Wito: Wanasiasa wa upinzani, wanaharakati na wadau wengine, anzeni kampeni ya kupinga sheria hii ya Bodi ya Mikopo ndani na nje ya nchi

Wito: Wanasiasa wa upinzani, wanaharakati na wadau wengine, anzeni kampeni ya kupinga sheria hii ya Bodi ya Mikopo ndani na nje ya nchi

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Tukubali sheria ya Bodi ya Mikopo inayoruhusu makato ya asilimia 15 ya mshahara ghafi wa mtu aliepewa huu mkopo(Siwezi kumuita mnufaika wa huu mkopo maana ni kutiana umasikini) pamoja na tozo ya asilimia 6 kama retention fee, ni sheria katili, mbaya na haistahili kuwepo katika nchi ya watu wanaojitawala.

Hivyo, natoa wito kwa wanasiasa wa upinzani (CCM ndio walileta na kupitisha hii sheria katili hivyo siwahusishi), wanaharakati na wadau wengine kuungana na kuanzisha kampeni ndani na nje ya nchi kuipinga sheria hii iliyowekwa na watu ambao wamesahau walikotoka huku baadhi yao walisoma vyuo vikuu bure kabisa kwa gharama za serikali.

Ikiwezekana,tushawishi taasisi za fedha za kimataifa na nchi wahisani kusitisha mikopo na misaada kwa serikali mpaka watapobadili au kufuta kabisa hii sheria kandamizi kama walivyofanya katika kutetea haki ya mtoto wa kike kuendelea na masomo baada ya kujifungua.

Njia mojawapo iwe ni kutumia mitandao ikiwa ni pamoja na kuanzisha hashtags za kupinga uwepo wa hii sheria kwani haizingatii mishahara na vipato duni vya watanzania walio wengi.

Niseme tu, Waafrika wanastahili kuendelea kutawaliwa kwa njia kama hizi, vinginevyo tutaumizana sana.

Sijui hizi ni roho za namna gani!
 
Yaani mwanafunzi anamaliza chuo ajira hakuna, halafu unamwambia kila akipitisha muda hajamaliza kulipa deni unaongeza riba, hii maana yake tutaendelea kuwa wafungwa wa kulipa hiyo mikopo miaka yetu yote.

Kwanini serikali angalau isitoe muda fulani atleast miaka mitano ndio waanze kuweka riba ili kumpunguzia mzigo huyu mwanafunzi aliemaliza chuo asie na ajira, na wala hajui ataipata lini? japo binafsi nashauri riba iondolewe kabisa.

Riba ni sawa na wizi, kama nimetumia mfano milioni 5 kulipia gharama zangu za chuo mpaka kumaliza, kwanini nije kulipia zaidi hata ambazo sikutumia? au huu mchezo umewekwa makusudi kuwakatisha tamaa waombaji wa mikopo?

Naishauri serikali itafute vyanzo vingine vya mapato, kumkamua mwanafunzi asie na ajira mtaani ni dhambi.
 
Tukubali sheria ya Bodi ya Mikopo inayoruhusu makato ya asilimia 15 ya mshahara ghafi wa mtu aliepewa huu mkopo(Siwezi kumuita mnufaika wa huu mkopo maana ni kutiana umasikini) pamoja na tozo ya asilimia 6 kama retention fee, ni sheria katili, mbaya na haistahili kuwepo katika nchi ya watu wanaojitawala...

IMG-20210109-WA0013.jpg
 
Yaani mwanafunzi anamaliza chuo ajira hakuna, halafu unamwambia kila akipitisha muda hajamaliza kulipa deni unaongeza riba, hii maana yake tutaendelea kuwa wafungwa wa kulipa hiyo mikopo miaka yetu yote.

Kwanini serikali angalau isitoe muda fulani atleast miaka mitano ndio waanze kuweka riba ili angalau kumpunguzia mzigo huyu mwanafunzi aliemaliza chuo asie na ajira, na hajui ataipata lini?
Sometimes unajiuliza sijui ni kwanini tulidai uhuru hupati majibu.
 
Solution rahisi ingekuwa kila muajiriwa
Awe alikopeshwa au hakukopeshwa akatwe asilimia ndogo sana kama asilimia 3 ya mshahara kuchangia Bodi..

Waliokopeshwa wachangie asilimia 7..

Wangepata hela nyingi bila kuumiza watu
 
Sometimes unajiuliza sijui ni kwanini tulidai uhuru hupati majibu.
Watendaji serikalini wanatakiwa kuumiza vichwa kutafuta vyanzo vipya vya mapato, sio kila njia inayowajia kwenye vichwa vyao wanaitumia tu bila kujali athari kwa wahusika.

Wasipoangalia wazazi wataona bora wasipeleke watoto wao vyuoni kuwaepusha na hiyo misalaba mbele ya safari, mpaka pale mzazi atakapopata uwezo wa kumlipia mtoto wake masomo mwenyewe, na hii itasababisha wengi kuahirisha masomo yao kwa kuogopa mzigo wa madeni mbele ya safari.

