Wito: "wanaoua Albino na wenyewe muwaue!" - Pinda


...mmhh...vipi tena mkuu........hapa anazungumziwa Mizengo Pinda - Waziri Mkuu.....au?
 
Habari nilizozipata sasa hivi zimethibitisha hofu yangu.

Mkulu mbona unatuacha kwenye mabano? hofu yako gani iliyothibitishwa? hebu yaweke haya mambo wazi! ukishathibitisha basi hutaki kushare nasi ulichokithibitisha au inakuwaje?
 
Habari nilizozipata sasa hivi zimethibitisha hofu yangu.

Hivi Watanzania tumekuwa waoga kiasi cha kuambia 'acha' unatii wakati ushahidi unao! Hata hivyo teknolojia inakuwa sana wataumbuka sana one day.
 
people are wrong to assume that he didn't say what he is said to have said.. and are also wrong to assume that he didn't mean what he said.
 

Ogah, asante kwa mchango wako. Unajua watu wengi hawajui uandishi wa habari ni kitu gani na hivyo wanadhani wasipoelewa kitu ni lazima walaumu taaluma yenyewe na kudhani waandishi siyo wasomi - hawajaenda shule na siyo watu makni.

Ila inabidi na sisi tuwe na uelewa na tuwe tunajiuliza maswali. Kuna mfano ninataka niutumie kuonyesha namna mojawapo waandishi wa habari wanavyoweza kuandika kitu sahihi lakini wasomaji wakaona wamepotoshwa. Ukisoma habari iliyoandikwa hivi (soma hapa chini), utasemaje waandishi ni waongo?


Juma alikuwa akiendesha gari lenye abiria 30. Mara alipata ajali saa 7 mchana na abiria 3 walikufa papo kwa hapo, 20 walikimbizwa hospitali na abiria wengine 7 walikuwa wazima.

Tuchukue kuwa habari zimewafikia waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari 3 (X,Y, Z) na kila mmoja akatuma mwandishi mmoja.

Mwandishi kutoka chombo cha habari X alifika sehemu ya ajali saa 7:10 mchana kabla maiti au majeruhi hawajapelekwa hospitali; mwingine kutoka chombo cha habari Y alifika sehemu ya ajali saa 8:30 na kukuta vijana wakisaidia kuinua gari na hivyo akaonelea aende kuuliza hospitali kujua idadi kamili ya waliokufa na majeruhi na wa mwisho kutoka chombo cha habari Z alipigiwa simu kuwa maiti 3 na majeruhi 10 wamepelekwa hospitali. Kesho yake unafikiri habari zitakazoandikwa kwenye vyombo vya habari 3 zitakuwa sawa?

Obviously, mwandishi wa habari kutoka X aliyefika saa 7:10 mchana atasema 'Ajali ya gari mchana imeua 3, imejeruhi 20 na 7 ni wazima'.

Mwandishi wa habari aliyefika saa 8:30 anaweza akaripoti karibu sawa na X kwa vile atakuta tu eye-witnesses na pengine kwa vile alifika pia hospitali anaweza kukuta majeruhi wengine 2 wamekufa. Hivyo yeye atasema, 'Ajali iliyotokea saa 7:10 imeua 5, kujeruhi 17 na 7 ni wazima'.

Mwandishi kutoka Z ataweza kwanza kufika sehemu ya ajali, kisha kwenda hospitali na baadaye kuonana na wale wazima 7. Akifika hospitali anaweza kukuta idadi ya waliokufa imeongezeka na majeruhi imepungua na pia anaweza kukuta wawili kati ya wale waliosema ni wazima wamegundua tatizo baadaye walipofika nyumbani na hivyo wakaonelea waende hospitali (kwa nia ya kulazwa kama itabidi). Kwa hiyo yeye habari yake itasomeka 'Ajali iliyotokea jana mchana, iliua watu 7, majeruhi 8 na 5 ni wazima'.

Tukio moja reporters 3 na stories 3 tofauti - lakini zote zinazungumzia tukio lilelile ila muda wa reporters kufika kwenye tukio ni tofauti na kwa vile muda ni tofauti, obviously baadhi ya details za tukio zitakuwa tofauti pia.

Wasomaji wakisoma hizi stories 3, kwa vyovyote watalaani waandishi wa habari wakidhani wamewapotosha. But in the actual sense, kila mwandishi aliripoti kitu sahihi kabisa kadiri ya ama alivyoshuhudia au kupata habari ya ajali ilivyotokea.

Mara ngapi tunasikia hoja za namna hii lakini ni nani alisha'take time' kutafakari kwa nini tukio moja linaweza kuripotiwa na watu 3 na kila mmoja akawa na details tofauti? Hivyo, tujitahidi kuilewa hii taaluma. Ni 'technical' na siyo lazima details zikiwa tofauti au habari ikiwa haijitoshelezi basi waandishi hawajui, NO. Wakati mwingine it is done purposely ili wahusika waliojaribu kuficha habari fulani watoe habari hizo wao wenyewe kwa umma.

