Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwenye hii mada yetu hatumzungumzii Rais kama raia wa Tanzania bali tunamzungumzia Rais kama mhimili wa dola.Rais kama raia wa Tanzania hiyo ni mada nyingine ambayo kwa sasa siyo mada yetu.Wewe unaiongelea kesi iliyoko mahakamani....
Umeniambia Rais ameongelea juu ya ugaidi uliousema.....
Rais naye ni raia wa Tanzania pamoja na majukumu yake makubwa.....
Rais kama mhimili anapaswa kuheshimu mihimili mingine ikiwa ni pamoja na mahakama.Sote tulisikiliza yale maongezi na ndugu Kikeke...unaweza kusema lolote juu yake.....
Una ushahidi kuwa Rais anahusika hata chembe na kesi ya Mbowe?!!!
Ile kusema Mbowe ni gaidi na magaidi wenzie walishafungwa zamani (kwa maana Mbowe kacheleweshwa) na majaji (refarii wa mchezo) ni wateule wake, wewe binafsi unaonaje hapo?? Kaingilia au bado????Wewe unaiongelea kesi iliyoko mahakamani....
Umeniambia Rais ameongelea juu ya ugaidi uliousema.....
Rais naye ni raia wa Tanzania pamoja na majukumu yake makubwa.....
Sote tulisikiliza yale maongezi na ndugu Kikeke...unaweza kusema lolote juu yake.....
Una ushahidi kuwa Rais anahusika hata chembe na kesi ya Mbowe?!!!
Mbwa mama yakyake ndiyo si likuwa anamhoji mtuhumiwa anaandika na mtuhumiwa anasaini kwamba kilichoandikwa ni sawa sasa hapo kosa liko wapi? mbowe anaenda kula mvua za kutosha gaidi mkubwa mbwa huyu
NA WEWE PIAMbwa mama yak
Ni wazi kuwa huielewi logic ya hoja na swali la Behaviourist au unaamua kupotezea kwa makusudi badala ya kujibu...Kwani wewe unahusika hata CHEMBE na kesi hiyo unayoiongelea?!!
Thus kada kaaumbukaVuta, uongo si rahisi kuu-maintain consistently during narrations and when you are on mental tension. Ndicho kilichotokea.
Utajichanganya tu maana Ni vitu vya kutunga. Huwezi kusahau ukweli wa kitu ambacho umekifanya physically, utausahau uongo mtiririko wake wa kutungwa. Na wengine watakuwa vituko zaidi...
Hah hah hah. Nimecheka sana, eti Chief Hangaya nasi tuanze kampeni! Hah hah hah. Mtanyukana sana Lumumba safari hii!Tuache yote ila hilo la dawa la kulevya ni aibu kubwa; Hivi serikali inawetegemeaje hawa watu wakati wanawavua nguo Hivi kila siku?
Wewe Tupatupa wewe, kwa sasa utaionja Segerea.Jana nilikuwepo Mahakama Kuu, Divisheni ya Uhujumu Uchumi. Sikwenda pale kwa minajiri ya kuhudhuria kesi ya akina Mbowe. Nilikwenda kufuatilia mambo ya mwanangu anayesoma pale Law School of Tanzania. Kwakuwa nilimaliza kilichonipeleka mapema na niliwaona hata marafiki zangu wakijumuika kuhudhuria kesi ya akina Mbowe, niliamua kujumuika nao. Ni katika viunga hivyohivyo vya Law School of Tanzania.
Jana, upande wa Mashtaka (Jamhuri) ilianza kuleta mashahidi. Shahidi wa kwanza, na nilishajua na kumtegemea, akawa ni ACP Ramadhani Kingai ambaye kwasasa ni RPC wa Kinondoni. Kama shahidi wa kwanza na wa muhimu wa Jamhuri, Kingai alieleza mengi kwenye kesi ya msingi na hata kwenye kesi ndogo iliyoibuka baada ya mapingamizi yaliyotolewa na upande wa Utetezi uliokuwa ukiongozwa na Wakili Msomi Kibatala.
Katika uga wa kisheria, shahidi yeyote huandaliwa na Wakili anayemleta mahakamani. Kuandaliwa si kufundishwa cha kusema ila ni kuunda mtiririko na mueleweko wa ushahidi wa shahidi husika. Pia, maadalizi hujumuisha upembuzi wa kipi cha kuanza; kipi cha kumalizia; kipi cha kusemwa na kipi cha kutokusema mahakamani kwenye kesi husika. Hata ACP Kingai aliandaliwa na Wakili au Mawakili wa Jopo la Mashtaka.
