Uchaguzi 2020 Wito: Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na timu yake yote wajiuzulu

Uchaguzi 2020 Wito: Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na timu yake yote wajiuzulu

Acheni kupotosha umma uchaguzi umekuwa wa haki na uwazi mkubwa sasa mnaleta nadharia zenu kutafuta sympath.Tuliwaambia leo ndio mtaelewa wananchi wanaenda miaka 5 Tenaa na Magufuli.

Congratulations in advance President Magufuli


JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Ni hivi:

Mimi ningependa kuona wapinzani wanasusia chaguzi zote, za ngazi zote...
Changamoto ni kwamba vipo vyama vibaraka zaidi ya 10. Upinzani halisi ukisusa,upinzani mamluki uta cover gap. Hivyo unachokikusudia kionekane na kutokea kwa njia hiyo hakitatokea.
 
Solution kwa sasa baada ya huu uhuni ni kuwepo kwa Serikali ya maridhano au mpito ili kupata Katiba mpya na tume huru ya Uchaguzi ili uchaguzi urudiwe haraka iwezekanavyo ndani ya miezi sita au 12. Haiwezekani basi vikwazo vya kiuchumi vinatuhusu.
Vikwazo kawekewe wewe na ukoo wako..Tuliwaambia uchaguzi sio mihemko yenu ya kuropokaropoka haya angalieni mnalialia.

Congratulations in advance President Magufuli

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Endelea kuota!

2025 mtashiriki tena uchaguzi mkuu katika mazingira haya haya halafu mkipigwa kwenye sanduku la kura, mtarudia vilio vilevile.

Vyama vya upinzani viko kimaslahi binafsi mnooo zaidi ya kuwepo kwa maslahi ya taifa haswa wananchi waliowengi

Hakuna chama cha upinzani imara kinachodhamiria kuchukua dola kwa vitendo

Hakuna chama cha upinzani chenye dira ya kueleweka na inayotekelezeka

Hakuna chama cha upinzani kinacholea wanachama wake kwenye misingi imara ya uzalendo

Panapokua na upinzani dhaifu ni credit kwa chama tawala na hivi CCM inaweza kujisafisha kwa kiasi kikubwa watanzania walio wengi wameona na wamerudisha imani

Chadema ilikua imara sana lakini 2015 waliamua kuudhihirishia umma kwamba wao wanaweza kununulika kirahisi mno baada ya kumpokea waliyemuita fisadipapa, wakasaidiana na chama tawala kumnyoa kwa ushahidi kwamba hawezi kuendelea kuongoza baraza la mawaziri kwa uchafu alokwisha ufanya, halafu wakampokea wakamsafisha na kumpa dhamana ya kuongoza dola kwa sababu tuu alikua na mtaji wa mapesa na watu. Kwa maana nyingine sasa nchi yetu haiwezi kuwa salama mikononi mwao

Upinzani wasimtafute mchawi na wakati wao wenyewe ndio wanajimaliza
 
Dawa ni kususia chaguzi zote.

Kususia huko ndo kuta highlight upumbavu uliopo.

Kuendelea kushiriki chaguzi ambazo mnajua kabisa hazina mazingira yaliyo sawa kwa washiriki wote, ni uwendawazimu.

Anywho, endeleeni kushiriki na endeleeni kuwapa uhalali CCM.

Pia, endeleeni kulialia kuwa hakuna tume huru ilhali mnajua kabisa hatma yenu.

Huyo Mkapa angeyasema hayo ya tume huru ya uchaguzi kabla ya 1995, basi ningemwona wa maana sana.

Lakini kusema hivyo 2019 baada ya yeye kunufaika na hiyo hiyo tume isiyo huru, ni unafiki tu. 1995 na 2000 hakujua kuwa tume yetu ya uchaguzi si huru?
Vile vyama vya msimu kumi na ngapi vile, vinavyopewa pesa na ccm vitajitokeza na kushiriki uchaguzi kama vyama vikubwa vitasusia, na kwa hivyo kususia hakutasaidia.
 
Changamoto ni kwamba vipo vyama vibaraka zaidi ya 10. Upinzani halisi ukisusa,upinzani mamluki uta cover gap. Hovyo unachokikusudia kionekane na kutokea kwa njia hiyo hakitatokea.
Hata Afrika Kusini enzi za utawala wa makaburu, mamluki walikuwepo waliokuwa wakifanya kazi na hao makaburu.

Lakini ANC haikuvunjika moyo. Ikaendeleza mapambano.

Kususia chaguzi za maigizo bado ndo moja ya njia bora ya kuweka shinikizo la mabadiliko yanayohitajika.

Maishani mamluki hawawezi kukosekana.

Such is life.
 
Kupitia akaunti ya twitter ya Tundu Lissu,nimeona video(bila shaka ni huko Kawe, Dar-es-salaam) inayoonyesha rundo la kura zinazidaiwa kuwa ni feki huku Polisi wakishirikishwa kuzitambua/kushuhudia karatasi hizo za kura ambazo zimepigiwa kura mgombea wa CCM...
Hawa watapandishwa vyeo wote. Maana wanachokifanya wamepewa maelekezo. Ili uchaguzi ufutwe labda itokee fujo na jumuiya ya kimataifa iingilie.
 
Vile vyama vya msimu kumi na ngapi vile, vinavyopewa pesa na ccm vitajitokeza na kushiriki uchaguzi kama vyama vikubwa vitasusia, na kwa hivyo kususia hakutasaidia.
So?

Si ndio vizuri sasa kujua nani ni nani?

Au....?
 
Hawa wapinzani wa Tanzania hawaambiliki!

Ni sikio la kufa.

Nyani Ngabu hakuna mpinzani wa nchi hii ambae angeshika dola amefanya robo ya alichokifanya John Pombe Magufuli. Huo ni ukweli mchungu sana ila moyoni mwao wanajua
Wasiwalaumu watanzania ila wajilaumu wao wenyewe
 
Wewe unadhani ni kuota lakini Nchi kuendeshwa kidikteta matokeo yake ndiyo haya. Mkapa aliona mbali na ndiyo sababu bila aibu wala woga akataka kuwepo kwa wa Tume HURU lakini hakuna hata mmoja katika Wastaafu, walio ndani ya maccm au Serikali waliomuunga mkono.

Nchi haina maendeleo ya kweli kwani vipaumbele vya Watanzania vinadharauliwa na kwenye uchaguzi wanashindwa kuchagua viongozi wawatakao. Itafika wakati wananchi watachoka na hapo ndiyo yatatokea machafuko makubwa na ya kutisha.

Mubarak alikaa madarakani kwa miaka mingi na chaguzi zake FAKE kwa kujiaminisha jeshi zuri kuliko yote Afrika litamlinda lakini wananchi waliposema sasa basi jeshi halikufua dafu kwenye NGUVU YA UMMA. Tanzania si kisiwa yaliyotokea Misri yanaweza kabisa kutokea hapa. Itakuwa ni kilio cha mbwa mdomo juu kwani dalili za Watanzania kutaka mabadiliko ya uongozi wa Nchi ni kubwa mno.
Endelea kuota!

2025 mtashiriki tena uchaguzi mkuu katika mazingira haya haya halafu mkipigwa kwenye sanduku la kura, mtarudia vilio vilevile.
 
Back
Top Bottom