Uchaguzi 2020 Wito: Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na timu yake yote wajiuzulu

Uchaguzi 2020 Wito: Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na timu yake yote wajiuzulu

Screenshot-2020-10-28-at-15.54.29-660x400.png

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage amesema Tume hiyo haijapokea taarifa za uwepo wa kura feki katika majimbo ya Kawe, Pangani na Kigoma.

Amewataka wananchi kuendelea kujitokeza kupiga kura katika muda huu mchache.

Chanzo: Millard Ayo.

Kaijage analaumiwa bure ilihali hajapelekewa hizo case
Chadema fuateni utaratibu ili kuweza kupata haki yenu
 
Hujajibu swali kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka jana ambao ulisusiwa na wapinzani baada ya 98% ya wagombea wao kuenguliwa. Maccm bila woga wala aibu yakajipa ushindi wa bila kupingwa Nchi nzima. Nini kingewafanya washindwe kujipa ushindi mwingine Nchi nzima wa bila kupingwa kwa miaka mingine mitano kama upinzani ungesusia uchaguzi?

Wapinzani waliliona hilo na mimi nawapongeza sana kushiriki kwani wameweza kuionyesha dunia jinsi ambavyo chaguzi zetu zilivyojaa wizi, vitisho na kukosa uhuru na haki kwa wapiga kura kuchagua viongozi wawatakao.

Dawa ni kususia chaguzi zote.

Kususia huko ndo kuta highlight upumbavu uliopo.

Kuendelea kushiriki chaguzi ambazo mnajua kabisa hazina mazingira yaliyo sawa kwa washiriki wote, ni uwendawazimu.

Anywho, endeleeni kushiriki na endeleeni kuwapa uhalali CCM.

Pia, endeleeni kulialia kuwa hakuna tume huru ilhali mnajua kabisa hatma yenu.

Huyo Mkapa angeyasema hayo ya tume huru ya uchaguzi kabla ya 1995, basi ningemwona wa maana sana.

Lakini kusema hivyo 2019 baada ya yeye kunufaika na hiyo hiyo tume isiyo huru, ni unafiki tu. 1995 na 2000 hakujua kuwa tume yetu ya uchaguzi si huru?
 
Ajiudhulu Kwa njama za kipuuzi siyo??

Mpaka huu muda hakuna lalamiko lolote lile ktika ofs ya tume
 
2019 si upinzani ulisusia uchaguzi ule wa Mitaa baada ya wagombea wao wengi kuenguliwa kihuni? Kipi kilitokea?

Wangeamua kususia huu uhuni na wizi wa hali ya juu tungeujuaje? Dunia ingeujuaje?
Unadhani kwanini Mkapa alitaka iwepo tume huru ya uchaguzi?
View attachment 1614828
Basi walaumu wapinzani kwa ujinga wao
 
Kupitia akaunti ya twitter ya Tundu Lissu,nimeona video(bila shaka ni huko Kawe, Dar-es-salaam) inayoonyesha rundo la kura zinazidaiwa kuwa ni feki huku Polisi wakishirikishwa kuzitambua/kushuhudia karatasi hizo za kura ambazo zimepigiwa kura mgombea wa CCM.

Video hii ni tofauti na ile inayoonyesha wananchi wakichoma moto kura walizozikamata.

Ukiacha huko Kawe, kuna video nyingine mtandaoni(twitter), inaonyesha wananchi(mkoani Kigoma) wakivamia kituo cha kupigia kura baada ya kubaini uwepo wa kura feki kwenye mfuko huku mwenye mfuko akigoma kuutoa /kukaguliwa na kusababisha vurugu kituoni hapo.

Kwakuwa hali hii inaripotiwa katika maeneo mengi nchini ,ni wazi Tume ya Uchaguzi imeshindwa kutimiza wajibu wake na hivyo inapaswa kujiuzulu yote kuanzia mwenyekiti,mkurugenzi na watendaji wengine wote waliohusika kusimamia huu uchaguzi.

