Wito wa mpito kwa DPP: Wakili aliyemwandaa ACP Kingai aondolewe jopo la Mashtaka la akina Mbowe

CROSS EXAMINATION OF WITNESS SIO MCHEZO MCHEZO UONGO NA UKWELI HUWA MAJI NA MAFUTA.
 
Mkuu; usiwashitue. Mungu kawatia upofu. Waache wajikaange kwa mafuta yao. Inapendeza na kufurahisha.
 
Hv unadhan yanaelewa haya???
 
Hata mkikaa pamoja bado mtapitiwa tu. Iliwahi kujitokea hii na jamaa angu . Tuliaibika mbele ya mkuu wa kituo sitakaa nisahau.
 
Hivi ni lini mahakama zetu zitaanza kufanya live streaming ya mwenendo wa kesi hasa zile zenye hisia na maslahi mapana ya jamii.
 
Kwanini mawakili wa Jamhuri mara nyingi hawafanyi mambo kwa umakini?
Wamechoka kupewa kesi za kubumba wakati wao ni mawakili wasomi(ndio maana spika inamkera wakijiita wasomi)
 



Sasa hii ni kuandaliwa au kufundishwa kudanganya!!
 
Mashahidi wameamua kukimbia wakajipange upya, Kingai alijikojolea wengine watakata gogo kizimbani…. dadadeeki.
 
MWENENDO MZIMA WA KESI YA MH. FREEMAN MBOWE MAHAKAMANI LEO.
PART 7.

[emoji117]Wakili Peter Kibatala anaendelea..

Sehemu ya kwanza ya pingamizi letu kuhusu ushahidi wetu ni kuhusu jambo la sheria na sehemu ya pili ni namna ushahidi ulivyopatikana

Naiomba mahakama ifanye kesi Ndogo katika kesi Kubwa..

[emoji117]Wakili Kibatala anaendelea

Jaji kwa maana hiyo tutoe hukumu sehemu ya 1 Au tufanye hukumu kwa zote mbili?

Kibatala; tutoe hukumu sehemu ya 1 kisha tufanye kesi ndani ya kesi

JAJI; unafikiri inawezekana utaratibu zote na uchukuaji wa ushahidi unaweza kuwa sehemu ya kesi ndogo?

[emoji117]Wakili Kibatala; ndiyo inawezekana kwa sababu sisi tunataka tuzingatie kifungu 169 CPA

Wakili Mtobesya; ukisoma kifungu cha 151 kinaruhusu kuondoa muda pale mtuhumiwa anakuwa anaendelea na upelelezi, lakini kwa ushahidi wa shahidi wa 1 waliwakamata tarehe 05 na waliwaweka lockup

[emoji117]Maelezo labda kama pangelikuwa na ushahidi Mbele yako unaonyesha pana sababu iliyosababisha wasichukue maelezo

Ukisoma hukumu mbalimbalimbali za Mahakama Kuu, zinaeleza kuwa labda kama palikuwa na mazingira yaliyopeleka msichukue maelezo wakati wanafanya Maelezo

[emoji117]Tarehe 06 walikuwa nao wote na akasafiri kuja DSM na wakafika tarehe 07 Alfajiri

Mheshimiwa Jaji Kuna muda hapa haujaelezewa, Ukisoma ushahidi wa Shahidi wa kwanza anasema hawa watu walihifadhiwa majira ya saa 4 Usiku, Ukiangalia sioni sababu kuna nini kiliwazuia wasichukue

[emoji117]JAJI: je unaona unahitaji kesi ndogo Nlndani ya kesi hii kama Wakili Kibatala alivyosema kwa Kifungu cha 169 cha CPA?

Wakili Mtobesya: Vifungu vya ushahidi vinamtaka shahidi yeye ndiyo aeleze, tukienda upande wa pili wa kesi ndogo inampa shahidi kuelewa ambayo hajayaleza,

[emoji117]Jaji; Je, Mshtakiwa wa pili alitoa hayo maelezo au hajayatoa? Je, washtakiwa walitoa maelezo au hawajatoa iwe kwa mateso au lah?

