Wito wangu kwa nyie walimu mnaodhani mna wito. Tusije laumiana baadaye

Wito wangu kwa nyie walimu mnaodhani mna wito. Tusije laumiana baadaye

Mkuu Walimu nchi nzima tumesainishwa mikataba ya kufuta daraja F...

Serikali imetusainisha tufute F utadhani imeleta watoto waliofaulu kumbe imewavusha..

Sasa ukisema tuwaache tu si balaa...
Wakipata F watawafanya nini watawafuta kazi nchi nzima na hata ufundishaje daraja F uwezi kulikwepa kwa wanafunzi hawa . hila timiza majukumu fundisha wanaotaka kusoma watasoma tu lakini kulazimisha watoto wafate vile maadili yanataka itakua changamoto naona wazazi na wenye nchi awapo upande wa mwalimu kweli likikifika jambo utashughulikiwa kwa kebei na dharau
 
Mmeajiriwa kufundisha. Nendeni mkafundishe. Hilo ndilo jambo linalowapa mshahara. Acheni kujifanya mna uchungu sana na watoto wa wenzenu.

Huo ni wendawazimu. Nyie fundisheni tu masomo. Tabia si kazi yenu ku deal nazo. Kama mtoto ameamua kutokuja shule mwachieni hilo jukumu mzazi wake kuhangaika naye.

Kama mtoto hafanyi home work wewe mwalimu unapungukiwa na nini? Mshahara wako hulipwi? Mnajipa majukumu ambayo si yenu. Sisi wazazi hawa watoto wameshatushinda tunawaleta shule waje wakue. Pia tunalazimishwa tu na serikali sometimes.

Sasa jichanganye vibaya litokee jambo. Utajibeba. Achaneni na habari ya kusema Walimu ni wito au kujifanya mna uchungu sana na watoto wa wenzenu. Narudi nyie mkafundishe masomo. Msitoe adhabu hata kidogo. Achaneni na huo ujinga.

Yakitokea majanga mnabaki peke yenu hakuna wa kuwatetea. Mnabaki kuwa waathirika. Ni sababu ya Ujinga wenu kudhani mtawanyoosha watoto wa wenzenu ambao wameshapinda.

Mimi ningekuwa mwalimu ningekuwa naingia darasani nafundisha natoa zoezi. Watakaoleta ndiyo nitakaowasahishia. Watakaokuja shule ndiyo nitakao deal nao wasiokuwepo ni suala la wazazi husika. Nsingeshika kiboko hata siku moja. Ningewa saidia wanaotaka kusaidika. Mnashindwaje kufanya hivi?

Watoto wanapokuwa watoro,watukutu wanunulieni ice cream au cake wale.siyo kuwachapa.kama hawaandiki wanunulieni burger,sambusa,kachori n.k watapenda shule.

Lakini pia kama wengi hawafanyi kazi mnazowapa.si ndo mshukuru zoezi la kusahisha linakuwa jepesi?

Acheni ujinga wa kudhani ninyi mnaweza badilisha tabia ya mtoto ambaye wazazi wake wanaona zipo sawa. Tusije laumiana huko mbeleni.
Una point kubwa , siku hizi habari za mtoto wa mwenzio ni wako ilishaisha ! Usichape mtoto wa mtu ! Muelekeze tu akikaza fuvu achana nae kikubwa asikuvunjie heshima !! Pia zama za fimbo ziko ukingoni walimu msipokua makini utapata shida ! Malezi ni kuanzia ngazi ya familia wewe kazi yako umjaze maarifa dogo ! Mengine achia wazazi !! Halafu madogo muwaonee huruma wamekaa kinyonge sana 😂😂😂 wana mishono kila sehemu ! Unaweza ukasema utamchapa bakora moja kumbe unapiga kwenye mshono !!! Sio zama zetu uko below 40 walimu wanapanga msitari kama 15 unapita kila mmoja unakula fimbo 3 za ujazo mpaka ufike wa mwisho dadeki , mkimaliza mnaenda kong'oa visiki na kupasua kuni !!!
 
Adhabu zizingatie sheria na viwango.Kuna adhabu nyingine unapaswa kutumia akili zaidi kuliko vipigo.Si kwamba watoto wasiadhibiwe,laa hasha!Msiwapige mangumi,viboko sehemu mbaya,mara vichwa na yafananayo na hayo.Kwani wakiadhibiwa kisheria kuna shida gani?Unataka umchape mtoto fimbo za kwenye ulimi ili iweje sasa?

Mnapenda kuyakuza! Hali halisi haiko hivyo mashuleni kama ambavyo zile video zinasambaa huko mitandaoni.

Matukio yale hutokea mara moja-moja tu(Sporadic and Isolated Incidents), lakini huwa yanatumika kukashifu waalimu wote na kupenyeza ajenda za kijinga dhidi ya taifa. Hili halikubaliki hata kidogo.

Mimi sitetei ukatili dhidi ya watoto, ila ni lazima watoto waadhibiwe ili wawe na adabu. Wazazi siku hizi wanajidai kuiga Umagharibi kwenye malezi, ilhali hawafahamu kinachoendelea nyuma ya pazia.

Ila kama nilivyosema mwanzo, hutaki mtoto wako apigwe peleka akasoma GCSE, tuachieni sisi NECTA yetu.
 
Ok sawa, mimi kama mwalimu nafuata kanuni za ufundishaji, kwa maana kwamba nafundisha wanafunzi wenye utayari wa kujifunza. Hawa wanafunzi watukutu walioshindikana kupokea ushauri nasaha siwalazimishi kufanya kazi za darasani. Ya nini kupiga wanafunzi wa hivyo? Kama darasa lina wanafunzi wengi ni watukutu na mmoja ni msikivu anayefanya kazi za darasani huyo huyo anatosha kunihalalishia malipo ya mshahara wangu. By the way kichapo kitaendelea kuwepo, siwezi kulea ujinga shuleni, mzazi akija nae anachezea kichapo akafundishe mtoto wake nyumbani kwake. Siwezi kulea jamii iliyokengeuka kimaadili, lazima nitimize jukumu langu la kuonesha jamii njia nzuri katika malezi na makuzi ya mtoto
 
Kwa hali ya sasa ilivyo, ualimu hasa sekondari ni hatari ya danger! Usipowapiga wao wanakupiga! Ukiwapiga ndivyo tulivyoyasikia
Usichape mtoto shule , kama anazingua bifu lirudishe kitaa ukampe vitasa huko nje ya shule mkaupange mkono huko huko , usimwachie jeraha😂😂😂 akirudi shule atasambaza taarifa kwa madogo wenzie !!
 
Kwa jinsi walimu watakavyo Acha kuwaonya watoto inabdi niende shule niwalipe binafsi wanipgie mwanangu anapozingua ila kwa sasa walimu waache kuchapa aisee wazazi wenyewe ndo sisi ma single father na masingle mother unafikiri ata tunaweled wa malezi basi .
 
Tutafuata ushauri wako, ni kweli kufaulu au kufeli kutabaki kuwa jukumu la mwanafunzi kwa %100.
 
Ni bora wazazi na walezi waelimishwe faida ya viboko na sio kwamba viboko anavyochapwa mwanajeshi ndio achapwe mtoto Kama wewe ni mkristo soma kwenye biblia mithali 23:13(usimnyime mtoto mapigo) pia soma mithali 22:15(ujinga wa mtoto umefungwa kwenye fimbo) hata yesu aliwachapa watu ndani ya kanisa (yohana 2:12-25)
 
Back
Top Bottom