Mfano, mwandishi akienda polisi kupata habari na akinyimwa ushirikiano ataandika bila details lakini atasema: 'Polisi alipoulizwa kuhusu habari hii alikataa kutoa ushirikiano na polisi mwenyewe atakapokabwa na wakubwa wake atasema 'Mwandishi wa habari ameni'quote' vibaya'. Kwa hiyo, inabidi tujifunze intricacies za journalism na siyo kulaumu tu bila kujua namna gani habari zinapatikana. Siyo rahisi kupata habari kwa vile watu wengi hawana ushirikiano. Kwa upande mwingine baadhi ya waandishi wa habari wana mapungufu. Lakini tusiidharau taaluma hii; inatufundisha na kutuhabarisha mengi kuliko hao wanaodhani ni wasomi kuliko waandishi wa habari wanavyotufundisha/tuhabarisha.
 
Last edited:
Hata Mwakyembe jana ame vindicate ninacho ki-guess kila siku humu kwamba waandishi ni watoto wa shule. Mwakyembe kasema mwandishi wa MwanaHALISI aliyemnukuu juzi ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Nyegezi. !

Kuhani, kama mwakyembe amesema maneno hayo basi Mwakyembe basi inabidi nihoji umakini wake wa kusoma na kufikiri. Mwandishi wa Mwanahalisi(tena si wa habari, ni wa makala) hakumnukuu Mwakyembe, alinukuu alichonukuliwa Mwakyembe na mwandishi wa Mwananchi Januari 14 kutokana na mkutano wake wa Kyela maneno ambayo Mwakyembe hakuyakanusha siku zote. (Same as Pinda, kama amenukuliwa vibaya alipaswa akanushe au ofisi yake ikanushe na kusema bayana alichokisema hasa ni nini).

Kwa hiyo:

1. Aliyeandika maneno ya Mwakyembe na kumnukuu kwenye habari ni mwandishi wa Mwananchi, ambaye si mtoto wa shule.

2. Kilichoandikwa na Mwanahalisi ni Makala ya uchambuzi ambayo ilinukuu habari ya Mwananchi, sasa badala ya kulaumu makala ya Mwanahalisi; Mwakyembe alipaswa kuihukumu habari ya Mwananchi(kama iliandika kitu ambacho hakusema) na kuhoji umakini wa Mwananchi badala ya kuhoji uhuru wa Mwanahalisi kuchapa makala ya uchambuzi.

Its crummy press or crummy politicians?

.........ndiyohiyo.
 


Kuhani:

Ushahidi huu hapa chini;

Aliyemnukuu Mwakyembe ni Mwandishi wa Mwananchi Richard Kilumbo ambaye si mtoto wa shule. Kama Mwakyembe aliona kauli hii ni ya uongo kwamba hakusema maneno hayo, angekanusha. Badala ya kumlaumu Mwanachuo Kikuu Isango Josephat(ambaye umemuita mtoto wa shule) kwa kuandika Makala ya Uchambuzi kwenye Mwanahalisi kuchambua madhara ya kauli ya Mwakyembe kama ilivyonukuliwa na Mwananchi.

Hapa ni kama Pinda, badala ya kulaumu Mwananchi na Tanzania Daima, Pinda aeleze ni ni hasa alisema sio nini alimaanisha. Akanushe hizo kauli alizonukuliwa na hayo magezeti kama hawawezi kukanusha basi wote Pinda na Mwakyembe waache umma uzijadili hizo kauli zao.


Dk. Mwakyembe awakatalia wapiga kura kuondoka CCM
Richard Kilumbo,Kyela


Chanzo: Mwananchi


Na Isango Josephat Ng'imba


Chanzo: Mwanahalisi
 

Huyu ni Waziri Mkuu wa nchi anawashauri wananchi wajichukulie sheria mkononi, anawaamuru vijana wa CCM wavunje sheria za nchi, anaonyesha dharau kwa katiba aliyoapa kuiheshimu na kwa mbwembwe na jeuri anatamka hivyo hadharani - halafu Gembe, msomi aliyebobea na anayetumia avatar ya Mwalimu, haoni uzito wala umuhimu wa kuhoji hili. Words fail me !!!
 
Umeua albino, kukata viungo vyake na nakukimbia navyo. Tunakufukuza na kukukamata, je tukupeleke polisi tusubili uhukumiwe na mahakama? Hatutaweza kusubiri, tutakuuwa tu!"

Mizengo Pinda

Umeiba fedha za umma, ukachukua na kupeleka kwenye akaunti yako ama kununua majumba ya kifahari. Tutakuvizia na kukuzunguka, je tukupeleke polisi tusubili uhukumiwe na mahakama kwa ufisadi? Hatutaweza kusubiri, tutakuzomea na kukupiga mawe tu!"

Asha Abdala
 

Asha

kama hizi kauli zinatoka kwa mwanachama mwa chama m-badala aliye mstari wa mbele kwenye strategic plan za kuhakikisha chama m-badala kinaingia chukua madaraka 2010; inaashiria kuwa huko chama m-badala hamjui au mnajua ila hamzingatii utawala wa sheria. Ni masikitiko makubwa kwa nchi yangu kama unayesema unataka kugombea uongozi huko chama mbadala unapigia debe mob justice!

