitungwe.

Rais akisema hakuna katiba mpya, hakutakuwa na katiba mpya hata mfanye nini.

Narudia tena, nchii hii bila wananchi kuamka na kupambana na hawa maharamia, ccm haiwezi kutoka madarakani abadani.

Hapa tutawaonea chadema bure. Wanaostahili lawama ni hawa maharamia wanaoharibu nchi na kutawala kidhalimu kinyume na matakwa ya wananchi.
Harakati za kudai katiba mpya na tume huru si za CHADEMA peke yake.

Hilo kwangu halina ubishi.

Ni wajibu wa kila mpenda demokrasia kudai hivyo vitu.

Bado naamini kwamba kwa kuendelea kushiriki chaguzi zao [yes, hizi chaguzi ni za kwao CCM], kunawapa CCM uhalali ambao hawaustahili.

Ingekuwa ni juu yangu, ningesusia kabisa kushiriki hizo chaguzi mpaka kuwepo na mazingira ya kueleweka na yanayotoa fursa sawa kwa washiriki wa mchakato wote.

Siwezi kushiriki shughuli iliyo na ushindani ambayo mahindani wangu ndo anaweka mwamuzi, timekeeper, kamisaa, mashabiki, na kila kitu kingine kinachompa yeye advantage dhidi yangu.

Never.
 
Vyama vya upinzani viko kimaslahi binafsi mnooo zaidi ya kuwepo kwa maslahi ya taifa haswa wananchi waliowengi

Hakuna chama cha upinzani imara kinachodhamiria kuchukua dola kwa vitendo

Hakuna chama cha upinzani chenye dira ya kueleweka na inayotekelezeka

Hakuna chama cha upinzani kinacholea wanachama wake kwenye misingi imara ya uzalendo

Panapokua na upinzani dhaifu ni credit kwa chama tawala na hivi CCM inaweza kujisafisha kwa kiasi kikubwa watanzania walio wengi wameona na wamerudisha imani

Chadema ilikua imara sana lakini 2015 waliamua kuudhihirishia umma kwamba wao wanaweza kununulika kirahisi mno baada ya kumpokea waliyemuita fisadipapa, wakasaidiana na chama tawala kumnyoa kwa ushahidi kwamba hawezi kuendelea kuongoza baraza la mawaziri kwa uchafu alokwisha ufanya, halafu wakampokea wakamsafisha na kumpa dhamana ya kuongoza dola kwa sababu tuu alikua na mtaji wa mapesa na watu. Kwa maana nyingine sasa nchi yetu haiwezi kuwa salama mikononi mwao

Upinzani wasimtafute mchawi na wakati wao wenyewe ndio wanajimaliza
Hii ndio justification yako ya wizi wa kura mlioufanya leo?!

Umeandika maelezo mengi ambayo hayaendani kabisa na mada iliyopo mezani, unajaribu kujiliwaza kwa kuficha uozo mnaoufanya sasa chini ya kapeti!.
 
Back
Top Bottom