Mwisho, uchaguzi huu wote ufutwe.
Tuonyeshe hiyo video ya tweeter ikionyesha hao polisi wakihakiki hizo karatasi, msije kua ni mkatengeza karatasi zilizopigwa kura kutaka kuaminisha watu kua uchaguzi haukua fair, mlichoma ofisi yenu hili litawashindaje?, Kubalini tu matokeo, hii janja haiwasaidia kamwe
 
Weka ushahidi hapa Tundu Lisu akipiga kura kama ilivyo kawaida kwa Wagombea wote Duniani, weka ushahidi tu, its eaaasy , ...

Wewe kama nani? Kama hukuona si ni shauri yako unampigia nani kelele hapa
 
Kupitia akaunti ya twitter ya Tundu Lissu,nimeona video(bila shaka ni huko Kawe, Dar-es-salaam) inayoonyesha rundo la kura zinazidaiwa kuwa ni feki huku Polisi wakishirikishwa kuzitambua/kushuhudia karatasi hizo za kura ambazo zimepigiwa kura mgombea wa CCM.

Video hii ni tofauti na ile inayoonyesha wananchi wakichoma moto kura walizozikamata.

Ukiacha huko Kawe, kuna video nyingine mtandaoni(twitter), inaonyesha wananchi(mkoani Kigoma) wakivamia kituo cha kupigia kura baada ya kubaini uwepo wa kura feki kwenye mfuko huku mwenye mfuko akigoma kuutoa /kukaguliwa na kusababisha vurugu kituoni hapo.

Kwakuwa hali hii inaripotiwa katika maeneo mengi nchini ,ni wazi Tume ya Uchaguzi imeshindwa kutimiza wajibu wake na hivyo inapaswa kujiuzulu yote kuanzia mwenyekiti,mkurugenzi na watendaji wengine wote waliohusika kusimamia huu uchaguzi.

Mwisho, uchaguzi huu wote ufutwe.
Na nilazima tume yote mpaka ngazi ya Jimbo warudishe pesa yote ya uchaguzi ni Kama pesa umetumika bure
 
Hujajibu swali kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka jana ambao ulisusiwa na wapinzani baada ya 98% ya wagombea wao kuenguliwa. Maccm bila woga wala aibu yakajipa ushindi wa bila kupingwa Nchi nzima. Nini kingewafanya washindwe kujipa ushindi mwingine Nchi nzima wa bila kupingwa kwa miaka mingine mitano kama upinzani ungesusia uchaguzi?

Wapinzani waliliona hilo na mimi nawapongeza sana kushiriki kwani wameweza kuionyesha dunia jinsi ambavyo chaguzi zetu zilivyojaa wizi, vitisho na kukosa uhuru na haki kwa wapiga kura kuchagua viongozi wawatakao.
Ni hivi:

Mimi ningependa kuona wapinzani wanasusia chaguzi zote, za ngazi zote.

Wanayo sababu ya msingi kabisa kufanya hivyo.

Wakisusia hizo chaguzi halafu CCM wajipe ushindi, so be it.

We’ve been there before.

Toka mwaka 1965 hadi 1995, nchi hii ilikuwa nchi ya chama kimoja.

Kila kitu kilianzia na kuishia na CCM.

And guess what? We survived it.

Naamini kabisa tunaweza kabisa ku survive kipindi kingine ikiwa lengo ni kudai mazingira bora yenye kutoa haki na fursa sawa kwa washindani wote.

CCM wakisusiwa, na wao wakiamua kujipa ushindi wa mezani, watakosa uhalali mbele ya wananchi na hata mbele ya jumuia za kimataifa kwa sababu, sababu za kususia chaguzi za maigizo zina mashiko.

Hivyo, kama tuli-survive miaka 30 ya chama kimoja, sioni kabisa kwa tusiweze ku survive kipindi kingine.

Acha CCM wajipe hata ushindi wa asilimia 500!

Mimi sioni kabisa mantiki ya kushiriki chaguzi ambazo mtu unajua kabisa ni zoezi la kuwapa tu uhalali CCM.

Who is going to blame you for boycotting sham elections?

Boycotting sham elections is about courage, convictions, and principles. It’s about honor.

Taking part in sham elections is about fear. Fear of your opponent taking it all.

Im not down with fear. Not now, not ever.

However, I’m down with the courage of my convictions.

Boycott these sham elections.
 
Back
Top Bottom