Kuna mambo ya wazi kabisa ambayo yameleta mkanganyiko badala ya muunganiko kwenye ushahidi wa Kingai. Mkanganyiko usio na tija. Kuhusu mtiririko wa matukio; kilichotokea na kilichofanyika na polisi. Nitatoa mifano michache kwakuwa mambo yenye mkanganyiko yalikuwa mengi mno. Kwanza, Kingai hakutaja kwenye ushahidi wake kuhusu watuhumiwa kufikishwa kituo cha Polisi Mbweni. Aliishia kusema walifikishwa Central Dar. Kwanini hakuandaliwa kuhusu hilo?
Pili, Kingai amesema kuwa watuhumiwa walikutwa na bastola moja na risasi tatu. Ni tofauti na Hati ya Mashtaka inayotaja risasi moja. Tatu, amezungumzia watuhumiwa kukutwa na madawa ya kulevya. Kwanini hakuandaliwa kuacha kuzungumzia kitu kisicho sehemu ya mashtaka ya akina Mbowe? Nne, Kingai amesema kuwa alipokuwa akiongoza timu ya upelelezi na ukamataji alikuwa Regional Criminal Officer (RCO) wa Arusha. Hakuandaliwa kueleza kwanini alifanyia kazi mikoa ya wengine kwenye ma-RCO na askari wengine?
Au Kingai naye alikuwa Sabaya wa pili? Tena, Kingai ameeleza kuwa kuna mashahidi walichukuliwa maelezo yao Moshi. Hapohapo akasema watuhumiwa walichukuliwa maelezo yao Dar es Salaam kwakuwa ndiko jalada lilipokuwa limefunguliwa. Kwanini wahusika wa jambo moja watofautishwe mahali pa kuchukuliwa maelezo yao? Hapa pia hakuandaliwa vyema. Kingai amefanya kadiri ya uwezo wake kuelezea. Lakini, hakuandaliwa vyema.
Halafu, kama mkamataji hakupaswa kushiriki kwenye kuwachukua maelezo washtakiwa. Hivi Wakili aliyemwandaa hakulijua hata hilo? Maana Kingai amekuwa akirudiarudia mahakamani kuwa aliwachukua maelezo washtakiwa ambao yeye mwenyewe ndiye aliyewakamata. Kufanya hivyo si kuandika stori yake mwenyewe anayetaka wengine waiamini na kumpongeza kwa uandishi wa stori tamu kuwahusu washtakiwa?
DPP Mwakitalu, chukua hatua mapema. Ondoa Wakili au Mawakili waliomuandaa Kingai. Kama Kingai amejikanyaga vile, watakaofuata wataanika madudu mapya na yakutisha zaidi.
Chief Hangaya, nasi tuanze kampeni chamani?
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
[emoji1666][emoji1666]Kwa maoni yangu Kingai kuacha kutaja Kituo cha Mbweni haikua bahati mbaya. Walikusudua kuficha kitu
Kitendo cha kuhamisha hamisha vituo watuhumiwa ni ili polisi wahalalishe kuendelea kuwashikilia na pia kuwapa kibano(utesaji). Wasingeweza kusema hivyo
Hivi uliona wapi polisi anayekamata ndiye tena anaandika maelezo wewe boyaaa??yake ndiyo si likuwa anamhoji mtuhumiwa anaandika na mtuhumiwa anasaini kwamba kilichoandikwa ni sawa sasa hapo kosa liko wapi? mbowe anaenda kula mvua za kutosha gaidi mkubwa mbwa huyu
Sasa si mpaka huko shule awe amekwenda kweli?Mijadala ya great thinkers nakushauri uwe unasoma tu bila kuchangia kitu. Maana hapo ndipo unapochemka kuuficha ujinga wako....
Yani hata logic ndogo tu kwenye hoja ya jamaa hujaielewa? Kwani shuleni ulienda kusomea ujinga?
Mungu ni Mungu tu mkuu,si uliona alivyotuondolea yule dictator mwezi April.Jeuri ubabe na kila aina ya unyanyasaji akalamba jivu sasa hivi yupo mavumbini.Mungu bhanaa....usichezee
Nikikujibu ban itanihusu,ila chukua kioo ujiangalieNyie jipeni matumaini tu hizo ni hoja mrenda mrenda sana mbowe lazima ale mvua yaani kumbe ni kweli jamaa ni gaidi na aliznza zamani
Huyo Kingai amelikoroga wacha alinywe.Jana nilikuwepo Mahakama Kuu, Divisheni ya Uhujumu Uchumi. Sikwenda pale kwa minajiri ya kuhudhuria kesi ya akina Mbowe. Nilikwenda kufuatilia mambo ya mwanangu anayesoma pale Law School of Tanzania. Kwakuwa nilimaliza kilichonipeleka mapema na niliwaona hata marafiki zangu wakijumuika kuhudhuria kesi ya akina Mbowe, niliamua kujumuika nao. Ni katika viunga hivyohivyo vya Law School of Tanzania.