Uongozi uliopita uliipatia fursa CCM kutumia propaganda zake chafu dhidi ya Chadema kwa kuiita mara chagadema, mara saccos na mara chama cha manyumbu!
Kwa namna hiyo chama cha majizi (CCM) kiliweza kuwashawishi baadhi ya wazalendo kusita kuhusishwa na Chadema, kuogopa kukiunga mkono na hata kukichangia.
Chadema ilihitajiwa izaliwe upya kwa umbo na sura hali ambavyo kwa miaka ishirini ilikuwa ni ile ile na watu wale wale walioridhika na kuitwa chama kikuu cha upinzani.
Kama kuna kitu mlichokosea mnaojiita G-55 ni ku-underestimate uwezo na ushawishi walio nao hawa jamaa wawili; Tundu Lissu na John Heche ndani ya Chadema!
Naomba samahani kwa kutumia hilo neno la Kiingereza, underestimate, kwa kukosa tafsiri sahihi katika Kiswahili na hivyo naomba msaada wa wanajukwaa, JF!
Kuna baadhi yetu tulifanya kautafiti kadogo na kungámua mara moja kiu ya wanaChadema kuhusu mustakhabali wa chama chao na kumuomba Mh. Mbowe apumzike.
Lahaulaa! tukajikuta ni kama tumegusa kisichogusika. Kilichopunguza hamasa ya hao wanaojiita sasa G-55 ni ile imani yao ya miaka ishirini labda kwa kuwa uliwapa fursa fulani.
Haiwezekani mbuyu uanguke hivi hivi! Hawakuwa na wasiwasi hivyo kauli, "Tunawasihi hata baada ya uchaguzi tuendelee na umoja wetu na tusiyumbishwe na matokeo!"
Baada ya uchaguzi uliofanyika mapema mwaka huu na kuingiza sura mpya katika uendeshaji wa Chadema, waliokuwa wakisita sasa wanaitikia mwito wa Chadema mpya.
Hii Chadema ya sasa ni ya watu na si Chadema itakayo kaa ikisubiri kutupiwa makombo au ruzuku kupitia wabunge wa kuchonga, Chadema sasa ni chama cha wananchi!
Uzuri wa yote ni kwamba mmeamua wenyewe kujiondoa na mimi nasisitiza...it is hightime na nawatakia heri katika safari yenu, ni haki yenu na hivyo nawaomba, nendeni kwa amani, bye!
Hawawezi kukuelewa Drlfter, na wenzao niko pale 👉