Wakili Mtobesya; Maelezo yaliyochukuliwa kinyume na Sheria hayawezi kuwa maelezo halal

Wakili Mtobesya; Mheshimiwa Jaji baada ya kujiridhisha kama walifuatisha vifungu vya sheria ndiyo twende Kwenye kesi ndani ya kesi ya msingi.

Wakili wa Serikali wanasimama na kusema tumesikia mapingamizi yote...

[emoji117]Kwa maoni yetu, Mapingamizi hayo yaliyowasilishwa na Upande wa Utetezi, yanaweza kuteuliwa baada ya mahakama hii kufanya kesi ndogo ndani ya kesi..

Ni baada ya Wakili Kibatala sehemu ya Pili Kulalamikia ukiukwaji wa taratibu za kisheria wakati wa kuchukua maelezo

[emoji117]Jambo lingine hata wakati Wakili Mtobesya alikuwa anaelezea anashindwa kujitenganisha na ushahidi.

Wakili wa pili wa serikali; Mheshimiwa jaji ni msimamo wetu kuwa mapingamizi haya yasikilizwe kupitia kesi ndogo, Baada ya ushahidi kuwa umepokelewa mahakama ituruhusu kuwasilisha

[emoji117]Na hata sehemu ya Kwanza ya maelezo ya kwanza ya wakili Kibatala pia ina uhusiano na kesi kubwa

Sasa sisi tunaona pingamizi la kwanza lina uhusiano na Pingamizi la Pili, Mahakama ijielekeze kwenye kesi ndogo katika Kesi ya msingi

[emoji117]Kibatala alisema shahidi na maafisa wengine wa polisi waliwatesa washtakiwa, atusaidie kuwataja pasipo kutuacha, je ni akina nani?

Wakili Kibatala; tunaomba tupate ruhusa ya mahakama twende kwenye kesi ndogo katika kesi ya Msingi (Trial within a trial)

Ukimya unatawala kidogo

[emoji117]Tunasubiri Maamuzi ya Jaji juu ya mapingamizi 2 ya kupokelewa ushahidi wa ACP kingai ambao Umewekewa mapingamizi mawili na upande wa mawakili wa utetezi

1. Maelezo ya watuhumiwa kuchukuliwa nje ya muda.

2.Maelezo ya watuhumiwa kutolewa kwa mateso kwa watuhumiwa.

[emoji117]Lakini kwa Pingamizi la pili linataka mahakama ihairishe kusikiliza kesi ya msingi, tusikilize Kwanza kesi kuhusu pingamizi la pili kuhusiana na watuhumiwa kama waliteswa au sivyo..

BAADA YA DAKIKA 10

[emoji117]Jaji anasema kama ambavyo mawakili wasomi wamebainisha kuhusu maelezo yanayosadikiwa kuwa ni maelezo ya Onyo, Kimsingi pingamizi la kwanza lilikuwa linaweza kutatuliwa bila kuwa na kesi ndogo katika kesi ya Msingi.

[emoji117]Jaji anasema, nakubaliana na mawakili wasomi kusimamisha kesi kuu ya msingi kwanza na kuanza kusikiliza kesi ndogo, hivyo, nahairisha kesi hii ya msingi hadi saa nane mchana, tuanze kesi kusikiliza kesi ndogo..

Kesi imehairishwa hadi sasa nane mchana. Jaji ameondoka mahakamani

TUKUTANE SAA NANE......
 
yake ndiyo si likuwa anamhoji mtuhumiwa anaandika na mtuhumiwa anasaini kwamba kilichoandikwa ni sawa sasa hapo kosa liko wapi? mbowe anaenda kula mvua za kutosha gaidi mkubwa mbwa huyu
Hii mada siyo size yako. Ficha aibu kidogo waachie waelewa watoe mtiririko wa kisheria na sio wa kiudaku kama ulivyojaza kichwani mwako.
 
Mungu ndie alieumba ubongo unaotunza kumbukumbu ivyo anajua namna ya kuuchezea ubongo ili uaibike unapopotosha ukweli kwa kuumiza viumbe wengine.

Mungu hashindwi kurekebisha screw kwenye ubongo ili kumuaibisha mtu muovu
 
Sometimes stories dont have a clear beggining, middle and end-- fiction stranger than truth. Mapolisi wajipange upya. Attention ! -Fall out.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…