Ngoja tuone hilo bunge la CCM peke yao kama atajitokeza wa kuzungumzia hili.
 
Solution rahisi ingekuwa kila muajiriwa
Awe alikopeshwa au hakukopeshwa akatwe asilimia ndogo sana kama asilimia 3 ya mshahara kuchangia Bodi..

Waliokopeshwa wachangie asilimia 7..

Wangepata hela nyingi bila kuumiza watu
Ukisema hata ambaye hajakopeshwa akatwe nao utakuwa ni uonevu kwa ambao hawakukopeshwa, hawastahili hiyo adhabu, mimi naona hapa serikali ikate kiasi kile kile walichokopesha wanafunzi, waondoe hiyo riba ni unyonyaji.
 
Watendaji serikalini wanatakiwa kuumiza vichwa kutafuta vyanzo vipya vya mapato, sio kila njia inayowajia kwenye vichwa vyao wanaitumia tu bila kujali athari kwa wahusika....
Watu waliopewa madaraka nchi hii hawana ubunifu na pia hawafai kuwa viongozi. Watu hawa wamegeuka mzigo kwa wanaowaongoza.
 
Walibadilisha sheria ya makato kutoka 8% mpaka 15%. Mabadiliko haya yakawahusu hadi wale ambao walikuwa wanakatwa 8% katika mshahara. Wadau walipiga kelele lakini bodi hawakujali.

Sasa wameanza tena uhabaishaji wao kwa kuongeza makato (retention fee) kitu ambacho hakipo katika mikataba ambayo tulisaini miaka hiyo mfano mkataba wa bodi wa mwaka 2009.

Bodi wanatakiwa waheshimu mikataba tuliyosainishana, mfano mkataba wao wa mwaka 2009.

Bodi wakumbuke kuwa, mabadiliko yoyote hayapaswi kuwaathiri wale ambao tayari wamo katika makubaliano ya awali.

Kukaa kwetu kimya wasidhani tunaridhika na unyanyasaji wao. La hasha! tunasubiri muda tutapata haki yetu na kulipwa fidia kubwaaa.

Ni kwamba, nimeitunza nakala ya mkataba wa bodi niliousaini mwaka 2009.

Pia, kwa sasa, kila mwezi nadownload salary slip, nazi save kwenye mtandao, pia naziprint mpaka nitakapomaliza deni mwaka 2026.Salary slip ikiwa nyeupe, itakuwa ngumu kukubali makato mengine ya bodi, bodi wakilazimisha, itabidi kwenda mahakamani.

Kutokana na kuvunja mkataba, nimepanga kuwashitaki bodi ya mikopo hata kama ni mwaka 2040! Najua ipo siku mahakama itakuwa huru. Kwahiyo, chonde chonde bodi, jaribuni kufikiria future. Mtakuja kulipa fidia kubwa huko mbeleni.

Kwa sasa mmeshika mpini tumekaa kimya ila wengine tuna jambo letu, tunakusanya ushahidi. Cha ajabu, ikifika mwaka 2040 mahakama ikiamua tulipwe pesa ndefu kama fidia, wapo watakaotuona sisi siyo wazalendo, wakati leo tunavunjiwa mikataba, na wamekaa kimyaa.

Ushauri wa bure, bodi iombeni serikali hela ya kuwakopesha wanafunzi, mana ni jukumu la serikali kuwasomesha raia wake. Mnapotaka kujiendesha ndipo mnapoanza kutubambikia madeni, mwisho wa siku tunaishi maisha ya bila furaha.
 
Binafsi nashauri wapinzani wake kimya Wala wasiwasemee mitumishi mipumbavu maana wenyewe mliisaidia ccm kuiba kura na mkawasaliti kina Lissu ambao ndio walikuwa watetezi wenu kwasasa kila mtu ashinde mechi zake Lissu alitaka.kuuwawa kwa kuwatetea nyie Mbowe kaharibiwa vitega uchumi vyake kuwatetea nyinyi wakamvunja mguu mkamwita mlevi Leo hii wanapona majeraha kwa shida walizopitia ili nyie mkombolewe mnataka kuwaita wawasaidie nooooooooo big nooooooooo Salary Slip nakuheshimu Sana ila kwa hili acheni mpate shida mpaka matako yafikiri Kama kichwa Lissu kula bata ubelgiji baba mbowe injoi utajiri wako anko na lema kaa hukohuko uliko acheni hii milofa ya Tanzania ivune ilichopanda.
 
Eti wapinzani wawasemeee mavi yenu watumishi msio na shukrani Tena hayo makato yazidi Mara alfu huku salary slip zenu zikijaa madeni ya

Maboto
Nmb
Crdb
Letshego
Faidika
ABC nk

Wapuuzi nyie.
 
Back
Top Bottom