Hakuna pa kukimbilia na chama kilichopo madarakani kitazidi kuitawala hii nchi miaka mingi ijayo.
 


Hebu soma tena alichoandika ukielewe - hii kansa ya kukurupuka naona inaenea kwa kasi. Please read between the lines !!!
 


Kama haya ndio yamo kwenye taaluma ya uandishi wa habari, na kama ndugu wewe ni mwandishi wa habari basi umeconfess kuwa press ya Tanzania ni crummy, na shoddy.

Yaani hapa na wewe umeponda huo uandishi vile vile, umegongelea msumari wa moto kwenye kidonda. Hivyo usiseme unatetea. Waeleze ukweli hao waandishi wajue wapi wanateleza, wajifunze na kujirekebisha.
 

Hebu soma tena alichoandika ukielewe - hii kansa ya kukurupuka naona inaenea kwa kasi. Please read between the lines !!!

haya baba, maneno ya Asha hayo, yeye na wenzie hawataweza kusubiri mafisadi wahukumiwe mahakamani, watawapiga mawe tu.
 
Last edited by a moderator:
Hawakuingia madarakani kwa nguvu, tuliwachagua sisi wenyewe.
 
haya baba, maneno ya Asha hayo, yeye na wenzie hawataweza kusubiri mafisadi wahukumiwe mahakamani, watawapiga mawe tu.

Unajua neno cynicism ? Anakebehi msimamo wa Pinda - je upo ?
 
Unajua neno cynicism ? Anakebehi msimamo wa Pinda - je upo ?

Sikuwepo, asante kunijuza. Kumbe huwa anakebehi eeh, okay, well. Kumbe hayuko serious. Nitamchukulia kikebehi-kebehi.
 
haya baba, maneno ya Asha hayo, yeye na wenzie hawataweza kusubiri mafisadi wahukumiwe mahakamani, watawapiga mawe tu.

Soma kauli ya Pinda halafu soma ya kwangu utaona kuwa ni Satire inayotaka kuonyesha ujinga wa Pinda na madhara ya kauli yake kwa mfumo mzima wa utawala wa sheria katika nchi yetu!
 

HabarindioHiyo,

Huyo mwandishi wa MwanaHALISI Mwakyembe amesema ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Nyegezi. Na akaongeza kwamba huyu mwanafunzi alichukua info zake kutoka MWANANCHI.

Sasa hapo Mwakyembe kakosea nini kuonyesha kwamba katika mlolongo wa waandishi waliosambaza hizi habari kuna vi-rookie rookie vya shule humu! Responsible journalist huwezi kuchukua nukuu iliyoandikwa na wadaku wa MWANANCHI.

Sasa Habarindiohiyo, unatetea hawa ndugu zako waandishi, hebu nambie, kuwa mzalendo dakika moja, huyu mwandishi anaeuliza hapa Pinda hasa alisema nini sio yule yule alieandika taarifa inayosambaa na kusomwa all over the place sasa hivi akidai kwamba Pinda kasema hayo maneno, halafu kumbe hana uhakika, anaenda kuuliza wabunge wa CCM ambao nao hawakuwepo, mara anakuja kuuliza jamvini, mara anatoa zawadi kwa mwenye habari, wakati ameshaandika ripoti ndeeeefu ambayo hajai-retract bado, sasa jama kazi hizo sio upotoshaji huo? No, you tell me, utanambia tuna waandishi kweli hapo?

Kibaya kinachochekesha zaidi ni kwamba habari yenyewe imetoka kwenye mkutano wa wazi halafu mwandishi anasema aliyehutubia ana mpango wa kuficha alichohutubia! Kama kimefichwa mbona ametuhabarisha kwamba kimesemwa, umejuaje?

 

hapa ndipo ninaposhangaa; ungekuwa mchambuzi mzuri ungejua kuwa habari iliyokuwa kwenye mwanakijiji.com imetoka Mwananchi na imeandikwa na Victor Kinambile wa Tabora. Tulipoiupload kuna mahali ambapo unaweka jina la mwandishi au gazeti na sehemu nyingine ina default name la m.m. mwanakijiji

Kwa makosa yetu wakati tunaipandisha hatukujaza hiyo sehemu ya kwanza na hivyo inajaza sehemu ya pili. Ni mpaka hapa ninaposoma kwako ndiyo najua kosa lilipotokea na tayari tumesahihisha. Mara nyingi watu wakiona tumesahau kuweka source wanatushtua na hivyo tunasahihisha.

Sasa hiyo habari haikuandikwa na mimi bali na Victor. Natumaini hiyo itasaidia katika uchambuzi wako ujao kwa sababu yawezekana umesoma ukiwa na mawazo "mwandishi ni mwanakijiji" and hence your scathing attacks on Tanzanian journalists which has has become a standard banner for you rightly or wrongly.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…