digba sowey
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 10,508
- 23,368
Katika nyakati hizi ngumu, sauti zetu hazipaswi kuzimwa na woga wala hofu. Wale waliochoshwa na ukandamizaji, mauaji na utekaji unaoendelea nchini mwetu, ni wakati wa kusimama na kusema hapana. Hatutakubali kuona ndugu zetu wakipotea bila sababu, haki kupotoshwa, na sauti za wanyonge kufifia gizani.
Tukijadili juu ya dhuluma hii dhidi ya raia wenzetu, lazima tutumie lugha inayoakisi ukweli wa historia yetu. Tanganyika ndio ardhi yetu, na ndio tunakoshuhudia maovu haya ya mauaji,utekaji na ugandamizaji wa haki ambao hatujawahi kuushuhudia Toka tupate uhuru. Kuweka rekodi sawa ni kuwa,Tanzania ni muungano wa mataifa mawili—Tanganyika na Zanzibar. Lakini mauaji na utekaji vinavyoikumba jamii yetu havisikiki Zanzibar, bali ni Tanganyika pekee. Kwa hivyo, ili kuweka bayana hali halisi, ni vyema tutumie jina letu halisi—Tanganyika na Watanganyika tukiwa tuna zungumza juu ya dhuluma hii.
Zaidi ya hilo, kuitambua Tanganyika kwa jina lake kunawasha moto wa uzalendo na ari ya kuipigania haki yetu. Utawala dhalimu unajaribu kufifisha matumaini, kukandamiza wapigania haki, kuwateka ,kuwauwa na pengine kuwabambikizia kesi za uongo wale wanaothubutu kuzungumza. Lakini historia inatuambia kuwa ukandamizaji hauwezi kudumu milele—sauti za haki hushinda, na kila taifa lenye watu waliowezeshwa hujinasua kutoka kwenye minyororo ya dhuluma.
Kwa hiyo natoa wito ambao haupaswi kupuuzwa na yeyote aliyeumizwa na anayeumizwa na serikali hii dharimu hasa vyama vya upinzani, viongozi wa kidini katika makanisa na misikiti, pamoja na wanaharakati, wanapolaani mauaji, utekaji na ukandamizaji wa Watanganyika, ni lazima watumie majina sahihi yaani Tanganyika na Watanganyika ,Ni kupitia mwamko huu ndipo Watanganyika wataweza kushikamana kwa pamoja, kufungua macho yao, na kuamua kuikomboa Tanganyika yao, ili irudi mikononi mwa wenyewe.
Mwisho,Tanganyika si ya dhalimu na udhalimu bali ni ya Watanganyika!