Wito wangu kwa nyie walimu mnaodhani mna wito. Tusije laumiana baadaye

Wito wangu kwa nyie walimu mnaodhani mna wito. Tusije laumiana baadaye

Kuna mwalimu huyo pindi nasoma. Alikua anafundisha somo la biashara, yeye ilikua na mambo yake anakuja kufundisha akimaliza ni story na kusepa.

Ikifika zamu yake kusamimia wiki shule ndio wiki shule inafanyiwa usafi na wanafunzi wanapiga kazi kweli kweli.

Akikuta kuna wanafunzi wengi wanapigwa fimbo. Akishika fimbo ukifika kwake unasikia nenda nishakuchapa.

Alikua hafundishi ila ni somo wanafunzi walitumia kila njia kulielewa na kulifaulu
 
Kabisa aisee.... Nimeona yule mwalimu aliyewachapa wale watoto watukutu alivyoshambuliwa.
Anataka apate sifa za kijinga kwa ujinga wake.Mzazi nikiona unavyomkunyuga mtoto wangu,sijui kitakupata nini nikikukuta?Tabia za mtoto niachie mimi.Mwalimu kazi yako kumfundisha ajua aa,bee,chee na dee!Sikumleta shule umdunde.
 
Mkuu Walimu nchi nzima tumesainishwa mikataba ya kufuta daraja F...

Serikali imetusainisha tufute F utadhani imeleta watoto waliofaulu kumbe imewavusha..

Sasa ukisema tuwaache tu si balaa...
Kuna jambo serikali inapaswa kufanya, Kuna maagizo mengi yasiyo na tija katika elimu, mkurugenzi wa elimu ana maagizo, afisa elimu mkoa ana maagizo, afisa elimu wilaya ana maagizo. Kuna wilaya walimu wanaambiwa wafundushe Hadi saa kumi na mbili jioni, bila kujali walimu ni mama na baba wa familia wanahitaji kuhudumua familia zao.

Muda wa kazi wa serikali umeongezwa lini, kwanini mi kada ya walimu tu. Tuache walimu wafanye kazi kwa mujibu wa taaluma zao na si matamko.
 
Walimu ni punch bag... Kila anayejisikia anawapumzikia..
 
Kwa mujibu wa utafiti watanzania wengi Wana matatizo ya akili
 
Sawa tumekuelewa

Ila ukiwa na zamu lazima ushike kiboko na lazima kiboko kitembee lasivyo utaifagia shule mwenyewe na baadhi ya wanafunz wachache au ratiba za parade na kuanza vipindi vitakuwa nje ya muda
 
Mkuu Walimu nchi nzima tumesainishwa mikataba ya kufuta daraja F...

Serikali imetusainisha tufute F utadhani imeleta watoto waliofaulu kumbe imewavusha..

Sasa ukisema tuwaache tu si balaa...
Hata hiyo serikali, imeingia madaraki kwa lengo la kupunguza umaskini na kuleta maendeleo. Ila tokea Uhuru mpaka leo, wanakata viuno tu, hakuna cha maana.

Ww kama Mwalim huwezi futa F, wakati mzazi hana time na mwanae. Fanya unachoweza, umepewa kazi ya kufundisha, na sio ya kwenda vichochoroni kukamata wanafunzi wasiofika shule. Mtoto akiwa shuleni, ni jukumu lako, ila akishatoka mazingira hayo, muachie mzazi
 
Sawa tumekuelewa

Ila ukiwa na zamu lazima ushike kiboko na lazima kiboko kitembee lasivyo utaifagia shule mwenyewe na baadhi ya wanafunz wachache au ratiba za parade na kuanza vipindi vitakuwa nje ya muda
Shika kiboko chapa mwanafunzi uchukuliwe video uone moto wake. We jizime data tu uone matokeo yake. Hamjifunzi? Shauri yenu kaa na huo ujinga uone jinsi ambavyo hadi mkurugenzi wako, mkuu wa wilaya na mkoa watakavyokugeuka likitokea jambo.
 
  • Thanks
Reactions: K11
Walimu ni punch bag... Kila anayejisikia anawapumzikia..
Nadhani Kila anayetaka kung'ara ndani ya jamii na serikali anatakiwa amdhihaki mwalimu, amtishe mwalimu, amnyanyase mwalimu, bahati mbaya wengi wa wanyanyasiji wa walimu ni watu walio wahi kuwa walimu. Wanajua mazingira na ugunu wa kazi ya ualimu.

Kwa mfano Ili mwanafunzi afaulu mwalimu afundishe, mwanafunzi asome kwa bidii, ndipo yapatikane matokeo. Unapomsainisha mwalimu kuondoka f, kwa mwanafunzi asiyejali elimu unatafuta Nini kwa mwalimu?
Mgonjwa aikipewa dawa za kumeza, halafu azitupe, halafu azidiwe au afe kosa la hospital au daktari ni nini hapo?
 
Si afadhali mimi mjinga kuliko wewe falah unayedhani una jukumu la kubadilisha tabia ya watoto wa wenzio. Bwege kabisa kilaza wewe....[emoji16] Nikuone unamchapa mtoto uone nitakavyokushukia. Nitakupiga nao mpaka maji uite mma.
Shule sio sehemu ya kujifunza kuandika na kusoma tu.

Shule wanajifunza

Usafi
Nidhamu
Kazi
Utii
Stadi mbalimbali.
Tabia njema
Tunu za Taifa.

Mwalimu anao wajibu wa kuhakikisha kwamba mtoto huyo anapata hayo kwa kiwango kile kile kinachotakiwa.

Kwa namna hio viboko havikwepeki. Maana sisi waafrika bila viboko hatuelewi kabisa.

Mnawalaumu walimu bure.

Na wanasiasa kwa kushadidia mambo kutaka kujichukulia sifa nyepesi nyepesi ndio wanaharibu kabjsa.

Kama shule Haina nidhamu hio sio shule tena ni kijiwe Cha wahuni na watukutu.
 
Kwani hayo yote ni lazima upige?Hauna methodologies za ualimu wako kama mbadala wa vipigo?Kapige watoto wako ujifurahishe na kuondoa stresses zako.Asipokuwa mtii weye kama mwalimu utapunjwa mshahara wako?
 
Nadhani Kila anayetaka kung'ara ndani ya jamii na serikali anatakiwa amdhihaki mwalimu, amtishe mwalimu, amnyanyase mwalimu, bahati mbaya wengi wa wanyanyasiji wa walimu ni watu walio wahi kuwa walimu. Wanajua mazingira na ugunu wa kazi ya ualimu.

Kwa mfano Ili mwanafunzi afaulu mwalimu afundishe, mwanafunzi asome kwa bidii, ndipo yapatikane matokeo. Unapomsainisha mwalimu kuondoka f, kwa mwanafunzi asiyejali elimu unatafuta Nini kwa mwalimu?
Mgonjwa aikipewa dawa za kumeza, halafu azitupe, halafu azidiwe au afe kosa la hospital au daktari ni nini hapo?
Yote kwa yote,hapana kudunda watoto.Tumieni mbinu za kiualimu kufikia malengo.Hasira na gubu mziache kwa wenza wenu kama mnao.
 
Anataka apate sifa za kijinga kwa ujinga wake.Mzazi nikiona unavyomkunyuga mtoto wangu,sijui kitakupata nini nikikukuta?Tabia za mtoto niachie mimi.Mwalimu kazi yako kumfundisha ajua aa,bee,chee na dee!Sikumleta shule umdunde.
Siku akikuta mwanao analiwa kiboga atakuachia mwenyewe upambane nalo.

Siku walimu wakisema Wasiwazingatie wanafunzi kwa tabia na mienendo yao unadhani kama Taifa tutakuaje.

Mfano anamwona mwanao analawitiwa na wenzake yeye anauchuna.

Anamwona mwanao anavuta bangi mwalimu anakaa kimya.

Anamwona mwanao anafundishwa wizi anakaa kimya.

Halafu baada jitoto lako likishaharibikiwa unakuja tena kuwalaumu walimu kwa staili nyingine ... Oh mwalimu wanapuuza wanafunzi.... Ooh shule Haina nidhamu...

Yake masasa Tisa mwalimu anapokaa na mwanafunzi shule it means amepewa mandate kumtake care yule mtoto yaani anaplay both parts as as teacher and as a parent.

Kama kukaripia hakutoshi ni viboko tu ndio suluhisho.

Kama hutaki hizo mambo chukua mwanao mfundishe nyumbani kwako mbona rahisi sana.

Ila ukishamkabidhi mwanao shuleni usilete ujuaji na sheria za nyumbani kwako. Shule zina taratibu zake.
 
Back
Top Bottom